Thursday, 19 December 2019

Dawa za nywele huongeza hatari ya saratani ya matiti

Utafiti uliofanywa huko nchini Marekani umeonyesha kwamba wanawake wanaotumia dawa za nwyele wapo katika hatari kubwa ya kuugua saratani ya matiti


Dawa za nywele huongeza hatari ya saratani ya matiti

Hatari ya kupata saratani ya matiti kwa wanawake wanaotumia dawa kunyoosha na kubadili rangi nywele ni kubwa zaidi.
Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na SciTechDaily limechapisha matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya afya ya Marekani na kuchapishwa katika jarida la "International Journal of Cancer".Utafiti huo ulijumuisha wanawake elfu 46 na 709. Matokeo yalionyesha kwamba wanawake wanaotumia dawa hizo za nywele mara kwa mara wana hatari ya kupata saratani ya matiti kwa asilimia 9 zaidi ukilinganisha na wale wasiotumia.
Wanawake wenye asili ya kiafrika ambao hutumia dawa hizo za nywele kila baada ya wiki 5 hadi 8 wana ongezeko la hatari ya kupata kansa ya matiti kwa asilimia 60.

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...