Sunday, 9 October 2022

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

 

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baada ya mashabiki 125 kupoteza maisha uwanjani. Zipo taarifa zingine ambazo hazijathibitishwa zikionyesha idadi ya vifo ni zaidi ya 170.

Jumamosi usiku, maelfu ya mashabiki waliingia katika uwanja wa Kanjuruhan huko Malang, Java Mashariki, kushuhudia mechi ya kandanda kati ya vilabu viwili hasimu, lakini mechi ikageuka msiba, ikawa majonzi.

Mashabiki waliokuwa uwanja wa nyumbani walivamia uwanja baada ya timu yao kufungwa 3-2 dhidi ya Persebaya Surabaya. Polisi walijaribu kuwazuia kwa kurusha mabomu ya machozi, kukawa na kimbiakimbia, kukanyagana na hatimaye wengine kupoteza maisha wakiwemo watoto kadhaa, mmoja akiwa na umri wa miaka mitatu, mamlaka inasema.

Baadhi ya mashabiki walifia mikononi mwa wachezaji waliokuwa wamefika kuwashangilia, kocha wa timu ya nyumbani Arema FC alifichua.

Tukio la Indonesia sasa linashika nafasi ya pili duniani kwa matukio ya vifo yaliyoua watu wengi uwanjani. Kuanzia tukio la mashabiki wa Liverpool mpaka wale wa Ghana, yapo mengi, lakini haya matano yalitikisa dunia.

Liverpool

5: Mwaka 1996: Mashabiki 84 wafa mbele ya rais GUATEMALA

Mashabiki 84, walipoteza maisha baada ya kuibuka kwa ghasia na kusababisha mkanyagano kwenye uwanja wa taifa wa Mateo Flores, Guatemala katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia la mwaka 1998 kati ya Guatemala na Costa Rica.

Rais wa Guatemala wakati huo, Alvaro Arzu Irigoyen, alikuwepo uwanjani na kuagiza kuvunjwa kwa mchezo huo, usiendelee, na akatangaza maombolezo ya siku 3.

''Ilikuwa mbaya -- mbaya sana,'' alisema Marlon Ivan Leon, mlinzi wa timu ya taifa ya Guatemalan wakati huo, aliyeshuhudia maiti za mashabiki hao. Watu 147 walijeruhiwa.

4: Mwaka 1988: 93 wafa wakikimbia kimbunga uwanjani, Nepal

Maelfu ya mashabiki walikuwa katika uwanja wa taifa wa Nepal wakiangalia timu yao ya taifa ikimenyana na Bangladeshi. Inaelezwa kulikuwa na zaidi ya mashabiki 30,000 uwanjani wakati kimbunga kilipotokea kilichokwenda sabamba na mvua, radi na upepo mkali.

Katika kujiokoa na kimbunga, kilichosababisha mechi kusimama, mashabiki hao walikimbilia kwenye mageti ya kutokea ili kutoka, kwa bahati mbaya ni geti moja tu lililokuwa wazi.

Kwenye kugombea kutoka kupitia geti hilo, walikanyagana, kudondoshana na wengine kukosa pumzi ambapo mashabiki 93 walifariki dunia na mamia wengine kukimbizwa hospitalini.

3: Mwaka 1989: Vifo vya mashabiki 96 wa Liver -Hillsborough

Liverpool

Hili ni tukio baya zaidi katika historia ya matukio ya uwanjani yaliyosababisha vifo nchini England, ilikuwa mwaka 1989,katika uwanja wa Hillsborough, Sheffield.

Tukio hili lilisababisha vifo vya mashabiki 96 wa Liverpool wengine wakitaja 97, waliokwenda kuhudhuria mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA Cup dhidi ya Nottingham Forest.

Kwa mashabiki wa Liverpool ni tukio lisilosahaulika na kwa zaidi ya miaka 30, waliendesha kampeni ya kujua mambo mawili tu, ilikuwaje na kwa nini mashabiki wa timu hiyo walifikwa na umauti.

2: Mwaka 2001: Mashabiki wachukizwa na kipigo, 126 wafa, Ghana

Ghana

CHANZO CHA PICHA,GHANA N

Vifo 126 katika uwanja wa michezo wa Accra, Ghana mwaka 2001, ndio tukio baya zaidi la vifo uwanjani katika bara la Afrika. Tukio lilitokea mwishoni mwa mechi kati ya Hearts of Oaks na Kumasi, ambapo mashabiki wa Kumasi walipopatwa na hasira kufuatia timu yao kufungwa, na kuanza kuvunja viti, kuvirusha na kurusha vitu vingine kama chupa.

Polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi na hapo ndipo mwanzo wa kukanyagana na kusababisha vifo hivyo.

1: Mwaka 1964: Peru - vifo vya mashabiki 320

Peru

CHANZO CHA PICHA,DAILYSTAR

Hili linatajwa kuwa tukio baya zaidi kuwahi kutokea uwanjani na kusababisha vifo vya watu 320 na wengine zaidi ya 1,000 kujeruhiwa.

Lilitokea Mai 24, 1964, katika uwanja wa taifa katika mji mkuu wa Peru, Lima - ingawa vitu vingi kuhusu tukio hilo havikuwekwa wazi sana, idadi ya vifo ilitikisa dunia.

Ikiikaribisha Argentina, Peru ilikuwa nafasi ya pili kwenye kundi lake kutoka Amerika Kusini kwa ajili ya kufuzu michuano ya Olimpiki.

Walikuwa na imani zote. Wakati wakiisubiri Brazil katika mchezo wa mwisho, Peru ilikuwa inata sare tu dhidi ya Argentina ifuzu. Argentina ilitangulia kupata bao katika uwanja uliokuwa na mashabiki zaidi ya 53,000, zaidi ya 5% ya wakazi wote wa Lima wakati huo.

Lakini utata wa bao la kusawazisha, kukataliwa baada ya mpira wa kurushwa kuzuiwa na Kilo Lobaton na kuzama langoni , mashabiki wa Peru 

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...