Raia huyo ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani Reinhard Bonnke, ambaye alivutia umati mkubwa wa watu barani Afrika wakati wa mahubiri yake anaombolezwa na mamilioni ya Wakristo barani humo kufuatia kifo chake akiwa na umri wa miaka 79.
Mwandishi wa Kenya Jesse Masai anatazama ushawishi wake.
Akilinganishwa na wahubiri wengine wa Uingereza kama vile Charles Spurgeon hadi Billy Grahama wa Marekani , hadhi ya Bonke kama baba wa mahubiri ya kisasa ipo juu sana.
- Wahubiri' wageuka washambuliaji Nigeria
- Kutana na watoto wahubiri. Je ni sawa?
- Wachungaji 6 wa baadhi ya makanisa yaliyofungwa Rwanda wakamatwa
Katika bara la Afrika kumekuwa na mahubiri ya wiki moja , yanayoshirikisha idadi kubwa ya watu, mahema mengi , majukwaa ya kuvutia, vipaza sauti vya hali ya juu, wakalimani na mara nyingine wahubiri wakiiga jinsi Bonke alivyokuwa akifanya mahubiri yake hususan matamshi na jinsi alivyoshikilia kwa kutumia nguvu kipaza sauti.
Mwisho wa hotuba zake angewauliza ni nani kati ya walioko katika kongamano hilo alikuwa akisikia wito wa Mungu ili kuchukua kipaza sauti hicho kutoka kwa mikono yake.
Ujumbe wake wa matumaini hususan miongoni mwa mataifa ya Afrika ambayo yameathiriwa na ukame na majanga mengine ulikuwa muhimu.
Je Reinhard Bonnke alikuwa nani?
- Alizaliwa 1940 mjini Königsberg, Ujerumani
- Alianzisha shirika la Christ For All Nations (CFAN) 1974
- CFAN linadai kwamba Bonnke alisaidia kuingiza takriban watu milioni 79 katika Ukristo
- Alifariki tarehe 7 mwezi Disemba 2019
Wengine kama vile mhubiri mwenye umri wa miaka 83 wa kanisa la Pentocostal Wilson Mamboleo - ambaye alisaidia mahubiri ya Bonnke katika eneo la Afrika mashariki anadai kwamba wahubiri wakuu barani Afrika kama vile muhubiri wa Nigeria TB Joshua na Teresia Wairimu wa Kenya ni miongoni mwa walioshawishiwa na Bonnke.
'Waliokufa walifufuka'
Bonnke alijiunga na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakati wa kuanzishwa kwa kanisa la Muhubiri Wairimu la Faith Evangelistic Ministry mjini Nairobi mwezi Agosti 2016.
Shirika lake la Christ For All Nations (CFAN) , linalojulikana kwa kazi yake barani Afrika linadai Bonnke alisimamia zaidi ya watu milioni 79 katika Ukristo.
Katika mikutano mikuu ikiwemo mmoja uliofanyika katika mji wa Lagos , 2000 uliodaiwa kuvutia takriban watu milioni 1.6- Bonnke alidai kwamba ana uwezo wa kuponya kwa kutumia uwezo wa Mungu.
Pia aliwaambia wafuasi wake kwamba alishuhudia watu wakifufuka , licha ya kwamba miujiza kama hiyo ilipingwa na wakosoaji wake.
Countries with the largest Christian populations
Five of top 10 projected to be in Africa by 2050
Uhubiri wa Bonnke mara nyengine ulizua utata.
Stephen Mutua ambaye kati ya mwaka 1986 na 2009 alikuwa mkurugenzi wake wa kimataifa anakumbuka ghasia katika eneo la Waislamu la Kano nchini Nigeria 1990.
Waislamu walikuwa wamekasirishwa na hatua ya Bonnke kupata ruhusa ya kuhubiri katika eneo hilo.
''Katika ghasia hizo, nilijikuta katika gari ambalo haliwezi kuingia risasi kwa mara ya kwanza katika maisha yangu , kabla ya jeshi la Nigeria kutuondoa kwa ndege hadi mjini Lagos'' , Dkt Mutua anakumbuka.
Bonnke ambaye alikuwa akielewa hali ya kidini ya Nigeria , aliomboleza na taifa hilo katika ujumbe kwa serikali ya kijimbo katika eneo hilo na kuapa kurudi.
Kirasmi takriban watu wanane waliuawa lakini ripoti ambazo hazikuthibitishwa zinasema kwamba mamia ya watu walipoteza maisha yao.
''Baada ya kisa hicho tulinyimwa Visa na hatukurudi tena Nigeria kwa miaka 10''.
Dkt Mutua ambaye sasa anaongoza kanisa la African Evangalist Network mjini Nairobi, anasema kwamba mambo yalibadilika wakati rais Olesegun Obasanjo alipochukua madaraka 1999.
Anasema kwamba Nigeria, ambalo ndio taifa lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika limekuwa likimkaribisha Bonnke zaidi ya taifa jingine lolote lile la Afrika.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari , Muislamu kutoka kaskazini alimuomboleza muhubiri huyo akisema kwamba kifo chake kilikuwa hasara kubwa kwa Nigeria na dunia nzima kwa jumla.
No comments:
Post a Comment
yes by message