Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), imesema inaendelea kuwahoji vigogo wanaodaiwa kuhusika katika kashfa ya ufisadi kwenye mauzo ya hati fungani za dola milioni 600 (sawa na Sh. trilioni 1.3), akiwemo Kamishna Mkuu wa zamani wa TRA, Harry Kitilya, ambazo serikali iliziuzia kwenye benki ya Standard ya Uingereza mwaka 2012.
Mbali na Kitilya ambaye ameingia kwenye kashfa hiyo kwa wadhifa wake wa mmiliki wa kampuni ya ushauri wa kifedha ya EGMA, wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Benki ya Stanbic tawi la Tanzania, Basher Awale ambaye aifukuzwa nchini na Uhamiaji mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kugundulika ni raia wa Kenya.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Uwekezaji wa benki hiyo, Shose Sinare, vigogo kadhaa wa serikali na maofisa wa benki ya Standard ya Uingereza.
Akizungumza na Nipashe jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola, alisema wanaendelea kukusanya ushahidi kuhusiana na sakata hilo ambalo ni nyeti kwasababu linahusisha nchi mbili za Tanzania na Uingereza.
Mlowola alisema tayari wameshawahoji watu kadhaa waliotuhumiwa katika sakata hilo na kinachoendelea ni ukasanyaji wa ushahidi ili hatua nyingine ziweze kuchukuliwa itakapobidi.
Alisema kwa sasa hawawezi kueleza zaidi kwa sababu uchunguzi bado unaendelea.
Kashfa hiyo ya ufisadi iliibuka mwaka 2012 baada ya Benki ya Standard kukubali kuikopesha serikali ya Tanzania kiasi cha trilioni 1.3 mwaka huo kwa masharti ya kulipwa riba ya asilimia 1.4 lakini benki ya Stanbic, tawi la Tanzania iliongeza asilimia moja na hivyo kufanya serikali kutakiwa kulipa riba ya asilimia 2.4.
Benki ya Stanbic ambayo ni tawi la Standard iliyokuwa ikishughulikia mchakato huo ikishirikiana na maofisa wa serikali ya Tanzania, ilidai nyongeza hiyo ilikuwa kwa ajili ya malipo kwa wakala, kampuni ya EGMA iliyopewa kazi ya kushauri mauzo hayo ya hati fungani ingawa fedha hizo zinadaiwa pia kutumika kuhonga maofisa wa serikali.
Hata hivyo, benki ya Standard ililazimika kurejesha fedha hizo kwa serikali baada ya kukubaliana na Taasisi ya Kupambana na Rushwa Kubwa ya Uingereza (SFO).
Hivi karibuni, taasisi isiyo ya kiserikali ya kupambana na rushwa ya Uingereza (Corruption Watch), ilipinga kitendo cha watuhumiwa wa suala hilo kuachwa kufuatia uamuzi wa makubaliano ya Mahakama (DPA) kati ya (SFO) na benki ya Standard Novemba 30 mwaka jana.
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Southwark ya jijini London, Uingereza iliamuru serikali ya Tanzania irejeshewe Dola za Marekani milioni tisa (sawa na Sh. bilioni 12.6) kutokana na kubainika kuwapo kwa udanganyifu baada ya kesi hiyo kufunguliwa kwenye mahakama kupinga asilimia moja ya ziada ya mkopo huo ambayo ililipwa kwa EGMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI
Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...
-
Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Uingereza Johanna Konta amemshinda Venus Williams 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili ya shindano la tenisi ...
-
Wakali wa ‘comedy’ kwenye tasnia ya Bongo Movies, Mzee Majuto, Asha Boko na Mzee Majanga wamefanya kweli kwenye filamu yao mpya inayokwend...
No comments:
Post a Comment
yes by message