Friday, 7 October 2022

Baraza la Haki la UN kumteua mchunguzi huru dhidi ya Urusi

 Schweiz Genf | Sitzung UN-Menschenrechtsrat

Baraza hilo la Haki za binadamu lenye wanachama 47 limepasisha pendekezo hilo lililowasilishwa wiki iliyopita na nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya isipokuwa Hungary. Muda mfupi kabla ya kupiga kura hiyo huko mjini Geneva, Shirika la kutetea haki za binadamu la Russia Memorial lilitajwa kuwa mshindi mwenza wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka huu wa 2022.

Pendekezo la awali lilidhihirisha wasiwasi kuhusu kufungwa kwa wingi kwa vyombo huru vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na makundi ya upinzani nchini Urusi. Wanachama walio wengi wa Baraza hilo waliafiki kuteuliwa kwa "kamati maalum" itakayoendelea kufuatilia matukio ya ukiukaji wa haki nchini Urusi, kwa kutegemea kwa kiasi fulani msaada kutoka kwa makundi ya wanaharakati wa urusi ambao bado wapo nchini humo na hata nje ya nchi.

Soma zaidi:Umoja wa Mataifa kuamua juu ya uchunguzi Ukraine 

Urusi ambayo ilikuwa mwanachama wa Baraza la Haki za binadamu hadi mapema mwaka huu kabla ya kujiondoa kwake,  imechukua hatua kadhaa za kufifiza upinzani wa ndani kutokana na vita vyake nchini ukraine, ikiwa ni pamoja na kupitisha sheria inayopiga marufuku kueneza habari "za uongo" kuhusu jeshi la Urusi. 

Soma zaidi: Urusi yasimamishwa uanachama baraza la haki za Binaadamu la UN

Idadi ya vifo Zaporizhzia yaongezeka

Ukraine | Raketenangriff auf Saporischschja

Vikosi vya zima moto vya Ukraine vikijaribu kuuzima moto baada ya shambulio huko Zaporizhzhia mnamo Oktoba 6, 2022, moja mwa matukio ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Idadi ya waliofariki kutokana na shambulio la makombora katika eneo la makazi huko Zaporizhzhia imeongezeka na kufikia watu 11 huku kwa mara ya kwanza kabisa, ndege zisizo na rubani na zilizobeba vilipuzi zimefanya mashambulizi katika mji huo wa kusini mwa Ukraine na ambako kuna kinu kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi hayo:

" Urusi imeshambulia tena kwa makombora. Kwa bahati mbaya, kuna vifo, watu waliojeruhiwa, na majengo yaliyoharibiwa. Huko Zaporizhzhia, baada ya shambulio la kwanza la roketi, wakati watu wakiondoa vifusi, Urusi ilifanya shambulio la pili la roketi. Ni uovu na ukatili wa hali ya juu. Kumekuwa na maelfu ya matukio kama haya. Na kwa bahati mbaya mengine zaidi huenda yakashuhudiwa

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...