Showing posts with label Vijimambo. Show all posts
Showing posts with label Vijimambo. Show all posts

Thursday, 19 December 2019

Dawa za nywele huongeza hatari ya saratani ya matiti

Utafiti uliofanywa huko nchini Marekani umeonyesha kwamba wanawake wanaotumia dawa za nwyele wapo katika hatari kubwa ya kuugua saratani ya matiti


Dawa za nywele huongeza hatari ya saratani ya matiti

Hatari ya kupata saratani ya matiti kwa wanawake wanaotumia dawa kunyoosha na kubadili rangi nywele ni kubwa zaidi.
Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na SciTechDaily limechapisha matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya afya ya Marekani na kuchapishwa katika jarida la "International Journal of Cancer".Utafiti huo ulijumuisha wanawake elfu 46 na 709. Matokeo yalionyesha kwamba wanawake wanaotumia dawa hizo za nywele mara kwa mara wana hatari ya kupata saratani ya matiti kwa asilimia 9 zaidi ukilinganisha na wale wasiotumia.
Wanawake wenye asili ya kiafrika ambao hutumia dawa hizo za nywele kila baada ya wiki 5 hadi 8 wana ongezeko la hatari ya kupata kansa ya matiti kwa asilimia 60.

Matajiri nchini Nigeria watorosha dola bilioni 400 kuzipeleka kwenye pepo za kod

Viongozi wala rushwa, makampuni ya ndani na ya nje kwa pamoja wamekuwa wakishirikiana kutorosha mabilioni ya dola nchini Nigeria

Matajiri nchini Nigeria watorosha dola bilioni 400 kuzipeleka kwenye pepo za kodi

Imefahamika kwamba matajiri nchini Nigeria hutorosha pesa zao na kuzipeleka katika maeneo yajulikanayo kama “pepo za kodi
Mkutano wa 8  wa Umoja wa mataifa unaohusu mapambano dhidi ya uharamia na rushwa umefanyika Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. Dhima ya mkutano huo ilikuwa ukwepaji kodi.
Waziri wa sheria wa Nigeria, Abubakar Malam katika hotuba yake kwenye mkutano huo alisema kwamba matajiri wa nchini Nigeria wametorosha kiasi cha dola bilioni 400 kuzipeleka katika maeneo yajulikanayo kama “Pepo za kodi.”
Malama aliashiria kwamba viongozi wala rushwa mashirika ya ndani nay a kigeni kwa pamoja wanashirikiana katika kufanya uhalifu huo wa kutorosha pesa na kuzipeleka nje ya nchi. Katika kulidhibiti suala hilo serikali imechukua tahadhari za kutosha alisisitiza Malam

Wajinga Nyinyi: Jinsi wasanii wa Afrika Mashariki wanavyopambana kupitia vipaza sauti kuleta mabadiliko

Msanii Ney wa Mitego aliwahi kukamatwa na Basata ikapiga marufuku kabisa wimbo uliomkosoa rais Magufuli, lakini baadae rais aliagiza aachiliwe na wimbo wake uchezweHaki miliki ya pichaNEY WA MITEGO/FACEBOOK
Image captionMsanii Ney wa Mitego aliwahi kukamatwa na Basata ikapiga marufuku kabisa wimbo uongozi wa rais Magufuli, lakini baadae rais aliagiza aachiliwe na wimbo wake uchezwe
Miongoni mwa kazi za ya msanii ni kuielimisha, kuiburudisha, kuiliwaza na kuikosoa jamii na asipotekeleza hayo basi kazi yake haijakamilika.
Lakini je wasanii wa muziki wa Afrika Mashariki wameweza kuielimisha na kuikosoa jamii?.
Katika kile ambacho kilionekana kama njia ya kuikosoa na kuielimisha jamii King Kaka kwa jina lake halisi Kennedy Ombima, mwishoni mwa juma alitoa video tata ya wimbo aliouta 'Wajinga Nyinyi', akikosoa maovu miongoni mwa jamii ya Wakenya.
Katika wimbo huo amewatuhumu wazi wazi watu binafsi aliowataja majina moja kwa moja pamoja na wabunge na taasisi za umma kwa ufisadi, uliokithiri na maovu mengine katika jamii , huku akiwataka Wakenya kutafakari maovu hayo na kuyarekebisha.
Aliutumia wimbo huo huwatolea wito Wakenya kutafakari ujumbe wa video yake na kuchukua hatua.

Wimbo ulipokelewa kwa hisia tofauti

Tangu video ya wimbo huo kutoka, imekuwa ndio maarufu zaidi mitandaoni nchini Kenya .
Licha ya wimbo 'Wajinga nyinyi' ulioimbwa kwa mtindo wa rap kusifiwa na wengi kuwa maudhui yake yalikua ni ya kweli baadhi ya waliotajwa majina walimkosoa na kutishia kumshitaki.
Katika wimbo wake wenye utata 'Wajinga nyinyi' King Kaka aliwakosoa , wabunge na taasisi za umma kwa ufisadi
Image captionKatika wimbo wake wenye utata 'Wajinga nyinyi' King Kaka aliwakosoa , wabunge na taasisi za umma kwa ufisadi
King kaka alidai anatishiwa maisha na kujisalimisha katika Ofisi ya Mwendeshamashitaka mkuu wa Serikali (DCI), akidai lakini ofisi hiyo ilisema haikumuita.
Mwanamuziki huyo ambaye alipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wasanii wenzake kwa kutoa ujumbe huo, pia aliahidiwa utetezi wa kisheria na mawakili maarufu iwapo atapelekwa mahakamani kwa kuimba wimbo 'Wajinga nyinyi' .
Mbali na mwanamuziki King Kaka wanamuziki wengine wa Kenya pia awali walitoa nyimbo zilizokosoa ufisadi katika jamii yao. Mfanyo ni mwanamuziki Erick wa mtindo wa Afrobit Wainanaina katika wimbo wake 'Nchi ya kitu kidogo' na mwanamuziki wa mtindo wa Hiphop Juliani katika wimbo wake 'Sitasimama maovu yakitawala'

Hali ikoje nchini Tanzania?

Kwa muda sasa wasanii wa muziki nchini Tanzania wamekuwa wakiwasilisha ujumbe wao hususan baada ya kuingia madarakani kwa rais John Pombe Magufuli. Ukosoaji wao umekua ni ukijibu yanayofanyika nchini mwao.
Katika wimbo wake 'Iam Sorry JK'' Nikki Mbishialiongelea kuhusu namna baadhi ya Watanzania akiwemo yeye walimkosoa vibaya Kikwete alipokua mamlakani lakini sasa wanamkosa na kutamani angegombea awamu ya tatu mamlakani!.Haki miliki ya pichaNIKKI MBISHI/ FACEBOOK
Image captionKatika wimbo wake 'Iam Sorry JK'' Nikki Mbishi aliongelea kuhusu namna baadhi ya Watanzania akiwemo yeye walimkosoa vibaya Kikwete alipokua mamlakani lakini sasa wanamkosa na kutamani angegombea awamu ya tatu mamlakani!.
Wa kwanza alikua ni wanamuziki ni mwanamuziki wa Hip hop Karama Masopud na wimbo wake 'Magufuli balaa ' , al maarufu Kalapina.
Hata hivyo kalapina ambaye alishindwa katika harakatii zake za kuwania ubunge, alitoa wimbo mwingine wa kumsifu rais Magufuli. Aliimba: 'Unaweza kudhani ni ni miujiza lakini ni picha halisi. Upinani uko kimya, hauna la kusema. Amefanya walichopanga kukifanya.''
Msanii mwingine aliyekuwa na ujumbe wa ukosoaji miongo ni mwa jamii, ni mwanamuziki wa mtindo wa rap, Nikki Mbishi ambapo Januari 2017 aliimba:''I'm Sorry JK.''
Mtangulizi wa rais John Pombe Magufuli , Jakaya Kikwete, alifahamika kama 'JK'.
''Itaeleweka ikiwa nitasema siku moja kwamba, hakuna rais kama JK. Watanzania wanakukosa sanana kwa niaba ya Watanzania ninasema wanakukosa sana na wanatamani ungegombea awamu ya tatu kama rais''
Katika wimbo huo, msanii aliongelea kuhusu namna baadhi ya Watanzania akiwemo yeye walimkosoa vibaya Kikwete alipokua mamlakani lakini sasa wanamkosa na kutamani angegombea awamu ya tatu mamlakani!.
Alisema kwa sasa hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Mikopo ya wanafunzi wa Chuo Kikuu haipatikani tena kwa urahisi, uchumi unadhoofika na benki zinakabiliwa na wakati mgumu, hakuna pesa mitaani na demokrasia imebanwa, miongoni mwa mambo mengine.
Nakaaya Sumari katika wimbo wake 'Mr politician' na Mrisho Mpoto katika wimbo Mjomba'' ambao wengi wanaamini vilimlenga rais Jakaya Kikwete.Haki miliki ya pichaNAKAAYA SUMARI/ INSTAGRAM
Image captionNakaaya Sumari aliachia wimbo wake 'Mr politician' wa rais Jakaya Kikwete.
Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) lilimuita msanii huyo wa muziki wa rap na kumhoji. Baadae aliandika taarifa katika kituo cha polisi jijini Dar es salaam, na wimbo wake ukapigwa marufuku mnamo mwezi wa Februari 2017.
Kufuatia kuvamiwa kwa kituo cha TV na mshirika wa karibu wa rais, John Magufuli Paul Makonda, wasanii wa Hip hop walipeleka hasira zao juu ya kile kilichokua kikiendelea.
Ney wa Mitego alitoa wimbo, 'Wapo'. Ingawa hakutaja moja kwa moja jina lolote la kiongozi katika wimbo wake ilikua wazi kuwa alikua akielezea maeneo ambayo rais Joh Pombe Magufuli ''ameshindwa'' kutekeleza wajibu wake.
Wimbo huo ulipata umaarufu sana. Alikamatwa mara moja na Basata ikapiga marufuku kabisa wimbo huo.
Hata hivyo Jumatatu iliyofuatia, rais Magufuli aliagiza Ney aachiliwe huru na wimbo wake uchezwe.
Nyimbo nyingine zilizokosoa utawala wa rais Magufuli ni pamoja na 'Dereva wa 5 hana leseni' wa Wagosi wa Kaya, 'Usinipangie' wa Baghdad na 'Madaraka ya kulevya' wa Weusi.
Usinipangie uliimbwa kujibu kauli ya rais Magufuli kusema kuwa hatoambiwa la kufanya.

Unaweza pia kusoma:

Madaraka ya kulevya ni wimbo ambao mistari yake iliandikwa kwa ustadi lakini yenye utata. Wimbio huo haukuwazungumzia moja kwa moja rais Magufuli au Makonda , lakini maneno yaliyotumiwa yanaonyesha kumuhusu kiongozi aliyelewa mamlaka kukiuka maadili yake ya kiuongozi.
Msanii wa muziki wa rap Profesa Jay katika wimbo wake 'Ndio, mzee aalikosoa utawala wa rais Mkapa miaka ya 2000, Nakaaya Sumari katika wimbo wake Mr politician na Mrisho Mpoto katika wimbo Mjomba ambao wengi wanaamini vilimlenga rais Jakaya Kikwete.
Uganda
Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wasanii nchini Uganda walijitokeza kukosoa maovu wanayodai yanatekelezwa na utawala wa rais wa muda mrefu yoweri Museveni, huku wengine wakimsifu.
Mwaka 2012 katika wimbo wake Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine katika wimbo wake 'By Far' aliashiria nia yake ya kujiunga na siasa akiukosoa utawala wa rais Museveni.
Aliimba : 'My father said there is more politics music industry than in the Parliement, they dont know who they are dealing with' akimaanisha 'Baba yangu aliniambia kuna siasa zaidi katika muziki kuliko bungeni, lakini hawajui ninani wanaekabiliana nae'.
Bobi Wine amekua mkosoaji mkuu wa maovu katika jamii za Waganda ukosoaji wake ukiilenga zaidi serikali ya rais Museveni pamoja na viongozi wengine wa Uganda.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBobi Wine amekua mkosoaji mkuu wa maovu katika jamii za Waganda ukosoaji wake ukiilenga zaidi serikali ya rais Museveni pamoja na viongozi wengine wa Uganda.
Katika wimbo huu alielezea kuwa wakazi wa vitongoji duni kikiwemo kitongoji cha ambako alikua akiishi hawaogopi vitisho, huku akiwatolea wito raia kuamka na kupigania haki zao.
Akiimba kwa kwa lugha ya Luganda Bibi Wine, mwaka 2016, alitoa wimbo 'Dembe' au 'Amani' Msanii Bobi Wine aliouimba Bobi Wine alikemea kile alichokiita ghasia miongoni mwa viongozi wa Uganda, huku akiwalaumu kwa kuchochea ghasia hususan wakati wa uchaguzi.
Aliitaka jamii ya Waganda kupiga kura kwa amani ili kuepuka ghasia zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita, akiwatuhumu viongozi waliopo madarakani kuchochea ghasia hizo.
Imekua vigumu kutumia muziki kuelimisha na kukosoa maovu Uganda:
Nyimbo zake zilizojaa ukosoaji wa rushwa na ukosefu wa haki za kijamii nchini Uganda zilichangia kwa kiasi kikubwa kuchaguliwa kwa Bobi Wine kama mbunge wa kyadondo Mashariki mwaka 2017.
Mnamo mwaka 2017 , msanii huyo aliimba: 'Ugandans need equal opportunity', Waganda wanahitaji fursa sawa'', akitaka serikali ifikishe huduma kwa usawa miongoni mwa raia mkiwemo ajira kwa vijana.
Hata hivyo juhudi zake za kuendelea kuukosoa utawala wa rais Museveni kupitia usanii wake wa muziki zimegonga mwamba baada ya maafisa wa usalama kuzuia matamasha yake yote ya muziki.
Hivi karibuni jose Camelione (Kushoto) alitangaza kuingia siasa ili kukosoa maovu yanayofanyika Uganda, jambo lililosababisha kukosa ufuasi wa rais Yoweri Museveni katika mtandao wa kijamii wa Twitter.Haki miliki ya pichaFACEBOOK / JOSE CHAMELEONE
Image captionHivi karibuni jose Camelione (Kushoto) alitangaza kuingia siasa ili kukosoa maovu yanayofanyika Uganda, jambo lililosababisha kukosa ufuasi wa rais Yoweri Museveni katika mtandao wa kijamii wa Twitter.
Msanii wa muziki wa Hip hop na Afro bit Uganda ni Jose Chameleone kutoka nchini Uganda ambaye alifahamika kwa kutumbuiza nyimbo zake katika hafla za Chama tawala cha NRM pamoja na matukio mengine ya serikali ya rais Museveni sasa amegeuka kuwa mkosoaji wake.
Baada ya Chameleone Kutangaza nia yake ya kuingia siasa na kugombea kiti cha Meya wa Jiji Kuu Kampala ili kumaliza maovu yanayofanyika katika mji huo, rais Museveni ambaye alikua mfuasi wake katika ukurasa wa twitter alimua kuondoa ufuasi wake.
Kinyume na Bobi Wine pamoja na Jose' Chamilion, Msanii mwingine maarufu kwa jina la Bebe Cool amekua mstari wa mbele kuunga mkono utawala wa rais Yoweri Museveni, huku akiwakosoa wasanii wenzake kwa kuukosoa utawala.
Ni dhahiri kuwa wasanii wengi wa muziki katika nchi za Afrika Mashariki wamekua wakitumia kazi yao kuzielimisha na kuzikosoa jamii zao, japo katika mazingira magumu inapokuja katika ukosoaji wa kisiasa. Hata hivyo swali ni je ukosoaji huu

Oloni: 'Wanaume hawafurahishwi na hatua yangu ya kusaidia kina dada kimawazo

Dami Oloniskin



Awe kwenye kilabu au ananunua visodo, Dami Oloniskin mwenye umri wa miaka 29, kutakuwa na mtu anayetafuta ushauri wake kuhusiana na maisha ya kuwa na mchumba.
"Huwa najipata nikimwambia mtu, sikiliza, kwa sasa niko katika shughuli zangu!'' Mwanablogu huyo anayefahamika kama Oloni na mashabiki wake, anacheka, ''Jana, nilienda kwenye duka la kununua dawa na kwa haraka haraka nikanunua sababu za kuoga na za kuosha nyewele, ghafla nikasikia mtu akiniita, Samahani wewe ni Oloni?'"
Oloni mwenye ushawishi mkubwa ni shangazi anayewafunda wasichana wengi. Karibia watu elfu 200 wanamfuatilia katika ukurasa wa Instagram and Twitter (CLAP BAQ QUEEN @Oloni), pamoja na (@LaidBarePodcast) na pia ana kipindi anachoendesha katika runinga.
Anapendwa kutokana na ukweli anaoangazia wakati anajibu maswali ya mashabiki wake kuhusu masuala ya uhusiano na mapenzi.
Kwa sasa anapatikana katika mtandao wa Twitter ambapo mashabiki wake wanamuandikia simuli zao nzuri na za kuvutia kuhusu mapenzi jambo ambalo limemfanya kuwa sauti na mtu wa kutegemewa na wanawake vijana.
Lakini siyo kila mtu anayefurahia hilo.
Je kinachowachukiza wapenzi kiume ni kipi?
Oloni wakati wa kipindi chake cha televisheni
Image captionOloni anatoa majibu kuhusu maswali ya mapenzi bila kuficha lolote
"Wanaume wengi wanapata hofu kwa jinsi nilivyo na uwezo wa kuwasiliana na idadi kubwa ya wanawake. "Nafikiri hawafurahishwi na ukweli wa kwamba ninapata fursa ya kuwafunza na kuwaelimisha wanawake namna ya kufanya maamuzi sahihi katika masuala ya ngono pamoja na kuwapa maarifa ya kuongeza mahaba."
Oloniskin alianzisha blogu yake kuangazia masuala ya ndoa na mahusiano mwaka 2008 alipokuwa kijana.
Lakini wakati huo, alikuwa akiandika kuhusu maisha yake na mpenzi wake, anasema, na kuangazia masuala ambayo hayakuwa rahisi kuzungumziwa kwa uwazi nchini Nigeria hasa katika familia za Kikiristo.
"Nilikuwa nafurahia sana kuzungumzia masuala ya ngono na kutaka kuelimisha wanawake kwasababu nilihisi hili ni suala ambalo halizungumziwi hasa katika jamii zetu,'' anasema.
"Watu wanafikiria kwamba ukipenda kuzungumzia mambo ya mapenzi moja kwa moja, watu wanadhani wewe ni bingwa wa ponografia. Huo si ukweli. Hii inamaanisha kwamba unaufahamu mzuri wa suala lenyewe, suala la mapenzi unaliangalia kwa mtazamo chanya na unataka kufahamisha wanawake wengine wanaokuzunguka.''
Zaidi ya miaka 10 sasa, mwanadada huyo anapokea zaidi ya maombi 100 kutoka kwa watu wanaotaka ushauri kuhusu masuala ya ngono, na namna ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye utamaduni wake ni tofauti na yeye.
Anajibu watu katika mtandao wa Instagram, kupitia blogu yake na pia anatoa ushauri kwa njia ya simu kwa malipo fulani, ili kuzungumza na watu wanaopitia changamoto katika mahusiano yao.
Kwenye Blogu, Twitter... na sasa napatikana katika Televisheni
Oloni akiwa na washiriki wa kipindi anacho endesha kwenye televisheni, Yazmine na Tyler
Image captionOloni akitoa ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yake Yazmine, Tyler (kushoto) kwenye kipindi chake cha televisheni kinachofahamika kama ''My Mate's A Bad Date''
Katika kipindi chake kipya katika kituo cha televisheni cha BBC Three, kinachofahamika kama ''My Mate's a Bad Date'', anawashauri wanawake ambao hawajaolewa kwa njia ya simu, namna ya kudumisha uchumba.
Wakati Oloni anatoa ushauri wa maswali aliyoulizwa, akaelewa kwanini baadhi ya wanaume ambao wachumba wao wanamfuata kwenye mtandao wa kijamii hawako radhi naye.
Moja ya simulizi iliyomshangaza ilikuwa ni ya yule mwanamke aliyempigia simu baada ya kugundua ameambukizwa magonjwa ya zinaa.
"Dada mmoja aliniambia kwamba amemuuliza mpenzi wake kuhusu ugonjwa wa zinaa aliyejipata nao baada ya kufanya mapenzi naye, mpenzi wake akamjibu kwamba, 'Pengine uliupata kupitia matumizi ya choo'," anakumbuka alivyomjibu hewani. 'Hapana huyo ni mwongo'."
Oloni anachukulia simulizi hizi kama ushahidi wa kwamba suala la ngono halizungumziwi kikamilifu.
Hiyo ni moja ya sababu iliyomfanya aanzishe blogu yake. Anasema alitaka kuanza kuzungumzia kwa uwazi masuala kama magonjwa ya kuambukiza na vile wanawake wanavyoweza kujitosheleza kimapenzi.
"Nahisi kwamba kwasababu ya hilo, wanawake wengi hasa kutoka jamii yangu, wanajadiliana masuala hayo bila wasiwasi na wanapokutana na mimi, wananiambia kwamba, kama si mimi, hangewahi kupata ujasiri wa kuwaambia wapenzi wao fikra zao kwa uwazi - kwa hiyo nafurahi kusikia mabadiliko yameanza kushuhudiwa."

Vile Oloni kutoka jamii ya kikirsto, Nigeria, alikuwaje mshauri wa masuala ya ngono?

Oloniskin
Image caption"Kumlazimisha mtu siyo kupata idhini yake," anasema Oloni, ambaye haogopi kuwauliza wanawake na wanaume tofauti iliyopo kati ya maneno hayo mawili
Dada huyu mwenye umri wa miaka 29, kwa sasa ana uhusiano mzuri na kina dada wanaomzidi umri na maelfu ya wanawake wengine, lakini anasema kwamba elimu ya ngono anayotoa ilimfanya atengwe na Kanisa lake.
"Hili huwa nalifananisha na filamu ya Marekani ya Mean Girls, ambapo mshauri anasema, 'Ukifanya mapenzi utakufa,' anasema.
"Nakumbuka walivyonikalisha na kunishauri kwamba niachane na mpango huu wa kufunza wanawake kuhusu ngono? kisha wakatupa mipira ya kondomu na kutuambia kwamba tusijaribu kuwataja.''
Na alipotambua athari ya kufunza elimu ya ngono kwa namna hii, mwanablogi huyu amekuwa akitoa ushauri katika shule za upili ambako mwito wake umepokelewa vizuri.
Oloni anasema mafunzo kuhusu idhini ya kukubali kufanya ngono inastahili kuendelezwa: ''Mfano ni kwenye vilabu, unapotembea mbele ya mtu, kisha akakushika kiuno, ama kama anataka kucheza na wewe lakini hakubali kuwa wewe huna haja na hilo, mambo yote haya yapo chini ya 'idhini', na hayo ndiyo mazungumzo tunayokuwanayo mashuleni

Mabibi harusi wa Sudan wanashinikizwa kukeketwa ili kuwa 'mabikra' kabla ya harusi

Bibi harusi akishikilia maua nchini SudanHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBibi harusi akishikilia maua nchini Sudan
Katika msururu wa barua kutoka Afrika, mwandishi Zeinab Mohammed Salih anaangazia swala la ukeketaji kwa mara ya pili nchini Sudan.
Short presentational grey line
Baadhi ya wanawake nchini Sudan Kusini wameamua kufanyiwa ukeketaji mwezi mmoja ama miwili kabla ya harusi yao ili 'kujifanya kuwa mabikra'.
Hili linafanyika hata ijapokuwa wengi wao tayari washafanyiwa ukeketaji wakiwa wasichana - kitu ambacho hufanyika kati ya miaka 4 na 10.
Katika taifa hilo ambalo ni la Kiislamu - ukeketaji huo unahusisha kutolewa kwa sehemu za siri na unashirikisha kushonwa ili kupunguza upana wa sehemu nyeti.
Uzi uliotumiwa kushona sehemu hiyo hukatika wakati mwanamke anaposhiriki ngono.
Iwapo mwanamke anayetarajiwa kuolewa atafanyiwa ukeketaji zaidi na mkunga , maeneo zaidi ya siri yatakatwa na kuushona uke.
Bibi harusi na bwana harusi wakicheza densi nchini SudanHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBibi harusi na bwana harusi wakicheza densi nchini Sudan

'Hataweza kutembea kwa siku kadhaa'

''Ilikuwa uchungu sana na nililazimika kwenda na kukaa na rafiki hadi nilipopona kwasababu sikutaka mamangu ajue'' , alisema Maha ambalo sio jina lake la kweli ili asitambulike.
Kukojoa lilikuwa swala tata na hakuweza kutembea kwa siku kdhaa.
Maha alifanyiwa upasuaji ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kufanyika kwa harusi yake ambapo alifaa kuolewa na mtu ambaye umri wake ni mkubwa kumliko.
''Hangeweza kuniamini iwapo angegundua kwamba nilishiriki mapenzi kabla ya ndoa yetu'', alisema. ''angenizuia kwenda nje ama hata kutumia simu''.
Msichana huyo aliyefuzu na kupata shahada kutoka chuo kikuu ana umri wa miaka 20 na anatoka katika jimbo la Kaskazini mwa Sudan ambalo linapiga marufuku ukeketaji
Presentational grey line
Lakini kitendo hicho bado kinaendelea kufanyika - ikiwa asilimia 84 ya wanawake wa Sudan walio na umri wa kati ya miaka 14 hadi 49 wamefanyiwa ukeketaji kulingana na Umoja wa Mataifa.
Na ijapokuwa Maha anafanya kazi katika mji wa Khartoum ambapo tendo hilo ni haramu aliamua kwenda nyumbani ili kukeketwa na mkunga kwa njia ya siri.
Anamjua mkunga , ambaye alikubali kufanya operesheni hiyo kwa chini ya pauni 5000 za Sudan ambazo hutozwa.

'Nakata kwasababu nahitaji fedha'

Katika tamaduni nyingi ambapo ubikra kabla ya ndoa ni muhimu , wanawake hupendelea kufanyiwa upasuaji ili kuziba uke wao, ili kuweza kuficha vitendo vyovyote vya zamani vya wao kushiriki kingono.
''Upasuaji huo hufanywa na mpasuaji na haupatikani nchini Sudan na nimeambiwa kwamba kliniki moja inatoa huduma hiyo kwa wanawake walio katika ndoa pekee. Hivyo basi kushonwa ili kupunguza upana wa uke ndio chaguo bora''.
Graphic showing infibulation, with the vagina sewn up
Image captionKwa kawaida mfumo wa Infibulation huwa ni kushona sehemu ya uke na kuacha tundu ndogo tu
Baadhi ya wakunga pia hupendelea kukata baadhi ya sehemu nyeti wakati wa upasuaji huo.
Mkunga Dkt Sawsan alisema mwanaharakati wa kukabiliana na FGM nchini Sudan anasema kwamba mabadiliko yoyote katika uke hutambulika kama ukeketaji aidha mtu awe ameshonwa ama kutobolewa.
Hatahivyo hakuna utaratibu unaoweza kufanyika hospitalini, hata Khartoum kwa kuwa baraza la matibabu nchini Sudan haliruhusu.
Litamfuta kazi mkunga yeyote atakayepatikana akitekeleza kitendo hicho na kumpokonya vifaa vyake.
Ijapokwa katika hospitali tatu nilizotembelea , wakunga walifurahia kunipatia taratibu zinazochukuliwa. Mmoja wao hata alizungumza hadharani mbele ya wauguzi wengine na kunionyesha vyumba ambavyo uketeteji unaweza kufanywa.
Presentational grey line
"Je ungependelea kukata eneo nyeti{ clitoris?} Iwapo hutaki mimi nishike .. sitashika...lakini nitakata eneo la labia na kuzishona pamoja'', alisema.
Mkunga mwengine alisema kwamba alikua tayari kufanya ukeketaji huo lakini mara nynegine alihitajika kufanya hivyo ili kuweza kupata fedha.
Niliishona njia ya uke wa msichana mwenye umri wa miaka 18, ambaye alikuwa amebakwa na binamu wake.
''Mamake alikuja hapa na kulia hivyobasi nilitaka kuwasaidia'', alisema.
''Nilikula kiapo cha kutowakata wanawake ama wasichana tena, lakini mimi hufanya hivyo mara moja moja kwa kuwa ninawalea wajukuu wangu, ambao mama yao alifariki na nahitaji kulipa karo zao za shule''.
Mradi wa Saleem uliozinduliwa 2008 unasaidiwa na Umoja wa mataifa kusitisha kitendo hicho cha FGM nchini Sudan.

Enzi mpya?

Itachukua muda mrefu kubadili tabia kama hizo hususan katika jamii ya kihafidhina.
Natumai kwamba mke wangu atakuwa bikra,aliniambia mwanamume mmoja ambaye hajaoa mjini Khartoum akisema kwamba atamshuku kufanya mapenzi na watu wengine nje iwapo hilo halitakuwa limetimia.
Mchoro unaoonesha wembe , moto, kisu na sindano
Image captionItachukua muda mrefu kubadili mtazamo kuhusuukeketaji katika jamii ya kihafidhina.
Hii ni tabia ya kawaida kote Sudan ambapo wanaume hutarajia wanawake kushonwa.
Ijapokuwa wanaharakati wa FGM wana matumaini kwamba mambo yatabadilika kutokana na hatua ya serikali mwezi uliopita kubadilisha sheria moja ya umma ambayo inadhibiti jinsi wanawake wanavyoendelea na shughuli zao za kawaida na mavazi wanayovalia mbele ya umma, ikiwemo kupiga marufuku wanawake kuvalia suruali ndefu.
Sheria hiyo ilianzishwa takriban miaka 30 ya utawala wa rais Omar al Bashir ambaye alipenduliwa akiwa rais mwaka huu kufuatia maandamano ya umma.
Chini ya sheria ya kuweka amani katika maeneo ya umma , mamlaka ilikuwa na haki ya kuamua kile ambacho wanawake wanapaswa kuvalia , wanaozungumza nao, na kazi yoyote watakayofanya- huku yeyote anayekiuka sheria hiyo akiadhibiwa kwa kuchapwa viboko ama katika visa vingine anapigwa mawe hadi kufa na hata kunyongwa.
Nahid Toubia, mwanzilishi wa An Lan - kundi la wanaharakati wa kukabiliana na ukeketaji kutoka Sudan anasema kwamba wanawake wadogo hii leo wamepiga hatua ikilinganishwa na wazazi wao.
Wanadhania kwamba wana haki ya kushiriki ngono lakini pia wanalazimika kujishona mara ya pili ama hata kuvalia Hijab kabla ya harusi yao.

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...