Showing posts with label Sports {kitaifa}. Show all posts
Showing posts with label Sports {kitaifa}. Show all posts

Friday, 3 January 2020

Liverpool 2-0 Sheffield United: Reds wacheza ligi ya Premia bila kufungwa mwaka mzima

LIOS MEDIA
England
03/01/2020
Liverpool,imeshikilia uongozi wa ligi kuu ya England kwa mwaka mzima bila kufungwa baada ya Sheffield United kugaragazwa uwanjani Anfield.

Mohamed Salah and Sadio Mane

The Reds walipata ushindi wa mapema kupita Mohamed Salah katika dakika ya nne kutoka kwa pasi fupi kutoka kwa Andy Robertson.
Lakini hakuna bahati yoyote katika ushindi wao pale Sadio Mane alipofunga bao la pili baada ya Salah kukosa nafasi hiyo.
Majogoo wa Jiji Liverpool, waliweza kuweka mwanya huo wa alama 13 baada ya wapizani wake wa karibu Leicester na Manchester City kujipatia ushindi katika mechi za mwaka mpya.
Mohamed SalahHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMohamed Salah alifunga dhidi ya timu 22 kati wapinzani 25 wa ligi ya Premia aliopambana nao kama mchezaji wa Liverpool, na kushindwa kufunga bao dhidi ya Manchester United, Swansea na Aston Villa
Upande huo unaogozwa na Jurgen Klopp ulishuka kwa alama mbili wakiwa na alama 58 badala ya alama 60 msimu huu.
Kwa upande wa Chris Wilder ulikuwa wa kushindwa wa pili mfululizo kushindwa, lakini wamesalia wakakamavu na kuwa nambari sita katika jeduli ya ligi ya Premia na alama 29.
Ushindi wa Liverpool dhidi ya Sheffield United umeweka historia ya kuwa miongoni mwa timu ambazo hazijafungwa kwa mwaka mmoja katika ligi kuu Uingereza.
The Reds wameshiriki mechi 37 bila kupoteza na wakajizolea mechi bila kushindwa alama 101 wakati huo ambapo walipoteza kwa magoli 2-1 msimu uliopita kwa mabingwa wa Chapions Manchester City tarehe 3 mwezi Januari mwaka 2019.
Upande wa meneja Jurgen Klopp ndio timu inayoshiriki ligi ya Premia kuweza kukamilisha mwaka mmoja bila kushindwa.
Arsenal ambao walishiriki michezo 49 katika msimu wa mwka 2003-04 na Chelsea kutoka mwezi wa oktoba 2004 hadi Novemba 2005 ni miongoni mwa timu ambazo zimeweza kucheza mechi bila kushindwa kwa mwaka mmoja.
Jordan HendersonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJordan Henderson amkubatia mkufunzi wao Jurgen Klopp baada ya mechi yao dhidi ya Sheffield United
Liverpool ambayo ilishindwa nyumbani ni dhidi ya Wolves katika kombe la FA mwezi Januari mwaka jana.
Pamoja na timu yao ya vijana chipukizi kupoteza kwa Aston Villa katika kombe la Carabao mwezi uliopita.
Liverpool imepoteza mara mbili katika ligi ya Champions dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya mkondo wa kwanza kabla ya mkondo wao wa pili dhidi ya Napoli mwaka huu katika hatua ya makundi.
Licha ya kutofungwa , Liverpool haikushinda kombe lolote la nyumbani mwaka 2019.
Mafanikio yao yalikuwa katika mechi za kimataifa, kuwa klabu ya kwanza ya Uigereza kupata ushindi wa kombe la Champions, Uefa Super Cup waliolipata Agosti baada ya kuichapa Chelsea kwa mikwaju ya penati na katika michuano ya kombe la Fifa.

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 03.01.2020: Pogba, Grealish, Maddison, Can, Longstaff, Batshuayi, Giroud

LIOS MEDIA
England
03/01/2020

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 03.01.2020: Pogba, Grealish, Maddison, Can, Longstaff, Batshuayi, Giroud


Paul Pogba
Manchester United inapania kuwanunua viungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na James Maddison, 23, kutoka Leicester. (Independent)
Wachezaji wengine wanolengwa na United ni kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Emre Can, 25, na Sean Longstaff, 22, wa Newcastle. (ESPN)
James MaddisonHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJames Maddison wa Leicester ni miongoni mwa wachezaji wa safu ya kati wanaonyatiwa na United.
Aston Villa ina mpango wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 26, kwa lengo la kumpatia mkataba wa kudmu. (Footmercato - in French)
Villa pia wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33. (Sun)
Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ameelezea kujitolea kwake kwa Arsenal na kutuliza tetesi za kuondoka kwake mwezi Januari. (Evening Standard)
Gabon Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang azima tetesi kuwa huenda akaondoka Arsenal mwezi huu
Arsenal imeingia katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24. (Telegraph)
Inter Milan ni moja ya klabu zilizowasiliana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen. Kandarasi ya kiungo huyo wa miaka 27 inakamilika msimu huu wa joto. (Sky Sports)
Manchester City inatarajiwa kurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 34. (Sun)
FernandinhoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionManchester City kurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho.
Dau la Chelsea la yuro milioni 40 la kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele ,23, limekataliwa na Lyon. (Footmercato - Kwa Kifaransa)
Aston Villa inatafakari uwezekano wa kuweka dau la kumnunua kipa wa Stoke City Muingereza, Jack Butland, 26. (Mail)
Ajax imesitisha mpango wa kumnunua beki ya Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen kwa sababu bei ya mchezaji huyo wa miaka 32 ni ghali sana . (De Telegraaf - Ujerumani)
Jan VertonghenHaki miliki ya pichaINPHO
Image captionAjax imesitisha mpango wa kumnunua beki ya Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen (kulia)
Southampton wanataka kumsaini beki wa Valladolid raia wa Ghana Mohammed Salisu, 20. (Sky Sports)
Leicester imeipiku Arsenal katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa Juventus na Italia, Daniele Rugani, 25. (Express)
Arsenal imemuulizia winga wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24. (Marca - ya Uhispania)
Thomas LemarHaki miliki ya pichaEPA
Image captionThomas Lemar alipojiunga na Atletico Madrid mwaka 2018

Tetesi Bora Alhamisi

Real Madrid imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27. (Le10Sport)
Manchester United na Tottenham wanatarajiwa kukabiliwa kwa ushindani mkali wa kumnunua kiungo wa kati wa Lille Mfaransa Boubakary Soumare,20, huku ofa sita za kumnunua zikiripotiwa kupokelewa na klabu yake. (Mail)

Thursday, 19 December 2019

Matamshi ya Mesut Ozil: Kiungo wa Arsenal afutwa kwenye mchezo wa video China

Mesut Ozil prays before Arsenal's game against Manchester CityHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMesut Ozil, ni Muislamu wa asili ya Kituruki
Kiungo wa Arsenal Mesut Ozil ameondoshwa kwenye mchezo wa video wa Pro Evolution Soccer (PES) 2020 toleo la Uchina baada ya kuikosoa nchi hiyo kwa kuwatesa jamii ya Waislamu ya Uighur.
Ozil, 31, ambaye ni Muislamu, amewaita Wauighur (Wachina wa asili ya Kiislamu) "mashujaa wanaokabiliana na mateso".
Pia ameukosoa utawala wa Uchina na ukimya wa Waislamu katika kuwatetea wenzao nchini humo.
Kampuni ya NetEase, ambayo inatoa video za PES nchini China, imesema kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani ameondolewa kwenye matoleo matatu yaliyopo nchini humo.
"Ozil ametoa matamshi makali kuhusu Uchina kwenye mitandao ya kijamii," imesema kampuni hiyo kwenye taarifa yake.
"Matamshi yake yameumiza hisia za mashabiki wa Kichina na kuvunja kanuni ya michezo ya amani na upendo. Hatuelewi, kukubali ama kusamehe jambo hili.
Arsenal imesema kuwa klabu hiyo "si ya kisiasa" na wizara ya mambo ya nje ya Uchina imedai kuwa mchezaji huyo mwenye asili ya Kituruki amedanganyika na habari za uongo za mtandaoni.
Makundi ya haki za binaamu yanadai kuwa takribani watu milioni moja - wengi wao kutoka jamii ya Waislamu ya Uighur - wanashikiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka katika magereza yenye ulinzi mkali.
Uchina imekuwa ikikanusha kuwa inawanyanyasa Waislamu wa Uighur na kudai kuwa watu hao wanapatiwa mafunzo katika "vituo vya ufundi stadi" ili kukabiliana na ugaidi.
Kaibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Uingereza, amesema Ozil ni wa "kupongezwa san" na kudai kuwa kitendo cha Arsenal kujitenga naye ni cha "kusikitisha".

Tuesday, 17 December 2019

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 17.12.2019: Arteta, Ancelotti, Young, Dembele, Ibrahimovic

Mikel ArtetaManchester City wamekerwa na mchakato wa Arsenal kumfuatilia kocha wao msaidizi Mikel Arteta na wameionya Arsenal kuwa itawapasa watoe donge nono ili wamnyakue kocha huyo. (Mirror)
Arteta anatarajiwa kukutana na kiongozi mkuu wa Arsenal Josh Kroenke Jumatatu usiku kwa ajili ya kufanya usaili wa tatu na wa mwisho huku akikaribia kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Unai Emery aliyetimuliwa mwezi uliopita. (Mail)
Kocha wa zamani wa Chelsea, AC Milan, Real Madrid na Napoli Carlo Ancelotti amefikia makubaliano ya jumla kuwa kocha wa klabu ya Everton. (Sky Sports)
Carlo Ancelotti
Chelsea wamewajumuisha washambuliaji Mjerumani Timo Werner wa klabu ya RB Leipzig, 23, na Mfaransa wa klabu ya Lyon Moussa Dembele, 23, katika orodha ya wachezaji wanaotaka kuwasajili mwezi Januari. (Mail)
Mmiliki wa Napoli Aurelio De Laurentiis ametupilia mbali mipango ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, akisema kuwa klabu yake inabidi ianze kujinga upya kutokea chini. (Goal.com)
Klabu ya Leicester inatajwa kuwa na utashi wa kiwango cha juu kumsajili beki wa klabu ya Juventus na Uturuki mwenye thamani ya pauni milioni 25 Merih Demiral,21, kwenye dirisha dogo la usajili mwezi ujao. (Leicester Mercury)
Ashley Young
Mlinzi raia wa England Ashley Young, 34, anatarajia kuihama klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu na yupo tayari kuanza mazungumzo na vilabu mbalimbali kuanzia mwezi ujao. (ESPN)
Wachezaji waandamizi wa Tottenham wamemshauri kocha wao Jose Mourinho kumsajili mshambuliaji wa Wolves Adama Traore, 23, baada ya mchezaji huyo raia wa Uhispania kuonesha kiwango kizuri dhidi yao Jumapili iliyopita (Football Insider)
Winga wa Ujerumani Leroy Sane, 23, ameeleza kuwa hatimaye amereje kwenye uwanja wa mpira wakatiakikaribia kurejea kwenye kikosi cha Manchester City. Sane hajacheza toka mwezi Agosti alipopata majeraha makubwa. (Manchester Evening News)
Unai Emery
Kocha Unai Emery amekataa ofa ya kuifundisha Everton akiamini bado ni mapema kufundisha klabu nyengine ya Ligi ya Primia baada ya kufurushwa na Arsenal mwezi uliopita. (Marca)
Vilabu vya Leicester City, Newcastle, Southampton na Leeds United vinagombea saini ya mshambuliaji raia wa England Jarrod Bowen, 22, anayechezea klabu ya Hull City. (Mirror, via Leicester Mercury)
Liverpool wameonesha nia ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa klabu ya Coventry City raia wa England Sam McCallum, 19. (90min.com)
Posted by
Lios media


Friday, 8 January 2016

MBWANA SAMATTA Kama Diamond Vile Atutoa Kimasomaso Watanzania...Achukua Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika...

Hatimaye matarajio na matumaini ya mamilioni ya watanzania yametimia, Mbwana Ally Samatta ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya bara la Afrika.

Usiku wa January 7, 2016 umekuwa mtamu sana kwa Samatta na watanzania kwa ujumla kutokana na kijana huyo wa Mbagala kuiletea Tanzania heshima kubwa kwenye sekta ya michezo hususan soka.

ramaaa

Samatta alikuwa akipambana na wachezaji wengine wawili ambao ni Robert Kidiaba Muteba (DR Congo & TP Mazembe) na Baghdad Bounedjah (Algeria & Etoile du Sahel).

Msemo wa wahenga kwamba ‘nyota njema huonekana asubuhi usemi huo’ ulianza kujitokeza mapema pale ambapo jina la nyota huyo wa Afrika lilipojitokeza kwenye list ya majina ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha wachezaji wa Afrika.

Pierre-Emerick Aubameyang amenyakua tuzo ya mchezaji bora Afika 2015 na kumpiga chini Yaya Toure ambaye ni mshindi mara nne mfululizo wa tuzo tuzo hiyo na alikua anaitetea tena kwa mara nyingine lakini ameshindwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara tano.

Ukiachana na tuzo ambayo ilikuwa inasubiliwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka duniani kote ambayo ni tuzo ya mchezaji bora wa Afrika yenye vipengele viwili kipengele cha kwanza ni mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla na kipengele cha pili ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Afrika) kuna tuzo mbalimbali zilitolewa kwa washindi.

Haya ni majina ya washindi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa usiku wa January 7, 2016

Timu bora ya taifa ya mwaka kwa upande wa wanaume: Ivory Coast
Timu bora ya taifa ya mwaka kwa upande wa wanawake: Cameroon
Kocha bora : Herve Renard (aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coast)
Mchezaji bora kijana: Victor Osimhen (Nigeria)
Mchezaji bora chipukizi:Etebo Oghenakoro (Nigeria)
Fair play award (mchezaji muungwana): Allez Casa (Senegal)
Klabu bora ya mwaka: TP Mazembe
Mchezaji bora wa kike: Gaelle Enganamouit (Cameroon)
Mwamuzi bora wa mwaka: Papa Bakary Gassama (Gambia)
Wachezaji wakongwe: Charles Kumi Gyami (Ghana) na Samuel Mbappe Leppe (Cameroon).

Saturday, 2 January 2016

TASWIRA TATU, IBRA AJIB AKISHANGILIA BAO LAKE LILILOIUA NDANDA KWA KUPIGA SIMU YA KIATU

Ilikuwa raha ya aina yake wakati Ibrahim Ajib alipofunga bao lake pekee lililoiwezesha Simba kuituliza Ndanda kwa 1-0 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, leo.


Lakini utamu zaidi ulikuwa namna ambavyo Ajib alishangilia kwa kutumia kiatu, kama vile alikuwa anazungumza na simu. Basi ni mambo mapya kila mara na ndiyo raha yenye ya soka.

EXLUSIVE INTERVIEW: UNATAKA KUJUA KWANINI SAMATTA ANAKWEDA KUCHEZA UBELGIJI, AMESAINI MKATA WA MUDA GANI? MENEJA WAKE AMEFUNGUKA KILA KITU, MADINI YOTE YAPO HAPA

Safari ya  nyota wa Tanzania na TP Mazembe Mbwana Samatta kwenda kukipiga katika bara la Ulaya sasa imefika patamu baada ya manager wa mchezaji huyo Jamal Kisongo kuthibisha kwamba kila kitu kimeshakamilika na kinachosubiliwa ni mchezaji huyo kujiunga na kbabu ya Genk ya nchini Ubelgiji inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo maarufu kama Belgian Pro League.

Taarifa za Samatta kujiunga na klabu ya Genk zinasambaa kwa kasi sana na hicho ndiyo kitu ambacho kimefanya mtandao huu umtafute manager wa mchezaji huyo ili aweke wazi baadhi ya mambo ambayo wadau wa soka la Tanzania wamekuwa wakijiuliza kwa muda mrefu juu ya Samatta kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Hapa unaweza kupata majibu ya maswali yote kutoka kwa manager wa Samatta Bw. Jamal Kisongo baada ya kufafanua vitu kwa kina ikiwa ni pamoja na kwanini Samatta anakwenda Ubelgiji na si nchi nyingine za Ulaya sambamba na klabu ambayo atakwenda kuitumikia lakini pia ameweka wazi Samatta amesaini mkataba wa muda gani na Genk.

Ni kweli kwanza kipindi chake cha kikanuni kwa mujibu wa FIFA kwa yeye kuwa na haki ya kusaini kuchagua wapi anataka kwenda na kufanya maamuzi kimefika, kwasababu Mbwana mkataba wake unamalizika April 30, 2016 kwa maana hiyo kwa mujibu wa kanuni ya FIFA, mkataba ukibaki miezi sita na chini ya hapo una haki ya kusaini pre contract na hicho ni kitu cha msingi kabisa.

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...