Katika baadhi ya mikoa kusini na Pwani ya Tanzania, suala la binti kupatiwa mafunzo maalumu ya kimila ni desturi ambayo si ngeni, wao wanaita kumtoa mwari.
Utamaduni huo ujumuisha wasichana kuwekwa ndani kwa muda wa miezi kadhaa kwa ajili ya ya kufundwa na wataalamu wa masuala hayo.
Jambo hili kwa binti ambaye hajalipitia huenda likawa na gharama kubwa katika maisha yake ya ndoa ya baadaye kwani huonekana kama vile hajui mambo mengi na zaidi yale ya kumridhisha mume wake kwa mjibu wa mila zao.
Miongoni mwa jamii inayotajwa kuendeleza mila hizi hata katika kipindi hiki cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia ni Wamakonde kutoka mikoa ya Kusini mwa Tanzania na baadhi ya wakazi wa wilaya za mkoa wa Pwani nje kidogo ya jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Aidha utamaduni huu umekuwa ukilaumiwa na baadhi ya watu kuwa ndio chanzo cha kusitisha wasichana wengi masomo wakiwa na umri mdogo,
Mara nyingi sherehe hizi pia huwa zinafanyika mara tu wasichana wanapomaliza darasa la saba(elimu ya shule ya msingi) au wengine hata kabla hawajamaliza elimu hiyo.
Wazaramo ni kabila maarufu nchini Tanzania ambalo linasifika zaidi kwa ngoma.
Kuna msemo wa utani nchini humo unaowahusisha wanawake wa kabila hilo kupenda kucheza ngoma.
Lakini je, sifa hiyo wameipata kutokana na mafunzo waliyopitia?
Utaratibu wa shughuli hii ukoje na una maana gani katika jamii yao.
Mwandishi wa BBC Fatma Abdala aliweza kutembelea eneo la kisarawe mkoa wa Pwani na kutaka kufahamu zaidi juu ya utamaduni huu.
''Kwa sisi Wazaramo suala hili ni muhimu sana,na kabila letu ni moja ya makabila yanayopenda kuhakikisha kwamba wasichana wanashiriki shughuli zote na kisha kutolewa Mwali baada ya kukamilisha taratibu zote,na kwa wazaramo maandalizi ya sherehe hizo ni makubwa'' Bi Amina .
Ameongeza kuwa kuna mambo muhimu ambayo wasichana hawa hufundishwa na kungwi suala zima la mahusiano ya kawaida na watu wengine,mapenzi na ndoa kwa ujumla. mwanume kabla ya ndoa .
Mtaalamu mwingine wa shughuli hizo anabainisha kuwa mpaka mtoto anapotolewa na kuchezewa ngoma kama mali huenda akawa amekaa ndani kwa miezi kadhaa au mpaka mwaka mzima.
"Sherehe hii ni kubwa kwetu, huwa tunachanga fedha kwa ajili ya kuja katika sherehe hizo za kumcheza mwari na hata tunavaa sare", Bi.Halima anaeleza.
Licha ya kuwacheza wanawake, kabila hili nalo linawacheza wanaume yaani wanapeleka jando...ili waweze kupata mafunzo wakati wa kubalehe.
Kwa mujibu wa bi. Saada ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo ansema wanacheza mwali binti kuanzia umri wa miaka kumi, binti huyu huelekezwa unyumba namna ya kukaa na mume wake, nguo za kuvaa akiwa na mumewe, chakula cha kupika na kadhalika.
Pamoja na kuwa tamaduni hii imekuwa ikiendelee kwa miaka mingine, athari zake zimetajwa kuwa kubwa katika upande wa kuongeza idadi ya mimba za utotoni na hata kushusha maendeleo katika jamii hizo.
Hii ni kutokana na sherehe hizo pia kumuacha wazi mwali hadharani katika mavazi na hataka kuwa ishara ya kutangaza kuwa amekuwa na yuko tayari kwa wanaume.
Kwa upande wake Bi. Saum anasema kuwa hali hiyo inatokea kwa sababu wasichana wengi wanafanya tofauti na wanavyoelekezwa na hivyo kupelekea mabinti wadogo kubeba ujauzito na kubatili maana iliyolengwa.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa utamaduni ni heshima kwa mwanamke.
"Kuchezwa kuna raha yake lakini mwali wa kizaramo asipochezwa huchukuliwa kama hajakua mkubwa na hupelekea muda mwingine kukosa mume na hata kubaguliwa na wasichana wenzake waliopitia unyago," bi Halima anasisitiza.
Lios Media
No comments:
Post a Comment
yes by message