Showing posts with label International{ kimataifa}. Show all posts
Showing posts with label International{ kimataifa}. Show all posts

Thursday, 19 December 2019

Majibu ya maswali ya unayojiuliza juu ya uchunguzi unaomkabili Trump



President Trump was accused of abuse of power and obstruction of Congress

Donald Trump amekuwa rais wa tatu wa Marekani kufanyiwa uchunguzi unaoweza kumg'oa madarakani.
Tunajibu maswali yanayogonga vichwa wasomaji kuhusu mashtaka ya uchunguzi yaliyoletwa dhidi ya Trump.
Ni lini kesi ya Seneti itafanyika?
Bado haijafahamika, lakini makubaliano ya jumla katika Seneti huenda kesi ikaanza katika wiki ya pili ya mwezi Januari, baada ya Seneti kutoka katika mapumziko ya kipindi cha baridi na msimu wa Siku Kuu.
Hilo ndio ombi ambalo Chuck Schumer, kiongozi wa walio wachache katika bunge la seneti kupitia chama cha Democrat.
Na huku kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti kutoka chama cha Republican, Mitch McConnell anaweza kuwa hapendi mapendekezo ya wabunge wengine wa Demorat, kuhusu taratibu , huenda akakubali kuhusu kipindi hicho cha kuanza kusikiliza kesi hiyo.
Je uchunguzi huu unaweza kuwa na athari gani kwa azma ya rais Trump ya kuwania urais mwaka 2020 ikiwa atashitakiwa kulingana na vitendo alivyofanya wakati wa muhula wake wa kwanza?
Protesters in New York calling for impeachment on the eve of the House vote, 17 December 2019.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWaandamanaji mjini New York walitoa wito uchunguzi ufanyike siku moja kabla ya bunge kupiga kura
Hilo ni swali zuri zaidi - lakini halina jibu la wazi.
Republican wamekuwa wakijisifu kuwa uchunguzi umempa mtaji wa kampeni Trump na wafuasi wake wamekuwa wakimuunga mkono bega kwa bega kiongozi wao.
Democrat wao wanasema hata akishinda kwenye Bunge la Seneti, bado atabaki na doa jeusi ambalo wapiga kura hawataweza kulisahau kwenye uchaguzi wa mwakani.
Kura za maoni zilionyesha mgawanyiko mkubwa wa taifa ambalo maoni juu idadi ya wanaomuunga mkono na wanaompinga haijabadilika sana kwasababu ya uchunguzi unaoendelea.
Huendani mtu anaweza kutokua na hofu ya kusema kuwa uchaguzi wa 2020 utakuaungekua na matokeo yanayokaribiana kabla ya uchunguzi- na yatakua hivyo hivyo baada ya uchunguzi.
Ikiwa Trumpatavuliwa maadaraka na Pence (makamu wake) kuwa rais , inakubalika kisheriakwake kumteua Trump kama makamwarais, na halafu ajiuzulu?
Hakuna kitu katika katiba ya Marekani kinachozuwia hilo kufanyika, kwa hivyo inawezekana.
Kikwazo cha kwanza ni kwamba Mike Pence kumchagua Trump kuwa makamu wa rais litakua ni jambo litakalohitaji kuthibitishwa na wabunge walio wengi katika mabunge yote, la Wawakilishi na la Seneti.
Ikizingatiwa kwamba Democrat -ambayo inadhibiti bunge la wawakilishi linataka Trump achunguzwe na kushitakiwa, hilo linaonekana kuwa ni jambo ambalo huenda lisiwezekane.
Pia kuna uwezekano kwamba, kama sehemu ya tathmini yake kura ya kumuondoa madarakani, Seneti inaweza kusema kuwa Trump haruhusiwi kukalia kiti chochte cha kuchaguliwa siku zijazo.
Hilo linaweza kuzuwia yote haya kufikiwa.
Lakini kama Seneti haikufanya hilo, hakutakua na chochote cha kumzuwia Pence kujaribu karata hii.
House Representatives start debating impeaching President Donald Trump, 18 December 2019Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwanzo wa siku muhimu katika Bunge la wawakilishi
Kama Seneti haitapiga (uwezekano ni mkubwa) kura ya kumvua madarakaTrump, sasa ni nini maana ya mchakato wote huu?
Kama uliwasikiliza Democrats, sababu iliyowafanya wapitie yote haya hata kama mtazamo ni kwamba uwezekano wa Seneti (ambayo inatawaliwa na chama cha Trump, Republican) wa kumpata na hatia ni mdogo sana au haupo ni kwa sababu wanahisi wanawajibu wa kumuwajibisha rais kwa matendo yake.
Wanamtazama rais kama mtu aliyetumia vibaya mamlaka aliyonayo kuishinikiza Ukraine kufungua uchungzi dhidi ya hasimu wake wa kisiasa, na kama hawatachukua hatua - hata kama haitawezesha kuondolewa kwake madarakani - rais atalazimika kuchukua hatua zaidi ambazo zinaweza kuwa na athari kwa Democrat katika uchaguzi wa 2020.
Halafu kuna ukweli halisi wa kisiasa kwamba makao makuu ya Democrat yamekua yakijianda kwa uchunguzi huu kwa miezi kadhaa.
Kama maafisa wakuu wa Democrat wasingelichukua hatua, wangejipata katika hatari ya kuwakosa wafuasi wao - au kukabiliwa na changamoto katika uchaguzi wa majimbo au kupoteza ufuasi katika uchaguzi mkuu kwa sababu wafuasi wao wasingehisi kuwa na msukumo wa kutosha wa kurejea katika uchaguzi.
Ni kiasi gani inagharimu pesa za mlipakodi wa Marekani ?
Kama ukizungumzia garama kwa pesa tasilimu , ni vigumu kutambua ni kiasi gani. Ripoti ya uchunguzi ya Robert Mueller juu ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani iligarimu dola milioni 32, lakini uchunguzi huu wa Bung ulitegemea wafanyakazi waliopo na raslimali za bunge.
Democrat walipitisha mamia ya sheria tangu walipochukua udhibiti wa bunge la wawakilishi- udhibiti wa silaha, maadili na mageuzi ya upigaji kura, kuongeza kipato cha chini , na kuidhinisha sheria ya kudhibiti unyanyasaji dhidi ya wanawake kwa mfano, lakini ni sheria chache sana zilizopigiwa kura katika Bunge la Seneti linalod hibitiwa na Republican.

Saturday, 2 January 2016

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa afanya mazungumzo Tripoli


Matukio ya Afrika

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa afanya mazungumzo Tripoli

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya amefanya mazungumzo mjini Tripoli, akitafuta kuuhimiza utawala mjini humo kuheshimu mpango wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa inayoweza kumaliza miaka kadhaa ya umwagaji damu 

 

Matukio ya Afrika

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa afanya mazungumzo Tripoli

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya amefanya mazungumzo mjini Tripoli, akitafuta kuuhimiza utawala mjini humo kuheshimu mpango wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa inayoweza kumaliza miaka kadhaa ya umwagaji damu 

Martin Kobler, ambaye anafanya juhudi za kidiplomasia kuzishawishi serikali mbili pinzani za Libya kusaini
mpango wa kugawana madaraka, alikutana siku ya Alhamisi na wawakilishi wa serikali inayotambuliwa na jamii ya kimataifa karibu na makao yake makuu mashariki mwa nchi hiyo. Kisha jana akakutana na Nouri Abusahmein, mkuu wa bunge pinzani la Tripoli. Libya imekuwa katika machafuko tangu kuondolewa madarakani mwaka wa 2011 aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi na sas ina serikali mbili na mabunge mawili.

Makundi ya jihadi kama vile Dola la Kiislamu yamechukua nafasi hiyo ya kukosekana utawala thabiti kuingia katika ukanda wa pwani, na Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa mapigano yamewalazimu watu 435,000 kukimbia makazi yao.

Mnamo Desemba 17 mwaka jana, chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, wajumbe kutoka pande zote na viongozi kadhaa wa kibinafsi walisaini mpango wa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...