Tuesday, 17 December 2019

Pervez Musharraf: Rais wa zamani wa Pakistan ahukumiwa kifo kwa uhaini

Jenerali Musharraf akionekana katika uchaguzi wa 2013Jenerali Pervez Musharraf, kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini Pakistan amehukumiwa kifo katika mahakama maalum mjini Islamabad.
Mahakama hiyo ya watu watatu ilimuhukumu kwa kesi ya kiwango cha juu cha uhaini baada ya kuahirishwa tangu 2013.
Jenerali Musharraf alichukuwa mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi 1999 na akahudumu kama rais wa taifa hilo kutokea mwaka 2001 hadi 2008.
Kwa sasa anaishi Dubai baada ya kuruhusiwa kuondoka nchini humo kwa matibabu 2016.
Mashtaka hayo yanahusiana na hatua ya jenerali Musharraf ya kuiahirisha katiba 2007, wakati alipoweka utawala wa dharura uliolenga kuongeza muhula wake.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76 alitoa kanda ya video akiwa katika kitanda chake hospitalini mapema mwezi huu , akielezea kwamba kesi hiyo dhidi yake haina msingi wowote.
Jenerali Musharraf ni mtawala wa kwanza wa kijeshi kufanyiwa kesi nchini Pakistan kwa kusimamaisha katiba. Uamuzi huo ulitolewa Jumanne huku watatu hao wakipiga kura 2-1 kumhukumu.

Je kesi hiyo inahusiana na nini?

Mushaarfa akilihutubia taifa Agosti 18, 2008
Wakati Nawaz Sharif - mpinzani wake ambaye alimpindua 1999 alichaguliwa kuwa waziri mkuu 2013, alianzisha kesi ya uhaini dhidi ya jenerali Musharraf na mwezi Machi 2014, jenerali huyo wa zamani alishtakiwa kwa uhaini.
Jenerali Musharraf alisema kwamba kesi hiyo ilichochewa kisiasa na kwamba hatua alizochukua 2007 zilikubaliwa na baraza la mawaziri.
Lakini hoja yake ilifutiliwa mbali na mahakama na kushutumiwa kwa kwenda kinyume chas sheria.
Kulingana na katiba ya Pakistan , mtu yeyote anayepatikana na kiwango cha juu cha uhaini anaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo.


No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...