Matukio ya Afrika
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa afanya mazungumzo Tripoli
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya amefanya mazungumzo mjini
Tripoli, akitafuta kuuhimiza utawala mjini humo kuheshimu mpango wa
kuunda serikali ya umoja wa kitaifa inayoweza kumaliza miaka kadhaa ya
umwagaji damu

mpango wa kugawana madaraka, alikutana siku ya Alhamisi na wawakilishi wa serikali inayotambuliwa na jamii ya kimataifa karibu na makao yake makuu mashariki mwa nchi hiyo. Kisha jana akakutana na Nouri Abusahmein, mkuu wa bunge pinzani la Tripoli. Libya imekuwa katika machafuko tangu kuondolewa madarakani mwaka wa 2011 aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi na sas ina serikali mbili na mabunge mawili.
Makundi ya jihadi kama vile Dola la Kiislamu yamechukua nafasi hiyo ya kukosekana utawala thabiti kuingia katika ukanda wa pwani, na Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa mapigano yamewalazimu watu 435,000 kukimbia makazi yao.
Mnamo Desemba 17 mwaka jana, chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, wajumbe kutoka pande zote na viongozi kadhaa wa kibinafsi walisaini mpango wa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.
No comments:
Post a Comment
yes by message