Viongozi wala rushwa, makampuni ya ndani na ya nje kwa pamoja wamekuwa wakishirikiana kutorosha mabilioni ya dola nchini Nigeria
Imefahamika kwamba matajiri nchini Nigeria hutorosha pesa zao na kuzipeleka katika maeneo yajulikanayo kama “pepo za kodi”
Mkutano wa 8 wa Umoja wa mataifa unaohusu mapambano dhidi ya uharamia na rushwa umefanyika Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. Dhima ya mkutano huo ilikuwa ukwepaji kodi.
Waziri wa sheria wa Nigeria, Abubakar Malam katika hotuba yake kwenye mkutano huo alisema kwamba matajiri wa nchini Nigeria wametorosha kiasi cha dola bilioni 400 kuzipeleka katika maeneo yajulikanayo kama “Pepo za kodi.”
Malama aliashiria kwamba viongozi wala rushwa mashirika ya ndani nay a kigeni kwa pamoja wanashirikiana katika kufanya uhalifu huo wa kutorosha pesa na kuzipeleka nje ya nchi. Katika kulidhibiti suala hilo serikali imechukua tahadhari za kutosha alisisitiza Malam
No comments:
Post a Comment
yes by message