Matukio ya Kisiasa
Polisi ya Munich ilifahamu kuhusu kitisho cha ugaidi
Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Ujerumani umeonyesha kuwa
maafisa walijua kuhusu uwezekano wa kutokea shambulizi katika mji wa
kusini wa Munich kabla ya siku kuu ya Krismasi.
Gazeti la Ujerumani la Süddeutsche, pamoja na mashirika ya utangazaji ya
WDR na NDR yaligundua kuwa maafisa - wakiwemo wa ofisi za mambo ya
ndani na mwendesha mashtaka - walikuwa na habari ya uwezekano wa kutokea
shambulizi la kigaidi mjini Munich tangu Desemba 23.Mkuu wa polisi mjini Munich amesema walikuwa na "habari za kuaminika" kuhusu kitisho cha ugaidi, hali iliyowalazimu mamlaka mjini humo kufunga kituo cha treni. Waziri wa mambo ya ndani Thomas de Maiziere amesema katika taarifa kuwa hali barani Ulaya na Ujerumani inaendelea kuwa mbaya katika Mwaka Mpya.
No comments:
Post a Comment
yes by message