Showing posts with label Sports {kimataifa}. Show all posts
Showing posts with label Sports {kimataifa}. Show all posts

Sunday, 9 October 2022

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

 

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baada ya mashabiki 125 kupoteza maisha uwanjani. Zipo taarifa zingine ambazo hazijathibitishwa zikionyesha idadi ya vifo ni zaidi ya 170.

Jumamosi usiku, maelfu ya mashabiki waliingia katika uwanja wa Kanjuruhan huko Malang, Java Mashariki, kushuhudia mechi ya kandanda kati ya vilabu viwili hasimu, lakini mechi ikageuka msiba, ikawa majonzi.

Mashabiki waliokuwa uwanja wa nyumbani walivamia uwanja baada ya timu yao kufungwa 3-2 dhidi ya Persebaya Surabaya. Polisi walijaribu kuwazuia kwa kurusha mabomu ya machozi, kukawa na kimbiakimbia, kukanyagana na hatimaye wengine kupoteza maisha wakiwemo watoto kadhaa, mmoja akiwa na umri wa miaka mitatu, mamlaka inasema.

Baadhi ya mashabiki walifia mikononi mwa wachezaji waliokuwa wamefika kuwashangilia, kocha wa timu ya nyumbani Arema FC alifichua.

Tukio la Indonesia sasa linashika nafasi ya pili duniani kwa matukio ya vifo yaliyoua watu wengi uwanjani. Kuanzia tukio la mashabiki wa Liverpool mpaka wale wa Ghana, yapo mengi, lakini haya matano yalitikisa dunia.

Liverpool

5: Mwaka 1996: Mashabiki 84 wafa mbele ya rais GUATEMALA

Mashabiki 84, walipoteza maisha baada ya kuibuka kwa ghasia na kusababisha mkanyagano kwenye uwanja wa taifa wa Mateo Flores, Guatemala katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia la mwaka 1998 kati ya Guatemala na Costa Rica.

Rais wa Guatemala wakati huo, Alvaro Arzu Irigoyen, alikuwepo uwanjani na kuagiza kuvunjwa kwa mchezo huo, usiendelee, na akatangaza maombolezo ya siku 3.

''Ilikuwa mbaya -- mbaya sana,'' alisema Marlon Ivan Leon, mlinzi wa timu ya taifa ya Guatemalan wakati huo, aliyeshuhudia maiti za mashabiki hao. Watu 147 walijeruhiwa.

4: Mwaka 1988: 93 wafa wakikimbia kimbunga uwanjani, Nepal

Maelfu ya mashabiki walikuwa katika uwanja wa taifa wa Nepal wakiangalia timu yao ya taifa ikimenyana na Bangladeshi. Inaelezwa kulikuwa na zaidi ya mashabiki 30,000 uwanjani wakati kimbunga kilipotokea kilichokwenda sabamba na mvua, radi na upepo mkali.

Katika kujiokoa na kimbunga, kilichosababisha mechi kusimama, mashabiki hao walikimbilia kwenye mageti ya kutokea ili kutoka, kwa bahati mbaya ni geti moja tu lililokuwa wazi.

Kwenye kugombea kutoka kupitia geti hilo, walikanyagana, kudondoshana na wengine kukosa pumzi ambapo mashabiki 93 walifariki dunia na mamia wengine kukimbizwa hospitalini.

3: Mwaka 1989: Vifo vya mashabiki 96 wa Liver -Hillsborough

Liverpool

Hili ni tukio baya zaidi katika historia ya matukio ya uwanjani yaliyosababisha vifo nchini England, ilikuwa mwaka 1989,katika uwanja wa Hillsborough, Sheffield.

Tukio hili lilisababisha vifo vya mashabiki 96 wa Liverpool wengine wakitaja 97, waliokwenda kuhudhuria mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA Cup dhidi ya Nottingham Forest.

Kwa mashabiki wa Liverpool ni tukio lisilosahaulika na kwa zaidi ya miaka 30, waliendesha kampeni ya kujua mambo mawili tu, ilikuwaje na kwa nini mashabiki wa timu hiyo walifikwa na umauti.

2: Mwaka 2001: Mashabiki wachukizwa na kipigo, 126 wafa, Ghana

Ghana

CHANZO CHA PICHA,GHANA N

Vifo 126 katika uwanja wa michezo wa Accra, Ghana mwaka 2001, ndio tukio baya zaidi la vifo uwanjani katika bara la Afrika. Tukio lilitokea mwishoni mwa mechi kati ya Hearts of Oaks na Kumasi, ambapo mashabiki wa Kumasi walipopatwa na hasira kufuatia timu yao kufungwa, na kuanza kuvunja viti, kuvirusha na kurusha vitu vingine kama chupa.

Polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi na hapo ndipo mwanzo wa kukanyagana na kusababisha vifo hivyo.

1: Mwaka 1964: Peru - vifo vya mashabiki 320

Peru

CHANZO CHA PICHA,DAILYSTAR

Hili linatajwa kuwa tukio baya zaidi kuwahi kutokea uwanjani na kusababisha vifo vya watu 320 na wengine zaidi ya 1,000 kujeruhiwa.

Lilitokea Mai 24, 1964, katika uwanja wa taifa katika mji mkuu wa Peru, Lima - ingawa vitu vingi kuhusu tukio hilo havikuwekwa wazi sana, idadi ya vifo ilitikisa dunia.

Ikiikaribisha Argentina, Peru ilikuwa nafasi ya pili kwenye kundi lake kutoka Amerika Kusini kwa ajili ya kufuzu michuano ya Olimpiki.

Walikuwa na imani zote. Wakati wakiisubiri Brazil katika mchezo wa mwisho, Peru ilikuwa inata sare tu dhidi ya Argentina ifuzu. Argentina ilitangulia kupata bao katika uwanja uliokuwa na mashabiki zaidi ya 53,000, zaidi ya 5% ya wakazi wote wa Lima wakati huo.

Lakini utata wa bao la kusawazisha, kukataliwa baada ya mpira wa kurushwa kuzuiwa na Kilo Lobaton na kuzama langoni , mashabiki wa Peru 

Friday, 3 January 2020

Liverpool 2-0 Sheffield United: Reds wacheza ligi ya Premia bila kufungwa mwaka mzima

LIOS MEDIA
England
03/01/2020
Liverpool,imeshikilia uongozi wa ligi kuu ya England kwa mwaka mzima bila kufungwa baada ya Sheffield United kugaragazwa uwanjani Anfield.

Mohamed Salah and Sadio Mane

The Reds walipata ushindi wa mapema kupita Mohamed Salah katika dakika ya nne kutoka kwa pasi fupi kutoka kwa Andy Robertson.
Lakini hakuna bahati yoyote katika ushindi wao pale Sadio Mane alipofunga bao la pili baada ya Salah kukosa nafasi hiyo.
Majogoo wa Jiji Liverpool, waliweza kuweka mwanya huo wa alama 13 baada ya wapizani wake wa karibu Leicester na Manchester City kujipatia ushindi katika mechi za mwaka mpya.
Mohamed SalahHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMohamed Salah alifunga dhidi ya timu 22 kati wapinzani 25 wa ligi ya Premia aliopambana nao kama mchezaji wa Liverpool, na kushindwa kufunga bao dhidi ya Manchester United, Swansea na Aston Villa
Upande huo unaogozwa na Jurgen Klopp ulishuka kwa alama mbili wakiwa na alama 58 badala ya alama 60 msimu huu.
Kwa upande wa Chris Wilder ulikuwa wa kushindwa wa pili mfululizo kushindwa, lakini wamesalia wakakamavu na kuwa nambari sita katika jeduli ya ligi ya Premia na alama 29.
Ushindi wa Liverpool dhidi ya Sheffield United umeweka historia ya kuwa miongoni mwa timu ambazo hazijafungwa kwa mwaka mmoja katika ligi kuu Uingereza.
The Reds wameshiriki mechi 37 bila kupoteza na wakajizolea mechi bila kushindwa alama 101 wakati huo ambapo walipoteza kwa magoli 2-1 msimu uliopita kwa mabingwa wa Chapions Manchester City tarehe 3 mwezi Januari mwaka 2019.
Upande wa meneja Jurgen Klopp ndio timu inayoshiriki ligi ya Premia kuweza kukamilisha mwaka mmoja bila kushindwa.
Arsenal ambao walishiriki michezo 49 katika msimu wa mwka 2003-04 na Chelsea kutoka mwezi wa oktoba 2004 hadi Novemba 2005 ni miongoni mwa timu ambazo zimeweza kucheza mechi bila kushindwa kwa mwaka mmoja.
Jordan HendersonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJordan Henderson amkubatia mkufunzi wao Jurgen Klopp baada ya mechi yao dhidi ya Sheffield United
Liverpool ambayo ilishindwa nyumbani ni dhidi ya Wolves katika kombe la FA mwezi Januari mwaka jana.
Pamoja na timu yao ya vijana chipukizi kupoteza kwa Aston Villa katika kombe la Carabao mwezi uliopita.
Liverpool imepoteza mara mbili katika ligi ya Champions dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya mkondo wa kwanza kabla ya mkondo wao wa pili dhidi ya Napoli mwaka huu katika hatua ya makundi.
Licha ya kutofungwa , Liverpool haikushinda kombe lolote la nyumbani mwaka 2019.
Mafanikio yao yalikuwa katika mechi za kimataifa, kuwa klabu ya kwanza ya Uigereza kupata ushindi wa kombe la Champions, Uefa Super Cup waliolipata Agosti baada ya kuichapa Chelsea kwa mikwaju ya penati na katika michuano ya kombe la Fifa.

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 03.01.2020: Pogba, Grealish, Maddison, Can, Longstaff, Batshuayi, Giroud

LIOS MEDIA
England
03/01/2020

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 03.01.2020: Pogba, Grealish, Maddison, Can, Longstaff, Batshuayi, Giroud


Paul Pogba
Manchester United inapania kuwanunua viungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na James Maddison, 23, kutoka Leicester. (Independent)
Wachezaji wengine wanolengwa na United ni kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Emre Can, 25, na Sean Longstaff, 22, wa Newcastle. (ESPN)
James MaddisonHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJames Maddison wa Leicester ni miongoni mwa wachezaji wa safu ya kati wanaonyatiwa na United.
Aston Villa ina mpango wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, kwa lengo la kumpatia mkataba wa kudmu. (Footmercato - in French)
Villa pia wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33. (Sun)
Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ameelezea kujitolea kwake kwa Arsenal na kutuliza tetesi za kuondoka kwake mwezi Januari. (Evening Standard)
Gabon Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang azima tetesi kuwa huenda akaondoka Arsenal mwezi huu
Arsenal imeingia katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24. (Telegraph)
Inter Milan ni moja ya klabu zilizowasiliana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen. Kandarasi ya kiungo huyo wa miaka 27 inakamilika msimu huu wa joto. (Sky Sports)
Manchester City inatarajiwa kurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 34. (Sun)
FernandinhoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionManchester City kurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho.
Dau la Chelsea la yuro milioni 40 la kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele ,23, limekataliwa na Lyon. (Footmercato - Kwa Kifaransa)
Aston Villa inatafakari uwezekano wa kuweka dau la kumnunua kipa wa Stoke City Muingereza, Jack Butland, 26. (Mail)
Ajax imesitisha mpango wa kumnunua beki ya Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen kwa sababu bei ya mchezaji huyo wa miaka 32 ni ghali sana . (De Telegraaf - Ujerumani)
Jan VertonghenHaki miliki ya pichaINPHO
Image captionAjax imesitisha mpango wa kumnunua beki ya Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen (kulia)
Southampton wanataka kumsaini beki wa Valladolid raia wa Ghana Mohammed Salisu, 20. (Sky Sports)
Leicester imeipiku Arsenal katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa Juventus na Italia, Daniele Rugani, 25. (Express)
Arsenal imemuulizia winga wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24. (Marca - ya Uhispania)
Thomas LemarHaki miliki ya pichaEPA
Image captionThomas Lemar alipojiunga na Atletico Madrid mwaka 2018

Tetesi Bora Alhamisi

Real Madrid imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27. (Le10Sport)
Manchester United na Tottenham wanatarajiwa kukabiliwa kwa ushindani mkali wa kumnunua kiungo wa kati wa Lille Mfaransa Boubakary Soumare,20, huku ofa sita za kumnunua zikiripotiwa kupokelewa na klabu yake. (Mail)

Thursday, 19 December 2019

Vurugu wakati El Clasico ikiendelea

Mtanange wa El Clssico baina ya Real Madrid na Barcelona umemalizika kwa kuacha historia ya aina yake

Barcelona v Real Madrid 3.JPG

Barcelona v Real Madrid 2.JPG
Mchezo wa El Classico uliokuwa ukisuburiwa kwa hamu dunia nzima umechezwa na kuacha historia ya aina yake.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Camp Nou, ulivuta nyomi la mashabiki elfu 93 na 426 ikiwa ni idadi ya tiketi zilizouzwa. Mchezo huo baina ya Real madrid na Barcelona ulimalizika kwa sare ya 0-0 .
Ni mara ya kwanza ndani ya miaka 17 ikiwa ni katika mtanange wa  50 , El Clasico imemalizika kwa sare ya bila kufungana.
Kitachokumbukwa zaidi katika mtanange huo wa El Clasico sio matokeo ya mchezo bali ni vurugu zillizosababishwa na waandamanaji haramu wanaotaka Catalan “Barcelona” ijitenge kutoka Uhispania. Kipindi Fulani mchezo ilibidi kusimamishwa kwa dk kadhaa.



HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...