Showing posts with label Internationai news { kimataifa}. Show all posts
Showing posts with label Internationai news { kimataifa}. Show all posts

Friday, 7 October 2022

Tume ya maadili kuchunguza tuhuma za ufisadi Kenya

 Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini Kenya imesema inazifuatilia kaunti 24 kutokana na tuhuma za kuendeleza ufisadi wa kiwango cha juu.

    
Kenia | Amtseinführung Präsident William Ruto

Tume ya EACC inafuatilia matukio ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi katika kaunti 24 kati ya kaunti 47 nchini. Ripoti iliyotolewa na Tume inayosimamia mgao wa fedha na raslimali za umma nchini Kenya imeeleza kuwa serikali za kaunti zimekuwa zikipoteza mabilioni ya pesa kila mwaka kutokana na ufisadi pamoja na mifumo isio thabiti. Mwenyekiti wa tume ya EACC Eliud Wabukhala anasema :

"Tume ya EACC inatathmini hatari ilioko kwenye vitengo mbali mbali vya serikali za kaunti. Tumefanya hivyo kwenye kaunti 24 kufikia sasa.Tumegundua changamoto hizo na tukatoa ushauri kwa mianya hiyo kuzibwa, ndiposa tuweze kuokoa pesa za umma.”,alisema Wabukhala.

Tume ya EACC vilevile ina jukumu la kuchunguza na kushauri wizara, idara na kampuni za umma.

Wakati huo huo, baraza la magavana nchini limetoa wito kuwa Rais William Ruto kuagiza hazina kuu kusambaza fedha zilizotengewa serikali za kaunti kufikia jumatatu wiki ijayo.

''Hali ilivyo sasa kwenye kaunti zote 47 nchini inahuzunisha''

Kenia wartet mit Spannung auf das Urteil des Obersten Gerichtshofs zu den Wahlen

Mwenyekiti wa baraza hilo Anne Waiguru amesema kaunti zote nchini hazina pesa, na kwamba huduma na miradi muhimu imekwama. Waiguru ambaye pia ni Gavana wa kaunti ya Kirinyaga, amesema serikali za kaunti zinaidai serikali ya kitaifa shilingi billion 51.7 ya miezi ya Agosti na Septemba, na wanatarajia fedha zingine shilingi bilioni 29.6 za mwezi wa Octoba.

"Hali ilivyo sasa kwenye kaunti zote 47 nchini inahuzunisha. Inasikitisha kwamba awamu ya tatu ya uongozi wa kaunti nchini inaanza bila raslimali muhimu. Tungependa kuujulisha umma kuwa, katiba ya Kenya pamoja na sera ya fedha ya mwaka 2012 imeratibu kwamba fedha zilizotengewa serikali za kaunti zinapaswa kusambazwa kwa kaunti hizo kila tarehe 15 ya mwezi bila kuchelewa.”, alisema Waiguru.

Itakumbukwa pia kwamba Rais William Ruto alipoingia mamlakani aliiondoa wizara ya ugatuzi iliyokuwa inashughulikia maswala ya kaunti. Hii inaacha pengo katika namna kaunti zinavyofadhiliwa, na baraza la magavana limetoa wito kuwa Rais Ruto kuagiza wizara ya fedha kuwezesha usambazaji wa fedha zilizotengewa serikali za kaunti.

Ushirikiano wa taasisi

Aidha, malumbano kati ya mabunge mawili, bunge la seneti na bunge la kitaifa yameifanya vigumu kutekeleza mifumo na sera inayofaa katika ukaguzi wa raslimali za kaunti. Spika wa bunge la Seneti Amason Kingi aliahidi kuzika uhasama huu katika uongozi wake.

Mwenyekiti wa EACC Eliud Wabukala amehimiza ushirikiano kati ya mabunge ya serikali za kaunti na tume yao ili kufanikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.

Baraza la Haki la UN kumteua mchunguzi huru dhidi ya Urusi

 Schweiz Genf | Sitzung UN-Menschenrechtsrat

Baraza hilo la Haki za binadamu lenye wanachama 47 limepasisha pendekezo hilo lililowasilishwa wiki iliyopita na nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya isipokuwa Hungary. Muda mfupi kabla ya kupiga kura hiyo huko mjini Geneva, Shirika la kutetea haki za binadamu la Russia Memorial lilitajwa kuwa mshindi mwenza wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka huu wa 2022.

Pendekezo la awali lilidhihirisha wasiwasi kuhusu kufungwa kwa wingi kwa vyombo huru vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na makundi ya upinzani nchini Urusi. Wanachama walio wengi wa Baraza hilo waliafiki kuteuliwa kwa "kamati maalum" itakayoendelea kufuatilia matukio ya ukiukaji wa haki nchini Urusi, kwa kutegemea kwa kiasi fulani msaada kutoka kwa makundi ya wanaharakati wa urusi ambao bado wapo nchini humo na hata nje ya nchi.

Soma zaidi:Umoja wa Mataifa kuamua juu ya uchunguzi Ukraine 

Urusi ambayo ilikuwa mwanachama wa Baraza la Haki za binadamu hadi mapema mwaka huu kabla ya kujiondoa kwake,  imechukua hatua kadhaa za kufifiza upinzani wa ndani kutokana na vita vyake nchini ukraine, ikiwa ni pamoja na kupitisha sheria inayopiga marufuku kueneza habari "za uongo" kuhusu jeshi la Urusi. 

Soma zaidi: Urusi yasimamishwa uanachama baraza la haki za Binaadamu la UN

Idadi ya vifo Zaporizhzia yaongezeka

Ukraine | Raketenangriff auf Saporischschja

Vikosi vya zima moto vya Ukraine vikijaribu kuuzima moto baada ya shambulio huko Zaporizhzhia mnamo Oktoba 6, 2022, moja mwa matukio ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Idadi ya waliofariki kutokana na shambulio la makombora katika eneo la makazi huko Zaporizhzhia imeongezeka na kufikia watu 11 huku kwa mara ya kwanza kabisa, ndege zisizo na rubani na zilizobeba vilipuzi zimefanya mashambulizi katika mji huo wa kusini mwa Ukraine na ambako kuna kinu kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi hayo:

" Urusi imeshambulia tena kwa makombora. Kwa bahati mbaya, kuna vifo, watu waliojeruhiwa, na majengo yaliyoharibiwa. Huko Zaporizhzhia, baada ya shambulio la kwanza la roketi, wakati watu wakiondoa vifusi, Urusi ilifanya shambulio la pili la roketi. Ni uovu na ukatili wa hali ya juu. Kumekuwa na maelfu ya matukio kama haya. Na kwa bahati mbaya mengine zaidi huenda yakashuhudiwa

WAKIMBIZI ETHIOPIA WAPEWA HIFADHI

 Afrika Nahrungsmittelspende Church World Service Organisation in Marsabit

Huku makali ya kiangazi na ukame yakiendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya  Pembe ya afrika, idadi ya wahamiaji wanaotafuta chakula inaendelea kuongezeka katika eneo la Uran mpakani mwa Kenya na Ethiopia.

Familia zipatazo mia nne kutoka Ethiopia tayari zimevuka na kuingia upande wa kenya na kwa sasa zinahifadhiwa na wakaazi wa eneo la Uran.  Asili mia themanini ya wahamiaji hao ni akina mama na watoto ambao wamekuwa waathiriwa wakubwa wa baa la njaa.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa mkutano wa wadau wa kupambana na majanga jimboni Marsabit,mratibu katika shirika la World Vision Jarso James Galgallo ,amesema kuwa,kuna haja kwa serikali na wadau wengine kushikana mkono kuwasaidia wahamiaji hao ambao kwa sasa wanaishi katika mazingira duni.

"Kati ya familia mia tatu hamsini na mia nne wametoroka kwa sababu wameathirika na njaa.Mifugo waliokuwa nao wamekufa na sasa katika ile hali ya kujiokoa,wamekuja upande huu.”

''Mifugo wetu huelekea eneo la Ethiopia''

Kenia Marsabit Dürre Dromedar

Afisa huyo amesema kuwa,kuna haja ya mashirika ya kijamii kuwapa wahamiaji hao msaada, ikiwemo malazi na vyandarua vya kujikinga.

Serikali ya kaunti ya Marsabit imekiri kuwa na ufahamu kuhusu wahamiaji hao eneo la uran na kwamba imekuwa ikitoa msaada wa chakula japo hautoshi kwa wakaazi wenyewe.

Katibu wa serikali ya kaunti Ibrahim Adan Sora amesema wafugaji wamekuwa wakihamahama kutafuta malisho kwa mifugo wakati ambapo malisho yamepungua kutokana na hali mbaya ya ukame.

"Kwa sasa,tuna watu wengi eneo la Uran na hili ni kutokana na uhaba wa lishe na chakula.Hata sisi,mifugo wetu huelekea eneo la Ethiopia …”

Serikali ya kaunti aidha,imeeleza kuwa,maafisa kutoka shirika la kimataifa la kuwashugukikia wahamiaji IOM wanatarajiwa kuzuru eneo la Uran wanakohifadhiwa wahamiaji hao kabla ya kuchukua hatua zaidi.

Marsabit imeendelea kuripoti hali mbaya ya ukame huku maelfu ya wafugaji wakiendelea kuhamia katika majimbo Jirani kuokoa Maisha ya mifugo yao wakati huu

Tuzo ya Amani ya Nobel 2022 yawaendea wanaharakati wa haki za binadamu


Washindi wa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu ni mwanaharakati wa haki za binadamu Ales Bialiatski kutoka Belarus, Shirika la haki za binadamu la Memorial la nchini Urusi na shirika la uhuru wa kiraia la Ukraine.Mwenyekiti wa kamati inayosimamia tuzo hiyo ya amani yenye makao yake Norway Breit Reiss-Andersen ametangaza hayo leo mjini Oslo Norway.Tatyana Glushkova ambaye ni mwanachama wa bodi ya shirika la haki za binadamu la memorial la Urusi lililoshinda amesema tuzo hiyo ni uthibitisho kuwa kazi yao ni muhimu ulimwenguni.Reiss-Andersen amewaambia waandishi wa habari kwamba washindi hao wamefanya juhudi kubwa za kurekodi visa vya uhalifu wa kivita, ukiukwaji wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka.Maafisa wa Ulaya wamewapongeza washindi kwa kutetea haki za binadamu na demokrasia Urusi, Belarus na Ukraine.Baadhi ya viongozi waliotoa pongezi zao kwa washindi ni rais wa ufaransa Emmanuel Macron na mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg.

Thursday, 19 December 2019

Watu 6 wapoteza maisha katika mgodi wa dhahabu nchini Nigeria

Kulingana na ripoti za awali, watu 6 wamepoteza maisha katika mgodi wa dhahabu huko Plateau, nchini Nigeria


Watu 6 wapoteza maisha katika mgodi wa dhahabu  nchini Nigeria

Kulingana na ripoti za awali, watu 6 wamepoteza maisha katika mgodi wa dhahabu huko Plateau, nchini Nigeria.
Gwottson Fom, kiongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Zawan, amewaambia wanahabari kwamba kulikuwa na shimo katika mgodi huo haramu wa dhahabu katika mkoa wa Zawan,Plateau.
Karibu wafanyakazi 50 wamefunikwa  na ni  sita tu ndio wamefanikiwa kuokolewa.
Timu za utafutaji na uokoaji zinaendelea na shughuli.

Shambulizi la Boko Haram nchini Chad

Watu kumi na nne wameripotiwa kuuawa baada ya kundi la kigaidi la Boko Haram kuvamia na kushambulia kijiji

kimoja nchini Chad

Shambulizi la Boko Haram nchini Chad

Watu kumi na nne wameripotiwa kuuawa baada ya kundi la kigaidi la Boko Haram kuvamia na kushambulia kijiji kimoja nchini Chad.
Kulingana na vyombo vya habari vya Chad na Ufaransa,watu wengine watano wamejeruhiwa baada ya magaidi wa Boko Haram kuvamia na kushambulia kijiji cha wavuvi karibu na mji wa Kaiga,magharibi mwa Ziwa Chad.
Kwa mujibu wa habari,mpaka hivi sasa watu wengine kumi na watatu hawajulikani walipo.
Gavana wa eneo hilo Imouya Souabebe amebaini kuwa washambuliaji waliingia katika kijiji hicho siku iliyopita katika vikundi vidogo, na kwamba washambuliaji hao walikuwa washirika wa Boko Haram.
Zaidi ya watu 20,000 wameuawa katika vurugu za tangu 2009 ambazo zimekuwa zikifanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram, ambalo limekuwepo nchini Nigeria tangu miaka ya 2000.
Tangu mwaka 2015, kundi hilo  la kigaidi limefanya mashambulizi katika nchi jirani za mpaka wa Cameroon, Chad, Niger.
Karibu watu 2000 wamepoteza maisha katika shambulizi la Bonde la Ziwa la Chad.

Shambulizi la anga la jeshi la Israel Ukanda wa Gaza

Jeshi la Israel laendesha shambulizi  la anga dhidi ya Ukanda wa Gaza

Shambulizi la anga la jeshi la Israel Ukanda wa Gaza

Jeshi la Israel laendesha shambulizi  la anga dhidi ya Ukanda wa Gaza
Ndege za kivita za jeshi la Israel  zimeendesha mshambulizi dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Taarifa zilizotolewa na  mashuhuda katika eneo hilo zmesema kwamba mashambulizi hayo ya anga yalioendeshwa na  jeshi la Israel hayakupelekea uharibifu mkubwa.
Eneo ambalo limelenga ni  Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
Kwa  upande wake jeshi la Israel,  kombora lililorushwa  kutoka eneo hilo ndio sababu iliopelekea kuendeshwa kwa operesheni hiyo ya anga.

Idlib yapokea msaada kutoka Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa umetuma msaada wa kibinadamu kwa watu wenye mahitaji Idlib nchini Syria.


Idlib yapokea msaada kutoka Umoja wa Mataifa
Umoja wa Mataifa umetuma msaada wa kibinadamu kwa watu wenye mahitaji Idlib nchini Syria.

Kwa mujibu wa habari,malori 32 yametumwa Idlib kwa kupitia Hatay nchini Uturuki.
Msaada huo utasambazwa kwa wale wenye mahitaji Idlib,hasa katika maeneo ya vijijini.
Syria imekua katka mapigano tangu mwaka 2011

Guterres aonya juu ya chuki dhidi ya wageni na ubaguzi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema tofauti baina ya watu sio tishio bali ni utajir

Guterres aonya juu ya chuki dhidi ya wageni na ubaguzi


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN)Antonio Guterres, amesema inaonekana kuna ongezeko katika  kutoheshimu haki za binadamu ulimwenguni, “xenophobia” na  kesi za ubaguzi wa rangi pia zimeongezeka.
Guterres, ambaye yuko huko Roma, mji mkuu wa Italia kwa dhiara rasmi, alihutubia mkutano mkuu wa bunge la Italia, katika kikao maalum kilichofanyika kwa heshima yake.
Guterres alizungumzia kuhusu ubaguzi na siasa za “kipopulism”
 “Ulimwenguni kwa ujumla tunaona kuna ongezeko la kutokuheshimu haki za binadamu pamoja na ongezeko la chuki dhidi ya wageni “Xenophobia” na ubaguzi wa rangi.
Wanasiasa wa kipopulism hutumia fursa ya watu kutokuridhika kujipatia madaraka na umaarufu, Ni budi kupingana na wanasiasa wa aina hiyo kwa ujasiri na uongozi madhubuti”
 “Inahitajika muungano  wa kijamii ili kila mmoja aweze kuwa sehemu ya jamii na kuheshimu utambulisho wa kila jamii”.
Katibu mkuu aliongeza kwamba mikakati mipya inaandaliwa katika kuzilinda dini na kupiga vita lugha za chuki.
Kisha alituma salamu Ulaya. “Tunahitaji Ulya yenye nguvu, umoja na malengo kwani katika hali hiyo tofauti haziwezi kuleta changamoto”.
Kuhusiana na suala la wahamiaji haramu, Guterres alisema “ Nchi  za Mediterranea, Italia na ugiriki zina haki ya kutegemea mshikamano  na ushirikiano kutoka Umoja wa Ulaya”, Lakini mpaka hivi sasa nchi hizo hazijaona mshikamano huo.

Tuesday, 17 December 2019

Pervez Musharraf: Rais wa zamani wa Pakistan ahukumiwa kifo kwa uhaini

Jenerali Musharraf akionekana katika uchaguzi wa 2013Jenerali Pervez Musharraf, kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini Pakistan amehukumiwa kifo katika mahakama maalum mjini Islamabad.
Mahakama hiyo ya watu watatu ilimuhukumu kwa kesi ya kiwango cha juu cha uhaini baada ya kuahirishwa tangu 2013.
Jenerali Musharraf alichukuwa mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi 1999 na akahudumu kama rais wa taifa hilo kutokea mwaka 2001 hadi 2008.
Kwa sasa anaishi Dubai baada ya kuruhusiwa kuondoka nchini humo kwa matibabu 2016.
Mashtaka hayo yanahusiana na hatua ya jenerali Musharraf ya kuiahirisha katiba 2007, wakati alipoweka utawala wa dharura uliolenga kuongeza muhula wake.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76 alitoa kanda ya video akiwa katika kitanda chake hospitalini mapema mwezi huu , akielezea kwamba kesi hiyo dhidi yake haina msingi wowote.
Jenerali Musharraf ni mtawala wa kwanza wa kijeshi kufanyiwa kesi nchini Pakistan kwa kusimamaisha katiba. Uamuzi huo ulitolewa Jumanne huku watatu hao wakipiga kura 2-1 kumhukumu.

Je kesi hiyo inahusiana na nini?

Mushaarfa akilihutubia taifa Agosti 18, 2008
Wakati Nawaz Sharif - mpinzani wake ambaye alimpindua 1999 alichaguliwa kuwa waziri mkuu 2013, alianzisha kesi ya uhaini dhidi ya jenerali Musharraf na mwezi Machi 2014, jenerali huyo wa zamani alishtakiwa kwa uhaini.
Jenerali Musharraf alisema kwamba kesi hiyo ilichochewa kisiasa na kwamba hatua alizochukua 2007 zilikubaliwa na baraza la mawaziri.
Lakini hoja yake ilifutiliwa mbali na mahakama na kushutumiwa kwa kwenda kinyume chas sheria.
Kulingana na katiba ya Pakistan , mtu yeyote anayepatikana na kiwango cha juu cha uhaini anaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo.


Monday, 15 February 2016

Onyo: Ukivunja ahadi ya ndoa ni ubakaji India

Polisi nchini India wamemkamata mwanamume mmoja raia wa Scotland kwa madai ya ubakaji baada ya kuvunja ahadi ya ndoa na mwanamke aliyeshiriki ngono naye.
Mtu huyo alituhumiwa kwa kosa hilo baada ya aliyekuwa mpenziwe kumshataki kuwa amevunja ahadi ya kufunga ndoa.
Mwanamme huyo alikuwa akifanya kazi kwenye ukumbi wa mazoezi mjini Delhi na inaarifiwa kuwa alikuwa katika uhusiano na mwanadada huyo kwa muda wa miezi 5.
Baada ya mwanamme huyo kuvunja uhusiano kati yao, mwanadada huyo alimshtaki.
Anasema kuwa aliitikia kushiriki mapenzi naye kwani mwanamme huyo alimwarifu kuwa angemwoa.
 Mwanamume huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka kumi gerezani iwapo atapatikana na hatia na mahakama ya nchi hiyo.
India iko katika njia panda kuhusiana na mabadiliko ya maadili na mtazamo dhidi ya kushiriki mapenzi nje ya ndoa.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kesi kadha zinazokabiliana na kuvunjwa kwa ahadi ya ndoa na kuibua swali iwapo ni kosa la ubakaji ukishiriki ngono na mwanamke kisha uvunje ahadi ya kumuoa

Kizza Besigye azuiliwa na polisi Uganda

Mgombea urais wa chama cha upinzani cha FDC nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa na kuzuiliwa kwa muda na maafisa wa polisi mjini Kampala.
Gari lake lilikuwa likipitia barabara ya Jinja, mjini Kampala, msafara wake ukisindikizwa na mamia ya wafuasi, pale polisi walipotumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao na wakamkamata mwanasiasa huyo.
Alizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi cha Kira Road lakini akaachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka.
Polisi wanasema alikamatwa kwa sababu ya kutatiza uchukuzi mjini.
Bw Besigye alipangiwa kufanya mikutano ya kampeni katika mji huo mkuu.
Mkuu wa Polisi Jenerali Uganda Kalekezi Kayihura amethibitisha kwamba polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani lakini akakanusha habari kwamba Bw Besigye amekamatwa.

Msemaji wa polisi Fred Enanga amesema Bw Besigye alikaidi agizo la polisi la kutoingia katikati mwa mji na ndio maana akakamatwa.
“Besigye yuko huru kufanya kampeni mjini Kampala lakini sharti atii maagizo ya Tume ya Uchaguzi na Polisi ambayo yanaharamisha siasa katikati mwa jiji,” ameambia wanahabari.
Amesema alizuiwa kwa muda kutumia barabara ya Nasser na kwamba polisi walimzuilia wakihofia usalama wake baada ya kushindwa kudhibiti umati.
Hali ya wasiwasi ilitanda katika maeneo ya Kampala huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu. Watu kadha walikamatwa.
Baada ya kuachiliwa, kiongozi huyo wa upinzani aliruhusiwa kuendelea na kampeni zake hadi chuo kikuu cha Makerere huku polisi wakiendelea kushika doria.
Bw Besigye, alikuwa wakati mmoja daktari wa kibinafsi wa Bw Museveni, amekamatwa na kuzuiliwa mara nyingi lakini Jumatatu ilikuwa mara ya kwanza kukamatwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika Alhamisi.
Bw Besigye amewania urais mara tatu dhidi ya Bw Museveni bila mafanikio.

Saturday, 6 February 2016

Twitter yazifunga akaunti za IS

Mtandao wa kijamii wa Twitter, umesema kuwa umesimamisha akaunti zaidi ya 120,000 kwa uchochezi tangu katikati mwa mwaka uliopita.
Kampuni hiyo inasema akaunti nyingi zilikuwa na uhusiano mkubwa ma kundi la kigaidi la Islamic State.
Twitter walisema kuwa kutokana na hatua hiyo mawasiliano ya kigaidi imeanza kutoweka kwenye mtandao wao.

AU yaitaka Burundi kukubali wanajeshi wake

Muungano wa Afrika, AU, umetoa wito kwa viongozi wa mataifa matano kuishawishi Burundi kukubali kikosi maalum cha kudumisha amani kufuatia miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa nchini humo.
Kamati hiyo maalumu ya AU, inamshirikisha Waziri Mkuu wa Ethiopia, pamoja na Marais wa Afrika Kusini, Mauritania, Gabon na Senegal.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amepinga mpango huo, akisema huo ni uvamizi.
Uamuzi wake wa mwaka uliopita kutaka kugombea awamu ya tatu ulianzisha mapigano hayo ambapo kufikia sasa mamia ya watu wameuawa.
Image copyright
Image caption Viongozi wa Umoja wa Afrika
Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana juma lililopita walighairi juu ya swala la kuwatuma wanajeshi 5,000 wa kudumisha amani, na badala yake wakaamua kutumia njia za kidiplomasia.

Tetemeko baya lakumba Taiwan


Tetemeko kubwa la ardhi limekumba Taiwan Kusini, na kuangusha jengo moja la ghorofa 17 ambapo hadi kufikia sasa watu watatu wamethibitishwa kufariki.
Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi.

Sunday, 24 January 2016

Al Shabaab: Mwandishi akamatwa Kenya

Mwandishi mashuhuri wa habari za upekuzi nchini Kenya, amekamatwa na polisi kwa kuchapisha picha za shambulizi la kigaidi dhidi ya majeshi ya Kenya nchni Somalia.
Yassin Juma anatuhumiwa kwa kuchapisha picha za Al Shabaab zikionyesha kuchomwa kwa magari ya kijeshi.
Utawala nchini Kenya umewaonya wakenya dhidi ya kusambaza picha zilizochapishwa na Al Shabaab baada ya kuwashambulia na kuua idadi kubwa ya wanajeshi.
Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya alionya kuwa picha hizo zinahujumu usalama wa taifa.
Al Shabaab wanasema kuwa waliwaua zaidi ya wanajeshi 100 wa kenya lakini hilo halijathibitishwa.
Image captionWakenya wanaishinikiza serikali imwachilie huru mwandishi huyo wa habari
Habari za kukamatwa kwake zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuibua hamaki miongoni mwa wakenya.
Yamkini, #KOT walijitokeza kwa wingi kwenya mitandao ya kijamii na kuitaka serikali imuachilie huru mwandishi huyo chini ya kibwagizo cha#FreeYassinJuma.
Image captionKibwagizo hicho #FreeYassinJuma kinazidi kusambazwa na kufikia tulipochapisha habari hii
Kibwagizo hicho #FreeYassinJumakinazidi kusambazwa na kufikia tulipochapisha habari hii ndio kibwagizo maarufu zaidi nchini Kenya.

Iran kununua ndege 114 za Airbus

Waziri wa uchukuzi nchini Iran anasema kuwa nchi hiyo itatia sahihi kandarasi ya kununia ndege 114 aina ya Airbus.
Abbas Akhundi alinukuliwa na vyombo vya habari nchini Iran akisema kuwa kandarasi hiyo itatiwa sahihi wakati rais Hassan Rouhani atafanya ziara nchini Ufaransa siku ya Jumatano.
Hii ni baada ya kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa kufuatia mpango wa nuklia wa Iran.
Naibu wa Bwana Akhundi, pia amedokeza kuwa Iran ina hamu kubwa ya kununua ndege 100 kutoka kampuni ya Marekani, Boeing
Hiyo inafuatia kuondoshwa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran, baada ya maafikiano kuhusu udhibiti wa mradi wake wa nyuklia wa Iran.
Wakuu wa mataifa ya Magharibi na Iran, wanasema nchi hiyo itahitaji ndege kama 400 katika mwongo ujao, ili kubadilisha ndege zake zilizokuwa kongwe mno kufuatia marufuku ya miaka mingi.

Viongozi wa ANC ni mafisadi'- Goldberg

Mwanaharakati maarufu wa Afrika Kusini, Denis Goldberg, ametoa wito kuwa viongozi wa chama tawala cha ANC, waondoshwe madarakani.
Bwana Goldberg alifikishwa mahakamani pamoja na Nelson Mandela, na kutumikia kifungo cha miaka zaidi ya miaka 20 jela.
Lakin baada ya tathmini yake ya hali ya kisiasa ilivyo nchini Afrika Kusini, bwana Goldberg ameiambia idhaa ya BBC kuwa daraja zote za uongozi wa ANC, kutoka majimboni hadi ngazi za taifa, umehusika na rushwa
Kigogo huyo wa kisiasa mwenye ushawishi mkubwa ,alisema lengo lao la kujitajirisha kwa haraka kumewanyima wa-Afrika Kusini uhuru wao.

Saturday, 23 January 2016

Uchaguzi wa Haiti waahirishwa tena

Tume ya uchaguzi nchini Haiti imearisha marudio ya uchaguzi wa urais kwa miaka mitatu sasa, licha ya Rais Michel Martly kutangaza kuwa uchaguzi huo utaendelea.
Tume ya uchaguzi ilisema kuwa ilifanya uamuzi huo kutokana na ukosefu wa usalama.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi juu ya marudio ya uchaguzi huo wa Urais, kukiwa na maandamano ambapo makundi ya upinzani yamedai kuwa kuna njama ya kuiba kura.

Wanne wauawa katika ufyatulianaji risasi Canada

Polisi nchini Canada wamesema kuwa watu wanne wameuawa katika ufyatulianaji wa risasi katika shule moja katika Mkoa wa Saskachewan, katikati mwa Canada.
Ripoto za awali zilikuwa zimesema ni watu watano waliofariki.
Mshukiwa mwanamume ametiwa mbaroni nje ya Shule ya Kijamii ya Loche, ambako kisa hicho kilitokea.
Polisi pia wanaendelea kufanya uchunguzi katika tulio jingine la ufyatulianaji risasi katika kijiji cha watu 3,000 nchini humo.
Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudea, ametaja vifo hivyo kama hofu kubwa inayoweza kumkumba mzazi yeyote.
Mauaji ya watu wengi kwa bunduki nchini Canada si jambo la kawaida , ambako sheria za kuthibiti bunduki ni kali zaidi kuliko Marekani.

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...