Safari ya nyota wa Tanzania na TP Mazembe Mbwana Samatta kwenda
kukipiga katika bara la Ulaya sasa imefika patamu baada ya manager wa
mchezaji huyo Jamal Kisongo kuthibisha kwamba kila kitu kimeshakamilika
na kinachosubiliwa ni mchezaji huyo kujiunga na kbabu ya Genk ya nchini
Ubelgiji inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo maarufu kama Belgian Pro
League.
Taarifa za Samatta kujiunga na klabu ya Genk zinasambaa kwa kasi sana
na hicho ndiyo kitu ambacho kimefanya mtandao huu umtafute manager wa
mchezaji huyo ili aweke wazi baadhi ya mambo ambayo wadau wa soka la
Tanzania wamekuwa wakijiuliza kwa muda mrefu juu ya Samatta kwenda
kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Hapa unaweza kupata majibu ya maswali yote kutoka kwa manager wa
Samatta Bw. Jamal Kisongo baada ya kufafanua vitu kwa kina ikiwa ni
pamoja na kwanini Samatta anakwenda Ubelgiji na si nchi nyingine za
Ulaya sambamba na klabu ambayo atakwenda kuitumikia lakini pia ameweka
wazi Samatta amesaini mkataba wa muda gani na Genk.
Ni kweli kwanza kipindi chake cha kikanuni kwa mujibu wa
FIFA kwa yeye kuwa na haki ya kusaini kuchagua wapi anataka kwenda na
kufanya maamuzi kimefika, kwasababu Mbwana mkataba wake unamalizika
April 30, 2016 kwa maana hiyo kwa mujibu wa kanuni ya FIFA, mkataba
ukibaki miezi sita na chini ya hapo una haki ya kusaini pre contract na
hicho ni kitu cha msingi kabisa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI
Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...
-
Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Uingereza Johanna Konta amemshinda Venus Williams 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili ya shindano la tenisi ...
-
Wakali wa ‘comedy’ kwenye tasnia ya Bongo Movies, Mzee Majuto, Asha Boko na Mzee Majanga wamefanya kweli kwenye filamu yao mpya inayokwend...
No comments:
Post a Comment
yes by message