Showing posts with label Articles/Makala. Show all posts
Showing posts with label Articles/Makala. Show all posts

Friday, 3 January 2020

Shambulio la kigaidi : Watu watatu wauwawa ndani ya basi Lamu Kenya

LIOS MEDIA
Nairobi Kenya
03/01/2020
Watu watatu wameuwawa baada ya basi la Kenya kushambuliwa karibu na mpaka wa Somalia, maafisa wameeleza.
Map of Kenya and Somalia

Watu wengine wawili wamejeruhiwa na sasa wanapata matibabu katika kliniki za jirani.
Maafisa wa usalama ambao wanajumuisha wanajeshi, askari polisi, wa askari wa wanyama pori wameanzisha dorria la kuwasaka magaidi hao.
Juhudi za kusaka kundi linalosadikiwa kuwa ni magaidi wa al-shabab, waliokimbia kuelekea msitu wa Boni bado zinaendelea.
Basi lilikuwa linasafiri kutoka Mombasa na lilishambuliwa lilipofika kaunti ya Lamu na wanaume waliolisimamisha na kulimiminia risasi.
Watu waliofanya shambulio hilo bado hawajafahamika lakini nchini Somalia, kundi la kigaidi la al-Shabab limekuwa likihusika na mashambulizi kadhaa nchini humo.
Maafisa wanasema kuwa usalama wameuimarisha ili kuhakikisha wanawakamata wahusika ambao wamekimbia.
Kenya ina jeshi nchini Somalia inalosaidia Umoja wa mataifa-UN kusaidiana na serikali kupambana na magaidi wa al-Shabab.
Nchhi hiyo imekuwa katika tahadhari kubwa wakati wa sikukuu za krismasi na mwaka mpya, baada ya taarifa za intelijensia kueleza kuwa al-Shabab wanaweza kufanya shambulizi.

Gari la kwanza kutengenezwa nchini Uturuki TOGG lazinduliwa

Gari la kwanza kutengenezwa nchini Uturuki TOGG  baada ya uzinduzi wa toleo lake la kwanza

Gari la kwanza kutengenezwa nchini Uturuki TOGG  lazinduliwa

Gari la kwanza kutengenezwa nchini Uturuki TOGG  baada ya uzinduzi wa toleo lake la kwanza , uzalishaji wake utaendelea mwaka  2022.
Uzinduzi wake  umefanyika Gebze mkoani Kocaeli rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan akihudhuria.

Athari za kulala sana kwa mwanadamu

Imebainika kuwa kulala zaidi ya masaa 9 usiku na zaidi ya dakika 90 wakati wa mchana kunaweza kuongeza hatari 


Athari za kulala sana kwa mwanadamu

imebainika kuwa kulala zaidi ya masaa 9 usiku na zaidi ya dakika 90 wakati wa mchana kunaweza kuongeza hatari ya kupigwa na kiharusi.
Matokeo haya yameonyeshwa kwenye jarida la "Neurology" lililochapishwa nchini China baada ya kuwafanyia utafiti watu 31,750 wenye umri wa takriban miaka 62.
Mwanzoni mwa utafiti, iligundulika kuwa wale ambao hawakuwa na tatizo kupooza au shida zingine kubwa za kiafya ni wale wanaolala chini ya masaa nane ukilinganisha na wale ambao hulala masaa tisa.
Hatari ya kupooza imeonekana kuongezeka  kwa asilimia 25 kwa watu ambao walipumzika kwa zaidi ya dakika 90 mchana mara kwa mara, ikilinganishwa na wale ambao walipumzika kwa saa isiyozidi moja au ambao hawakulala usiku.
Utafiti pia umebaini kuwa wale ambao hulala kwa muda mrefu usiku na kulala muda mrefu wakati wa mchana wana uwezekano wa 85% ya kupooza.
Wakati wa utafiti huo, watu walichunguzwa kwa muda wa miaka sita na 1557 kati yao walipooza kwenye harakati za kuchunguzwa.

Ndege ya jeshi la Sudani yafanya ajali, watu 18 wafariki

Watu 18 wafariki katika jali ya ndege ya jeshi Magharibi mwa eneo la Darfur

Ndege ya jeshi la Sudani yafanya ajali, watu 18 wafariki

Watu 18 wafariki katika jali ya ndege ya jeshi Magharibi mwa eneo la Darfur.
Ndege ya jeshi la Sudan  yaripotiwa kufanya ajali katika eneo la Kaskazini mwa Darfur  nchini Sudani.
Watu 18 wamefariki katika  ajali hiyo.
 Msemaji wa jeshi Amri Muhammad  amesema kuwa  ndege ya mizigo ya jeshi la taifa hilo  aina ya Antonov-12 muda mchache baada ya kaunza safari yake kutoka katika uwanja wa ndege.
Wafanya kazi 7 katika ndege hiyo , watoto wanne ni miongoni mwa watu waliofariki katika  ajali hiyo

Thursday, 19 December 2019

Utamaduni wa sherehe za kumtoa mwari una maana gani Tanzania?

Sherehe za kimilaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Katika baadhi ya mikoa kusini na Pwani ya Tanzania, suala la binti kupatiwa mafunzo maalumu ya kimila ni desturi ambayo si ngeni, wao wanaita kumtoa mwari.
Utamaduni huo ujumuisha wasichana kuwekwa ndani kwa muda wa miezi kadhaa kwa ajili ya ya kufundwa na wataalamu wa masuala hayo.
Jambo hili kwa binti ambaye hajalipitia huenda likawa na gharama kubwa katika maisha yake ya ndoa ya baadaye kwani huonekana kama vile hajui mambo mengi na zaidi yale ya kumridhisha mume wake kwa mjibu wa mila zao.
Miongoni mwa jamii inayotajwa kuendeleza mila hizi hata katika kipindi hiki cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia ni Wamakonde kutoka mikoa ya Kusini mwa Tanzania na baadhi ya wakazi wa wilaya za mkoa wa Pwani nje kidogo ya jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Aidha utamaduni huu umekuwa ukilaumiwa na baadhi ya watu kuwa ndio chanzo cha kusitisha wasichana wengi masomo wakiwa na umri mdogo,
Mara nyingi sherehe hizi pia huwa zinafanyika mara tu wasichana wanapomaliza darasa la saba(elimu ya shule ya msingi) au wengine hata kabla hawajamaliza elimu hiyo.
Ngoma za kizaramoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wazaramo ni kabila maarufu nchini Tanzania ambalo linasifika zaidi kwa ngoma.
Kuna msemo wa utani nchini humo unaowahusisha wanawake wa kabila hilo kupenda kucheza ngoma.
Lakini je, sifa hiyo wameipata kutokana na mafunzo waliyopitia?
Utaratibu wa shughuli hii ukoje na una maana gani katika jamii yao.
Mwandishi wa BBC Fatma Abdala aliweza kutembelea eneo la kisarawe mkoa wa Pwani na kutaka kufahamu zaidi juu ya utamaduni huu.
''Kwa sisi Wazaramo suala hili ni muhimu sana,na kabila letu ni moja ya makabila yanayopenda kuhakikisha kwamba wasichana wanashiriki shughuli zote na kisha kutolewa Mwali baada ya kukamilisha taratibu zote,na kwa wazaramo maandalizi ya sherehe hizo ni makubwa'' Bi Amina .
Ameongeza kuwa kuna mambo muhimu ambayo wasichana hawa hufundishwa na kungwi suala zima la mahusiano ya kawaida na watu wengine,mapenzi na ndoa kwa ujumla. mwanume kabla ya ndoa .
Mtaalamu mwingine wa shughuli hizo anabainisha kuwa mpaka mtoto anapotolewa na kuchezewa ngoma kama mali huenda akawa amekaa ndani kwa miezi kadhaa au mpaka mwaka mzima.
"Sherehe hii ni kubwa kwetu, huwa tunachanga fedha kwa ajili ya kuja katika sherehe hizo za kumcheza mwari na hata tunavaa sare", Bi.Halima anaeleza.
Licha ya kuwacheza wanawake, kabila hili nalo linawacheza wanaume yaani wanapeleka jando...ili waweze kupata mafunzo wakati wa kubalehe.
Kwa mujibu wa bi. Saada ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo ansema wanacheza mwali binti kuanzia umri wa miaka kumi, binti huyu huelekezwa unyumba namna ya kukaa na mume wake, nguo za kuvaa akiwa na mumewe, chakula cha kupika na kadhalika.
Pamoja na kuwa tamaduni hii imekuwa ikiendelee kwa miaka mingine, athari zake zimetajwa kuwa kubwa katika upande wa kuongeza idadi ya mimba za utotoni na hata kushusha maendeleo katika jamii hizo.
Hii ni kutokana na sherehe hizo pia kumuacha wazi mwali hadharani katika mavazi na hataka kuwa ishara ya kutangaza kuwa amekuwa na yuko tayari kwa wanaume.
Kwa upande wake Bi. Saum anasema kuwa hali hiyo inatokea kwa sababu wasichana wengi wanafanya tofauti na wanavyoelekezwa na hivyo kupelekea mabinti wadogo kubeba ujauzito na kubatili maana iliyolengwa.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa utamaduni ni heshima kwa mwanamke.
"Kuchezwa kuna raha yake lakini mwali wa kizaramo asipochezwa huchukuliwa kama hajakua mkubwa na hupelekea muda mwingine kukosa mume na hata kubaguliwa na wasichana wenzake waliopitia unyago," bi Halima anasisitiza.
Lios Media

Reinhard Bonnke: Mtu aliyebadilisha sura ya Ukristo barani Afrika

Reinhard BonnkeHaki miliki ya pichaEVANGELIST REINHARD BONNKE - FACEBOOK
Image captionBonnke aliwapatia changamoto wafuasi wake kuchukua kazi yake
Raia huyo ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani Reinhard Bonnke, ambaye alivutia umati mkubwa wa watu barani Afrika wakati wa mahubiri yake anaombolezwa na mamilioni ya Wakristo barani humo kufuatia kifo chake akiwa na umri wa miaka 79.
Mwandishi wa Kenya Jesse Masai anatazama ushawishi wake.
Akilinganishwa na wahubiri wengine wa Uingereza kama vile Charles Spurgeon hadi Billy Grahama wa Marekani , hadhi ya Bonke kama baba wa mahubiri ya kisasa ipo juu sana.
Katika bara la Afrika kumekuwa na mahubiri ya wiki moja , yanayoshirikisha idadi kubwa ya watu, mahema mengi , majukwaa ya kuvutia, vipaza sauti vya hali ya juu, wakalimani na mara nyingine wahubiri wakiiga jinsi Bonke alivyokuwa akifanya mahubiri yake hususan matamshi na jinsi alivyoshikilia kwa kutumia nguvu kipaza sauti.
Mwisho wa hotuba zake angewauliza ni nani kati ya walioko katika kongamano hilo alikuwa akisikia wito wa Mungu ili kuchukua kipaza sauti hicho kutoka kwa mikono yake.
Ujumbe wake wa matumaini hususan miongoni mwa mataifa ya Afrika ambayo yameathiriwa na ukame na majanga mengine ulikuwa muhimu.
Presentational grey line
Je Reinhard Bonnke alikuwa nani?
  • Alizaliwa 1940 mjini Königsberg, Ujerumani
  • Alianzisha shirika la Christ For All Nations (CFAN) 1974
  • CFAN linadai kwamba Bonnke alisaidia kuingiza takriban watu milioni 79 katika Ukristo
  • Alifariki tarehe 7 mwezi Disemba 2019
Presentational grey line
Wengine kama vile mhubiri mwenye umri wa miaka 83 wa kanisa la Pentocostal Wilson Mamboleo - ambaye alisaidia mahubiri ya Bonnke katika eneo la Afrika mashariki anadai kwamba wahubiri wakuu barani Afrika kama vile muhubiri wa Nigeria TB Joshua na Teresia Wairimu wa Kenya ni miongoni mwa walioshawishiwa na Bonnke.

'Waliokufa walifufuka'

Bonnke alijiunga na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakati wa kuanzishwa kwa kanisa la Muhubiri Wairimu la Faith Evangelistic Ministry mjini Nairobi mwezi Agosti 2016.
Shirika lake la Christ For All Nations (CFAN) , linalojulikana kwa kazi yake barani Afrika linadai Bonnke alisimamia zaidi ya watu milioni 79 katika Ukristo.
Presentational grey line
Katika mikutano mikuu ikiwemo mmoja uliofanyika katika mji wa Lagos , 2000 uliodaiwa kuvutia takriban watu milioni 1.6- Bonnke alidai kwamba ana uwezo wa kuponya kwa kutumia uwezo wa Mungu.
Pia aliwaambia wafuasi wake kwamba alishuhudia watu wakifufuka , licha ya kwamba miujiza kama hiyo ilipingwa na wakosoaji wake.

Countries with the largest Christian populations

Five of top 10 projected to be in Africa by 2050
Source: Pew Research Center
Presentational white space
Uhubiri wa Bonnke mara nyengine ulizua utata.
Stephen Mutua ambaye kati ya mwaka 1986 na 2009 alikuwa mkurugenzi wake wa kimataifa anakumbuka ghasia katika eneo la Waislamu la Kano nchini Nigeria 1990.
Waislamu walikuwa wamekasirishwa na hatua ya Bonnke kupata ruhusa ya kuhubiri katika eneo hilo.
''Katika ghasia hizo, nilijikuta katika gari ambalo haliwezi kuingia risasi kwa mara ya kwanza katika maisha yangu , kabla ya jeshi la Nigeria kutuondoa kwa ndege hadi mjini Lagos'' , Dkt Mutua anakumbuka.
Bonnke ambaye alikuwa akielewa hali ya kidini ya Nigeria , aliomboleza na taifa hilo katika ujumbe kwa serikali ya kijimbo katika eneo hilo na kuapa kurudi.
People attend the speech of German pentecostal evangelist Reinhard Bonnke during his "farewell gospel crusade", on November 9, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBonnke held more crusades in Nigeria than in any other African country
Kirasmi takriban watu wanane waliuawa lakini ripoti ambazo hazikuthibitishwa zinasema kwamba mamia ya watu walipoteza maisha yao.
''Baada ya kisa hicho tulinyimwa Visa na hatukurudi tena Nigeria kwa miaka 10''.
Dkt Mutua ambaye sasa anaongoza kanisa la African Evangalist Network mjini Nairobi, anasema kwamba mambo yalibadilika wakati rais Olesegun Obasanjo alipochukua madaraka 1999.
Anasema kwamba Nigeria, ambalo ndio taifa lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika limekuwa likimkaribisha Bonnke zaidi ya taifa jingine lolote lile la Afrika.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari , Muislamu kutoka kaskazini alimuomboleza muhubiri huyo akisema kwamba kifo chake kilikuwa hasara kubwa kwa Nigeria na dunia nzima kwa jumla.

Oloni: 'Wanaume hawafurahishwi na hatua yangu ya kusaidia kina dada kimawazo

Dami Oloniskin



Awe kwenye kilabu au ananunua visodo, Dami Oloniskin mwenye umri wa miaka 29, kutakuwa na mtu anayetafuta ushauri wake kuhusiana na maisha ya kuwa na mchumba.
"Huwa najipata nikimwambia mtu, sikiliza, kwa sasa niko katika shughuli zangu!'' Mwanablogu huyo anayefahamika kama Oloni na mashabiki wake, anacheka, ''Jana, nilienda kwenye duka la kununua dawa na kwa haraka haraka nikanunua sababu za kuoga na za kuosha nyewele, ghafla nikasikia mtu akiniita, Samahani wewe ni Oloni?'"
Oloni mwenye ushawishi mkubwa ni shangazi anayewafunda wasichana wengi. Karibia watu elfu 200 wanamfuatilia katika ukurasa wa Instagram and Twitter (CLAP BAQ QUEEN @Oloni), pamoja na (@LaidBarePodcast) na pia ana kipindi anachoendesha katika runinga.
Anapendwa kutokana na ukweli anaoangazia wakati anajibu maswali ya mashabiki wake kuhusu masuala ya uhusiano na mapenzi.
Kwa sasa anapatikana katika mtandao wa Twitter ambapo mashabiki wake wanamuandikia simuli zao nzuri na za kuvutia kuhusu mapenzi jambo ambalo limemfanya kuwa sauti na mtu wa kutegemewa na wanawake vijana.
Lakini siyo kila mtu anayefurahia hilo.
Je kinachowachukiza wapenzi kiume ni kipi?
Oloni wakati wa kipindi chake cha televisheni
Image captionOloni anatoa majibu kuhusu maswali ya mapenzi bila kuficha lolote
"Wanaume wengi wanapata hofu kwa jinsi nilivyo na uwezo wa kuwasiliana na idadi kubwa ya wanawake. "Nafikiri hawafurahishwi na ukweli wa kwamba ninapata fursa ya kuwafunza na kuwaelimisha wanawake namna ya kufanya maamuzi sahihi katika masuala ya ngono pamoja na kuwapa maarifa ya kuongeza mahaba."
Oloniskin alianzisha blogu yake kuangazia masuala ya ndoa na mahusiano mwaka 2008 alipokuwa kijana.
Lakini wakati huo, alikuwa akiandika kuhusu maisha yake na mpenzi wake, anasema, na kuangazia masuala ambayo hayakuwa rahisi kuzungumziwa kwa uwazi nchini Nigeria hasa katika familia za Kikiristo.
"Nilikuwa nafurahia sana kuzungumzia masuala ya ngono na kutaka kuelimisha wanawake kwasababu nilihisi hili ni suala ambalo halizungumziwi hasa katika jamii zetu,'' anasema.
"Watu wanafikiria kwamba ukipenda kuzungumzia mambo ya mapenzi moja kwa moja, watu wanadhani wewe ni bingwa wa ponografia. Huo si ukweli. Hii inamaanisha kwamba unaufahamu mzuri wa suala lenyewe, suala la mapenzi unaliangalia kwa mtazamo chanya na unataka kufahamisha wanawake wengine wanaokuzunguka.''
Zaidi ya miaka 10 sasa, mwanadada huyo anapokea zaidi ya maombi 100 kutoka kwa watu wanaotaka ushauri kuhusu masuala ya ngono, na namna ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye utamaduni wake ni tofauti na yeye.
Anajibu watu katika mtandao wa Instagram, kupitia blogu yake na pia anatoa ushauri kwa njia ya simu kwa malipo fulani, ili kuzungumza na watu wanaopitia changamoto katika mahusiano yao.
Kwenye Blogu, Twitter... na sasa napatikana katika Televisheni
Oloni akiwa na washiriki wa kipindi anacho endesha kwenye televisheni, Yazmine na Tyler
Image captionOloni akitoa ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yake Yazmine, Tyler (kushoto) kwenye kipindi chake cha televisheni kinachofahamika kama ''My Mate's A Bad Date''
Katika kipindi chake kipya katika kituo cha televisheni cha BBC Three, kinachofahamika kama ''My Mate's a Bad Date'', anawashauri wanawake ambao hawajaolewa kwa njia ya simu, namna ya kudumisha uchumba.
Wakati Oloni anatoa ushauri wa maswali aliyoulizwa, akaelewa kwanini baadhi ya wanaume ambao wachumba wao wanamfuata kwenye mtandao wa kijamii hawako radhi naye.
Moja ya simulizi iliyomshangaza ilikuwa ni ya yule mwanamke aliyempigia simu baada ya kugundua ameambukizwa magonjwa ya zinaa.
"Dada mmoja aliniambia kwamba amemuuliza mpenzi wake kuhusu ugonjwa wa zinaa aliyejipata nao baada ya kufanya mapenzi naye, mpenzi wake akamjibu kwamba, 'Pengine uliupata kupitia matumizi ya choo'," anakumbuka alivyomjibu hewani. 'Hapana huyo ni mwongo'."
Oloni anachukulia simulizi hizi kama ushahidi wa kwamba suala la ngono halizungumziwi kikamilifu.
Hiyo ni moja ya sababu iliyomfanya aanzishe blogu yake. Anasema alitaka kuanza kuzungumzia kwa uwazi masuala kama magonjwa ya kuambukiza na vile wanawake wanavyoweza kujitosheleza kimapenzi.
"Nahisi kwamba kwasababu ya hilo, wanawake wengi hasa kutoka jamii yangu, wanajadiliana masuala hayo bila wasiwasi na wanapokutana na mimi, wananiambia kwamba, kama si mimi, hangewahi kupata ujasiri wa kuwaambia wapenzi wao fikra zao kwa uwazi - kwa hiyo nafurahi kusikia mabadiliko yameanza kushuhudiwa."

Vile Oloni kutoka jamii ya kikirsto, Nigeria, alikuwaje mshauri wa masuala ya ngono?

Oloniskin
Image caption"Kumlazimisha mtu siyo kupata idhini yake," anasema Oloni, ambaye haogopi kuwauliza wanawake na wanaume tofauti iliyopo kati ya maneno hayo mawili
Dada huyu mwenye umri wa miaka 29, kwa sasa ana uhusiano mzuri na kina dada wanaomzidi umri na maelfu ya wanawake wengine, lakini anasema kwamba elimu ya ngono anayotoa ilimfanya atengwe na Kanisa lake.
"Hili huwa nalifananisha na filamu ya Marekani ya Mean Girls, ambapo mshauri anasema, 'Ukifanya mapenzi utakufa,' anasema.
"Nakumbuka walivyonikalisha na kunishauri kwamba niachane na mpango huu wa kufunza wanawake kuhusu ngono? kisha wakatupa mipira ya kondomu na kutuambia kwamba tusijaribu kuwataja.''
Na alipotambua athari ya kufunza elimu ya ngono kwa namna hii, mwanablogi huyu amekuwa akitoa ushauri katika shule za upili ambako mwito wake umepokelewa vizuri.
Oloni anasema mafunzo kuhusu idhini ya kukubali kufanya ngono inastahili kuendelezwa: ''Mfano ni kwenye vilabu, unapotembea mbele ya mtu, kisha akakushika kiuno, ama kama anataka kucheza na wewe lakini hakubali kuwa wewe huna haja na hilo, mambo yote haya yapo chini ya 'idhini', na hayo ndiyo mazungumzo tunayokuwanayo mashuleni

Mabibi harusi wa Sudan wanashinikizwa kukeketwa ili kuwa 'mabikra' kabla ya harusi

Bibi harusi akishikilia maua nchini SudanHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBibi harusi akishikilia maua nchini Sudan
Katika msururu wa barua kutoka Afrika, mwandishi Zeinab Mohammed Salih anaangazia swala la ukeketaji kwa mara ya pili nchini Sudan.
Short presentational grey line
Baadhi ya wanawake nchini Sudan Kusini wameamua kufanyiwa ukeketaji mwezi mmoja ama miwili kabla ya harusi yao ili 'kujifanya kuwa mabikra'.
Hili linafanyika hata ijapokuwa wengi wao tayari washafanyiwa ukeketaji wakiwa wasichana - kitu ambacho hufanyika kati ya miaka 4 na 10.
Katika taifa hilo ambalo ni la Kiislamu - ukeketaji huo unahusisha kutolewa kwa sehemu za siri na unashirikisha kushonwa ili kupunguza upana wa sehemu nyeti.
Uzi uliotumiwa kushona sehemu hiyo hukatika wakati mwanamke anaposhiriki ngono.
Iwapo mwanamke anayetarajiwa kuolewa atafanyiwa ukeketaji zaidi na mkunga , maeneo zaidi ya siri yatakatwa na kuushona uke.
Bibi harusi na bwana harusi wakicheza densi nchini SudanHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBibi harusi na bwana harusi wakicheza densi nchini Sudan

'Hataweza kutembea kwa siku kadhaa'

''Ilikuwa uchungu sana na nililazimika kwenda na kukaa na rafiki hadi nilipopona kwasababu sikutaka mamangu ajue'' , alisema Maha ambalo sio jina lake la kweli ili asitambulike.
Kukojoa lilikuwa swala tata na hakuweza kutembea kwa siku kdhaa.
Maha alifanyiwa upasuaji ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kufanyika kwa harusi yake ambapo alifaa kuolewa na mtu ambaye umri wake ni mkubwa kumliko.
''Hangeweza kuniamini iwapo angegundua kwamba nilishiriki mapenzi kabla ya ndoa yetu'', alisema. ''angenizuia kwenda nje ama hata kutumia simu''.
Msichana huyo aliyefuzu na kupata shahada kutoka chuo kikuu ana umri wa miaka 20 na anatoka katika jimbo la Kaskazini mwa Sudan ambalo linapiga marufuku ukeketaji
Presentational grey line
Lakini kitendo hicho bado kinaendelea kufanyika - ikiwa asilimia 84 ya wanawake wa Sudan walio na umri wa kati ya miaka 14 hadi 49 wamefanyiwa ukeketaji kulingana na Umoja wa Mataifa.
Na ijapokuwa Maha anafanya kazi katika mji wa Khartoum ambapo tendo hilo ni haramu aliamua kwenda nyumbani ili kukeketwa na mkunga kwa njia ya siri.
Anamjua mkunga , ambaye alikubali kufanya operesheni hiyo kwa chini ya pauni 5000 za Sudan ambazo hutozwa.

'Nakata kwasababu nahitaji fedha'

Katika tamaduni nyingi ambapo ubikra kabla ya ndoa ni muhimu , wanawake hupendelea kufanyiwa upasuaji ili kuziba uke wao, ili kuweza kuficha vitendo vyovyote vya zamani vya wao kushiriki kingono.
''Upasuaji huo hufanywa na mpasuaji na haupatikani nchini Sudan na nimeambiwa kwamba kliniki moja inatoa huduma hiyo kwa wanawake walio katika ndoa pekee. Hivyo basi kushonwa ili kupunguza upana wa uke ndio chaguo bora''.
Graphic showing infibulation, with the vagina sewn up
Image captionKwa kawaida mfumo wa Infibulation huwa ni kushona sehemu ya uke na kuacha tundu ndogo tu
Baadhi ya wakunga pia hupendelea kukata baadhi ya sehemu nyeti wakati wa upasuaji huo.
Mkunga Dkt Sawsan alisema mwanaharakati wa kukabiliana na FGM nchini Sudan anasema kwamba mabadiliko yoyote katika uke hutambulika kama ukeketaji aidha mtu awe ameshonwa ama kutobolewa.
Hatahivyo hakuna utaratibu unaoweza kufanyika hospitalini, hata Khartoum kwa kuwa baraza la matibabu nchini Sudan haliruhusu.
Litamfuta kazi mkunga yeyote atakayepatikana akitekeleza kitendo hicho na kumpokonya vifaa vyake.
Ijapokwa katika hospitali tatu nilizotembelea , wakunga walifurahia kunipatia taratibu zinazochukuliwa. Mmoja wao hata alizungumza hadharani mbele ya wauguzi wengine na kunionyesha vyumba ambavyo uketeteji unaweza kufanywa.
Presentational grey line
"Je ungependelea kukata eneo nyeti{ clitoris?} Iwapo hutaki mimi nishike .. sitashika...lakini nitakata eneo la labia na kuzishona pamoja'', alisema.
Mkunga mwengine alisema kwamba alikua tayari kufanya ukeketaji huo lakini mara nynegine alihitajika kufanya hivyo ili kuweza kupata fedha.
Niliishona njia ya uke wa msichana mwenye umri wa miaka 18, ambaye alikuwa amebakwa na binamu wake.
''Mamake alikuja hapa na kulia hivyobasi nilitaka kuwasaidia'', alisema.
''Nilikula kiapo cha kutowakata wanawake ama wasichana tena, lakini mimi hufanya hivyo mara moja moja kwa kuwa ninawalea wajukuu wangu, ambao mama yao alifariki na nahitaji kulipa karo zao za shule''.
Mradi wa Saleem uliozinduliwa 2008 unasaidiwa na Umoja wa mataifa kusitisha kitendo hicho cha FGM nchini Sudan.

Enzi mpya?

Itachukua muda mrefu kubadili tabia kama hizo hususan katika jamii ya kihafidhina.
Natumai kwamba mke wangu atakuwa bikra,aliniambia mwanamume mmoja ambaye hajaoa mjini Khartoum akisema kwamba atamshuku kufanya mapenzi na watu wengine nje iwapo hilo halitakuwa limetimia.
Mchoro unaoonesha wembe , moto, kisu na sindano
Image captionItachukua muda mrefu kubadili mtazamo kuhusuukeketaji katika jamii ya kihafidhina.
Hii ni tabia ya kawaida kote Sudan ambapo wanaume hutarajia wanawake kushonwa.
Ijapokuwa wanaharakati wa FGM wana matumaini kwamba mambo yatabadilika kutokana na hatua ya serikali mwezi uliopita kubadilisha sheria moja ya umma ambayo inadhibiti jinsi wanawake wanavyoendelea na shughuli zao za kawaida na mavazi wanayovalia mbele ya umma, ikiwemo kupiga marufuku wanawake kuvalia suruali ndefu.
Sheria hiyo ilianzishwa takriban miaka 30 ya utawala wa rais Omar al Bashir ambaye alipenduliwa akiwa rais mwaka huu kufuatia maandamano ya umma.
Chini ya sheria ya kuweka amani katika maeneo ya umma , mamlaka ilikuwa na haki ya kuamua kile ambacho wanawake wanapaswa kuvalia , wanaozungumza nao, na kazi yoyote watakayofanya- huku yeyote anayekiuka sheria hiyo akiadhibiwa kwa kuchapwa viboko ama katika visa vingine anapigwa mawe hadi kufa na hata kunyongwa.
Nahid Toubia, mwanzilishi wa An Lan - kundi la wanaharakati wa kukabiliana na ukeketaji kutoka Sudan anasema kwamba wanawake wadogo hii leo wamepiga hatua ikilinganishwa na wazazi wao.
Wanadhania kwamba wana haki ya kushiriki ngono lakini pia wanalazimika kujishona mara ya pili ama hata kuvalia Hijab kabla ya harusi yao.

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...