Katika baadhi ya mikoa kusini na Pwani ya Tanzania, suala la binti kupatiwa mafunzo maalumu ya kimila ni desturi ambayo si ngeni, wao wanaita kumtoa mwari.
Utamaduni huo ujumuisha wasichana kuwekwa ndani kwa muda wa miezi kadhaa kwa ajili ya ya kufundwa na wataalamu wa masuala hayo.
Jambo hili kwa binti ambaye hajalipitia huenda likawa na gharama kubwa katika maisha yake ya ndoa ya baadaye kwani huonekana kama vile hajui mambo mengi na zaidi yale ya kumridhisha mume wake kwa mjibu wa mila zao.
Miongoni mwa jamii inayotajwa kuendeleza mila hizi hata katika kipindi hiki cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia ni Wamakonde kutoka mikoa ya Kusini mwa Tanzania na baadhi ya wakazi wa wilaya za mkoa wa Pwani nje kidogo ya jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Aidha utamaduni huu umekuwa ukilaumiwa na baadhi ya watu kuwa ndio chanzo cha kusitisha wasichana wengi masomo wakiwa na umri mdogo,
Mara nyingi sherehe hizi pia huwa zinafanyika mara tu wasichana wanapomaliza darasa la saba(elimu ya shule ya msingi) au wengine hata kabla hawajamaliza elimu hiyo.
Wazaramo ni kabila maarufu nchini Tanzania ambalo linasifika zaidi kwa ngoma.
Kuna msemo wa utani nchini humo unaowahusisha wanawake wa kabila hilo kupenda kucheza ngoma.
Lakini je, sifa hiyo wameipata kutokana na mafunzo waliyopitia?
Utaratibu wa shughuli hii ukoje na una maana gani katika jamii yao.
Mwandishi wa BBC Fatma Abdala aliweza kutembelea eneo la kisarawe mkoa wa Pwani na kutaka kufahamu zaidi juu ya utamaduni huu.
''Kwa sisi Wazaramo suala hili ni muhimu sana,na kabila letu ni moja ya makabila yanayopenda kuhakikisha kwamba wasichana wanashiriki shughuli zote na kisha kutolewa Mwali baada ya kukamilisha taratibu zote,na kwa wazaramo maandalizi ya sherehe hizo ni makubwa'' Bi Amina .
Ameongeza kuwa kuna mambo muhimu ambayo wasichana hawa hufundishwa na kungwi suala zima la mahusiano ya kawaida na watu wengine,mapenzi na ndoa kwa ujumla. mwanume kabla ya ndoa .
Mtaalamu mwingine wa shughuli hizo anabainisha kuwa mpaka mtoto anapotolewa na kuchezewa ngoma kama mali huenda akawa amekaa ndani kwa miezi kadhaa au mpaka mwaka mzima.
"Sherehe hii ni kubwa kwetu, huwa tunachanga fedha kwa ajili ya kuja katika sherehe hizo za kumcheza mwari na hata tunavaa sare", Bi.Halima anaeleza.
Licha ya kuwacheza wanawake, kabila hili nalo linawacheza wanaume yaani wanapeleka jando...ili waweze kupata mafunzo wakati wa kubalehe.
Kwa mujibu wa bi. Saada ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo ansema wanacheza mwali binti kuanzia umri wa miaka kumi, binti huyu huelekezwa unyumba namna ya kukaa na mume wake, nguo za kuvaa akiwa na mumewe, chakula cha kupika na kadhalika.
Pamoja na kuwa tamaduni hii imekuwa ikiendelee kwa miaka mingine, athari zake zimetajwa kuwa kubwa katika upande wa kuongeza idadi ya mimba za utotoni na hata kushusha maendeleo katika jamii hizo.
Hii ni kutokana na sherehe hizo pia kumuacha wazi mwali hadharani katika mavazi na hataka kuwa ishara ya kutangaza kuwa amekuwa na yuko tayari kwa wanaume.
Kwa upande wake Bi. Saum anasema kuwa hali hiyo inatokea kwa sababu wasichana wengi wanafanya tofauti na wanavyoelekezwa na hivyo kupelekea mabinti wadogo kubeba ujauzito na kubatili maana iliyolengwa.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa utamaduni ni heshima kwa mwanamke.
"Kuchezwa kuna raha yake lakini mwali wa kizaramo asipochezwa huchukuliwa kama hajakua mkubwa na hupelekea muda mwingine kukosa mume na hata kubaguliwa na wasichana wenzake waliopitia unyago," bi Halima anasisitiza.
Miongoni mwa kazi za ya msanii ni kuielimisha, kuiburudisha, kuiliwaza na kuikosoa jamii na asipotekeleza hayo basi kazi yake haijakamilika.
Lakini je wasanii wa muziki wa Afrika Mashariki wameweza kuielimisha na kuikosoa jamii?.
Katika kile ambacho kilionekana kama njia ya kuikosoa na kuielimisha jamii King Kaka kwa jina lake halisi Kennedy Ombima, mwishoni mwa juma alitoa video tata ya wimbo aliouta 'Wajinga Nyinyi', akikosoa maovu miongoni mwa jamii ya Wakenya.
Katika wimbo huo amewatuhumu wazi wazi watu binafsi aliowataja majina moja kwa moja pamoja na wabunge na taasisi za umma kwa ufisadi, uliokithiri na maovu mengine katika jamii , huku akiwataka Wakenya kutafakari maovu hayo na kuyarekebisha.
Aliutumia wimbo huo huwatolea wito Wakenya kutafakari ujumbe wa video yake na kuchukua hatua.
Tangu video ya wimbo huo kutoka, imekuwa ndio maarufu zaidi mitandaoni nchini Kenya .
Licha ya wimbo 'Wajinga nyinyi' ulioimbwa kwa mtindo wa rap kusifiwa na wengi kuwa maudhui yake yalikua ni ya kweli baadhi ya waliotajwa majina walimkosoa na kutishia kumshitaki.
King kaka alidai anatishiwa maisha na kujisalimisha katika Ofisi ya Mwendeshamashitaka mkuu wa Serikali (DCI), akidai lakini ofisi hiyo ilisema haikumuita.
Mwanamuziki huyo ambaye alipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wasanii wenzake kwa kutoa ujumbe huo, pia aliahidiwa utetezi wa kisheria na mawakili maarufu iwapo atapelekwa mahakamani kwa kuimba wimbo 'Wajinga nyinyi' .
Mbali na mwanamuziki King Kaka wanamuziki wengine wa Kenya pia awali walitoa nyimbo zilizokosoa ufisadi katika jamii yao. Mfanyo ni mwanamuziki Erick wa mtindo wa Afrobit Wainanaina katika wimbo wake 'Nchi ya kitu kidogo' na mwanamuziki wa mtindo wa Hiphop Juliani katika wimbo wake 'Sitasimama maovu yakitawala'
Hali ikoje nchini Tanzania?
Kwa muda sasa wasanii wa muziki nchini Tanzania wamekuwa wakiwasilisha ujumbe wao hususan baada ya kuingia madarakani kwa rais John Pombe Magufuli. Ukosoaji wao umekua ni ukijibu yanayofanyika nchini mwao.
Wa kwanza alikua ni wanamuziki ni mwanamuziki wa Hip hop Karama Masopud na wimbo wake 'Magufuli balaa ' , al maarufu Kalapina.
Hata hivyo kalapina ambaye alishindwa katika harakatii zake za kuwania ubunge, alitoa wimbo mwingine wa kumsifu rais Magufuli. Aliimba: 'Unaweza kudhani ni ni miujiza lakini ni picha halisi. Upinani uko kimya, hauna la kusema. Amefanya walichopanga kukifanya.''
Msanii mwingine aliyekuwa na ujumbe wa ukosoaji miongo ni mwa jamii, ni mwanamuziki wa mtindo wa rap, Nikki Mbishi ambapo Januari 2017 aliimba:''I'm Sorry JK.''
Mtangulizi wa rais John Pombe Magufuli , Jakaya Kikwete, alifahamika kama 'JK'.
''Itaeleweka ikiwa nitasema siku moja kwamba, hakuna rais kama JK. Watanzania wanakukosa sanana kwa niaba ya Watanzania ninasema wanakukosa sana na wanatamani ungegombea awamu ya tatu kama rais''
Katika wimbo huo, msanii aliongelea kuhusu namna baadhi ya Watanzania akiwemo yeye walimkosoa vibaya Kikwete alipokua mamlakani lakini sasa wanamkosa na kutamani angegombea awamu ya tatu mamlakani!.
Alisema kwa sasa hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Mikopo ya wanafunzi wa Chuo Kikuu haipatikani tena kwa urahisi, uchumi unadhoofika na benki zinakabiliwa na wakati mgumu, hakuna pesa mitaani na demokrasia imebanwa, miongoni mwa mambo mengine.
Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) lilimuita msanii huyo wa muziki wa rap na kumhoji. Baadae aliandika taarifa katika kituo cha polisi jijini Dar es salaam, na wimbo wake ukapigwa marufuku mnamo mwezi wa Februari 2017.
Kufuatia kuvamiwa kwa kituo cha TV na mshirika wa karibu wa rais, John Magufuli Paul Makonda, wasanii wa Hip hop walipeleka hasira zao juu ya kile kilichokua kikiendelea.
Ney wa Mitego alitoa wimbo, 'Wapo'. Ingawa hakutaja moja kwa moja jina lolote la kiongozi katika wimbo wake ilikua wazi kuwa alikua akielezea maeneo ambayo rais Joh Pombe Magufuli ''ameshindwa'' kutekeleza wajibu wake.
Wimbo huo ulipata umaarufu sana. Alikamatwa mara moja na Basata ikapiga marufuku kabisa wimbo huo.
Hata hivyo Jumatatu iliyofuatia, rais Magufuli aliagiza Ney aachiliwe huru na wimbo wake uchezwe.
Nyimbo nyingine zilizokosoa utawala wa rais Magufuli ni pamoja na 'Dereva wa 5 hana leseni' wa Wagosi wa Kaya, 'Usinipangie' wa Baghdad na 'Madaraka ya kulevya' wa Weusi.
Usinipangie uliimbwa kujibu kauli ya rais Magufuli kusema kuwa hatoambiwa la kufanya.
Madaraka ya kulevya ni wimbo ambao mistari yake iliandikwa kwa ustadi lakini yenye utata. Wimbio huo haukuwazungumzia moja kwa moja rais Magufuli au Makonda , lakini maneno yaliyotumiwa yanaonyesha kumuhusu kiongozi aliyelewa mamlaka kukiuka maadili yake ya kiuongozi.
Msanii wa muziki wa rap Profesa Jay katika wimbo wake 'Ndio, mzee aalikosoa utawala wa rais Mkapa miaka ya 2000, Nakaaya Sumari katika wimbo wake Mr politician na Mrisho Mpoto katika wimbo Mjomba ambao wengi wanaamini vilimlenga rais Jakaya Kikwete.
Uganda
Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya wasanii nchini Uganda walijitokeza kukosoa maovu wanayodai yanatekelezwa na utawala wa rais wa muda mrefu yoweri Museveni, huku wengine wakimsifu.
Mwaka 2012 katika wimbo wake Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine katika wimbo wake 'By Far' aliashiria nia yake ya kujiunga na siasa akiukosoa utawala wa rais Museveni.
Aliimba : 'My father said there is more politics music industry than in the Parliement, they dont know who they are dealing with' akimaanisha 'Baba yangu aliniambia kuna siasa zaidi katika muziki kuliko bungeni, lakini hawajui ninani wanaekabiliana nae'.
Katika wimbo huu alielezea kuwa wakazi wa vitongoji duni kikiwemo kitongoji cha ambako alikua akiishi hawaogopi vitisho, huku akiwatolea wito raia kuamka na kupigania haki zao.
Akiimba kwa kwa lugha ya Luganda Bibi Wine, mwaka 2016, alitoa wimbo 'Dembe' au 'Amani' Msanii Bobi Wine aliouimba Bobi Wine alikemea kile alichokiita ghasia miongoni mwa viongozi wa Uganda, huku akiwalaumu kwa kuchochea ghasia hususan wakati wa uchaguzi.
Aliitaka jamii ya Waganda kupiga kura kwa amani ili kuepuka ghasia zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita, akiwatuhumu viongozi waliopo madarakani kuchochea ghasia hizo.
Imekua vigumu kutumia muziki kuelimisha na kukosoa maovu Uganda:
Nyimbo zake zilizojaa ukosoaji wa rushwa na ukosefu wa haki za kijamii nchini Uganda zilichangia kwa kiasi kikubwa kuchaguliwa kwa Bobi Wine kama mbunge wa kyadondo Mashariki mwaka 2017.
Mnamo mwaka 2017 , msanii huyo aliimba: 'Ugandans need equal opportunity', Waganda wanahitaji fursa sawa'', akitaka serikali ifikishe huduma kwa usawa miongoni mwa raia mkiwemo ajira kwa vijana.
Hata hivyo juhudi zake za kuendelea kuukosoa utawala wa rais Museveni kupitia usanii wake wa muziki zimegonga mwamba baada ya maafisa wa usalama kuzuia matamasha yake yote ya muziki.
Msanii wa muziki wa Hip hop na Afro bit Uganda ni Jose Chameleone kutoka nchini Uganda ambaye alifahamika kwa kutumbuiza nyimbo zake katika hafla za Chama tawala cha NRM pamoja na matukio mengine ya serikali ya rais Museveni sasa amegeuka kuwa mkosoaji wake.
Baada ya Chameleone Kutangaza nia yake ya kuingia siasa na kugombea kiti cha Meya wa Jiji Kuu Kampala ili kumaliza maovu yanayofanyika katika mji huo, rais Museveni ambaye alikua mfuasi wake katika ukurasa wa twitter alimua kuondoa ufuasi wake.
Kinyume na Bobi Wine pamoja na Jose' Chamilion, Msanii mwingine maarufu kwa jina la Bebe Cool amekua mstari wa mbele kuunga mkono utawala wa rais Yoweri Museveni, huku akiwakosoa wasanii wenzake kwa kuukosoa utawala.
Ni dhahiri kuwa wasanii wengi wa muziki katika nchi za Afrika Mashariki wamekua wakitumia kazi yao kuzielimisha na kuzikosoa jamii zao, japo katika mazingira magumu inapokuja katika ukosoaji wa kisiasa. Hata hivyo swali ni je ukosoaji huu
Mbunge mmoja nchini Zimbabwe Joseph
Chinotimba ameingia katika kumbukumbu za Afrika baada ya kumbusu mke
wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kunakiliwa barani Afrika.
Mbunge huyo na mkewe walizoa tuzo hilo baada ya kupigana busu kwa dakika 10 na sekunde 17.
Rekodi hiyo iliwekwa katika hafla moja iliyopigiwa upatu na kunadiwa kuwa ''Mashindano ya busu refu zaidi kuwahi barani Afrika''
Hafla hiyo ilipangwa na kuandaliwa kwa ushirikiano na waandalizi wa Daftari la rekodi barani Afrika.
Hafla hiyo iliandaliwa katika mji mkuu wa Harare kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao iliyoadhimishwa jumapili.
MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Loveness Watson ‘Love’
amefunguka kwa kuwalaumu wasanii wa filamu Bongo movie kuwa ni wabinafsi
hawana msaada wowote katika matatizo zaidi ya wao kujiangalia na rafiki
zao wa karibu ameliona hilo alivyompoteza mama yake.
“Sina hamu na Bongo Movie misiba na matatizo ni ya kwao tu lakini
sisi hakuna ushirikiano wowote, mimi mwaka jana mwezi wa 12 nilifiwa na
mama yangu Mbeya nikatuma ujumbe hakuna hata wa kusema pole,”anasema
Love
Msanii huyo amedai kuwa amekuwa akishiriki kila msiba au ugonjwa na
kuchangishwa michango yeye pamoja na kaka yake Lekonia Watson ambaye pia
ni msanii lakini walipofiwa na mama yao kuna mtayarishaji mmoja tu ndio
aliyekwenda Mbeya kushiriki mazishi lakini si wasanii wa Bongo movie.
Shilolekwenye ubora wake, kama ukiangalia kwenye kipande cha hii video utaona mabadiliko mengine ambayo Shishi Baby kaamua kuja nayo.
Ni vipande viwili vya video vyenye sekunde kama hivi jumla, dalili nzuri kwamba mzigo mzima hauko mbali kuletwa… Hizi nimekutana nazo Instagram na mimi nimeona nikusogezee mtu wangu.
Zari wa Diamond Awachokonoa Tena Watanzania...Andika Maneno yafuatayo kwenye picha;
Baadhi ya Comments za Wabongo baada ya post hiyo ya Zari Hizi Hapa chini;
angiielly Uande hukoo kama hatujui English si arid kwao wanakoangea English stupid kabisaaa..... Nashangaa mijitu inamsupport huyu mkimbizi kwel kuna mijitu bado mikolon
angeljohn__ Hihihi tatizo Nyerere dah tungekuwa tunamwaga ung'eng'e na cc
doro_cute3 Awache kupotezea story za DNA, we want to see or else take tiffa to katunzi
ma_fusa_de_beauty @zarithebosslady wew n nyoko boss wng sio kwa kauli io panic at your own risk haha salute
kisuramie Chezea lugha ilokuja kwa majahazi@olivermakundi wifi kaamua now dayz c kwa kutushushua huku
catyfranco19 thanx to those kwonz english en not kiswakinge 4h By Lios Media
STAA aliyekuwa akitingisha kwa wasanii Bongo kutoka Kundi la Kaole, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa Mungu amemuona baada ya kukaa benchi kwa takriban miaka mitano bila kurekodi sinema.
Akizungumza na Ubuyu wa Town, Nora alisema alikuwa ameshakata tamaa lakini anaishukuru Kampuni ya Didas Entertainment ambayo imemthamini na kumrudisha tena kwenye gemu.
“Watu waliniona mimi sifai tena wala sina thamani tena lakini Dida aliniona mimi nina kipaji cha pekee, amenichukua na kufufua kipaji changu cha enzi na enzi, soon mashabiki wataniona,” alisema Nora.
Kupitia ukurasa wake mtandaoni,staa mrembo wa Bongo Movies ‘Lulu’ amefunguka haya;
Kuna Msemo Unasema “NDEGE WANAOFANANA HURUKA PAMOJA” hii misemo huwa inamaana sana Kwa akili yangu ndogo nilijaribu kuuweka huu Msemo katika Maisha ya kawaida Na nikagundua Una asilimia kubwa ya ukweli
Katika Maisha yetu ya mahusiano,urafiki,undugu,ujamaa Na hata ushabiki sio kwamba mambo yanatokeaga Kama miujiza tu,Mfano kwenye urafiki Huwezi kuwa Na Urafiki Na mtu ambaye hamuendani ki mawazo Na mtazamo,mnaweza kutofautiana Muonekano Na kila mtu nje akawa anashangaa lkn ndani yetu mna strong chemistry ambayo inawafanya muwe marafiki,kama Wewe Una character ya umbea Huwezi ukadumu Na rafiki ambaye ana character ya Ucha Mungu…itabidi upate rafiki mwenye character,maono Na mitazamo Kama yako ili kuweza kuruka pamoja Kwenye mahusiano ya Mapenzi iko hvyo pia…mtu anaweza kuwa Na mahusiano Na mtu Na watu nje wasimuelewe imekuwaje ameamua kuwa Na mtu wa aina hyo,pengine NI mtu ambaye hawaendani kbs Kwa Muonekano wa nje…point NI ile ile kuna chemistry ambayo iko ndani Yao yenye kuwafanya wawe Na mawazo sawa,maono sawa Na tabia zinazoendana Hata Kama sio asilimia kubwa…hyo NDO inayowafanya wawe pamoja bila kujali Umri,Muonekano au kitu chochote cha Muonekano wa nje..! Iko hvyo hata Kwa watu wanaokuzunguka,wanaokupenda Na kukuchukia…utapendwa Na watu mnaoendana tu wengine ambao hamna Aina yoyote Na uendano kwanza lazima wasikuelewe Na wasikupende pia kwasababu huna ambacho wanacho moyoni Kwa kichwanihaitokei tu from no where japo Kwa akili Za kawaida unaweza ukachukulia hvyo lkn Kiukweli Hivi NI vitu ambavyo vinaanza ndani yetu(Mioyoni) Na kuonekana nje NI matokeo ya mwisho kbsa..! Usione ajabu Wala kujisikia vibaya ukiona aina flani ya Marafiki inaondoka,Aina flani ya ndugu hupatani nao au Aina flani ya watu hawakupendi…Jua tu Hufanani Naowasikukwaze Tafuta unaofanana nao
Kufuatia gazeti moja la udaku kuandika stori ya uongo juu yake, Staa wa Bongo Movies, Halima Yahaya ‘Davina’ amemtolea uvivu muandishi wa stori hiyo kupitia ukurasa wake mtandaoni.
Hivi nyie waandishi wengne hv kwann hamnaga utu lini nimeongea na wewe lini? zuwenanyembo na ktk story umeandika nimekutaja mpk jina me nakujua ww Wkt mwingne mnasemaga hatudumu ktk ndoa wasanii lkn wkt mwingne nyie mnasababisha hivi kweli Mwanaume gn ataona mwanamke wake unatolewa story km hii akakuelew? Hyo mimba ulinipima? Mmezushaa wee ya Mike mpk kaamua kuwaonyesha mchumba wake lkn bdo mnamuandama haya huyo mchumba anaona huo ujinga hapo atajickiaje maskin haya Bosco ndo nani jmn ungeandika bac hata full name umetunga tu jina na kuandika I see…Hyo mimba mmenipima na ya nn mie au hujui hata km nina watoto wa kutosha nisiekaa nikasomesha na mimba tena ya wanaume wawili…muwe na Utu bac msitumie kalamu yenu vbaya..uwe na uhakika na unachoandika ww unapata PESA mimi UNANIHARIBIA ni DHAMBI jmn…… I hate u 4 this
Hali halisi kama inavyoonekana eneo la Kinondoni, mkwajuni, jijini Dar ambalo wananchi wake walikumbwa na bomoa bomoa baada ya mvua kubwa kunyeesha usiku wa kuamkia leo.
Staa wa bongo movies anayesifiwa kwa kuvaa uhusika kwenye kazi zake, Riyama Ally ameshare nasi picha hii kupitia ukurasa wke mtandaoni akiwa Kibaha na waigizaji wenzake ambapo riyama aliezega kuwa wapo kazina wafikanya kazi yake mpya.
“Riyamaally#Mkegani mke wa #kazibure damwan kazini wapendwa wangu #kibaha Kwa mfipa…..!!! #bi* damwan #kakamuhogomchungu @senatormsungu @barafusuleiman @mwanaher @cutyhassan @mbotohaji #babajemsi zairii14 n. K. Kaeni mkao wakula kazi ya mikono yangu damwan”-RIYAMA