Muungano wa Afrika, AU, umetoa wito
kwa viongozi wa mataifa matano kuishawishi Burundi kukubali kikosi
maalum cha kudumisha amani kufuatia miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa
nchini humo.
Kamati hiyo maalumu ya AU, inamshirikisha Waziri Mkuu wa
Ethiopia, pamoja na Marais wa Afrika Kusini, Mauritania, Gabon na
Senegal.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amepinga mpango huo, akisema huo ni uvamizi.
Uamuzi wake wa mwaka uliopita kutaka kugombea awamu ya tatu ulianzisha mapigano hayo ambapo kufikia sasa mamia ya watu wameuawa.
Image copyrightImage caption
Viongozi wa Umoja wa Afrika
Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana juma
lililopita walighairi juu ya swala la kuwatuma wanajeshi 5,000 wa
kudumisha amani, na badala yake wakaamua kutumia njia za kidiplomasia.
No comments:
Post a Comment
yes by message