Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema tofauti baina ya watu sio tishio bali ni utajir
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN)Antonio Guterres, amesema inaonekana kuna ongezeko katika kutoheshimu haki za binadamu ulimwenguni, “xenophobia” na kesi za ubaguzi wa rangi pia zimeongezeka.
Guterres, ambaye yuko huko Roma, mji mkuu wa Italia kwa dhiara rasmi, alihutubia mkutano mkuu wa bunge la Italia, katika kikao maalum kilichofanyika kwa heshima yake.
Guterres alizungumzia kuhusu ubaguzi na siasa za “kipopulism”
“Ulimwenguni kwa ujumla tunaona kuna ongezeko la kutokuheshimu haki za binadamu pamoja na ongezeko la chuki dhidi ya wageni “Xenophobia” na ubaguzi wa rangi.
Wanasiasa wa kipopulism hutumia fursa ya watu kutokuridhika kujipatia madaraka na umaarufu, Ni budi kupingana na wanasiasa wa aina hiyo kwa ujasiri na uongozi madhubuti”
“Inahitajika muungano wa kijamii ili kila mmoja aweze kuwa sehemu ya jamii na kuheshimu utambulisho wa kila jamii”.
Katibu mkuu aliongeza kwamba mikakati mipya inaandaliwa katika kuzilinda dini na kupiga vita lugha za chuki.
Kisha alituma salamu Ulaya. “Tunahitaji Ulya yenye nguvu, umoja na malengo kwani katika hali hiyo tofauti haziwezi kuleta changamoto”.
Kuhusiana na suala la wahamiaji haramu, Guterres alisema “ Nchi za Mediterranea, Italia na ugiriki zina haki ya kutegemea mshikamano na ushirikiano kutoka Umoja wa Ulaya”, Lakini mpaka hivi sasa nchi hizo hazijaona mshikamano huo.
No comments:
Post a Comment
yes by message