Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha
wizara hiyo, Waziri aliyasema hayo wakati akitoa mwelekeo wa utendaji wa
wakala huo akizungumza na watendaji wa TEMESA.
Alisema Serikali ya awamu ya tano inaitaka TEMESA kufanya kazi kwa
weledi ili kuongeza mapato na kuhudumia wateja wao kikamilifu ili
kuinua uchumi wa wakala huo na kuondoa malalamiko kwa wadau na
watumishi.
‘Acheni kufanya kazi kwa upendeleo na usiri kwani huo ndio mwanzo
wa hujuma na ubadhirifu hali inayochochea malalamiko na kudumaza huduma
za TEMESA,” alsiema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa aliitaka TEMESA kuhakikisha inatengeneza magari ya
wadau wote kwa wakati na kutoa huduma za vivuko kwa ufanisi na
kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kukuza mapato na kuboresha huduma
za ufundi na umeme.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano sehemu ya ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga aliitaka TEMESA
kuongeza bidii Katika kukusanya madeni yake ili ipate uwezo wa
kibiashara na hivyo kumudu ushindani wa kibiashara.
Mtendaji mkuu wa TEMESA Mhandisi, Marceline Magesa alimhakikishia
Waziri Mbarawa kuwa TEMESA inaendelea na mkakati wa kujenga vivuko
vipya viwili ili kuongeza huduma hiyo katika eneo la Magogoni jijini Dar
es salaam na Pangani mkoani Tanga.
Aidha, alimhakikishia waziri kuwa ukarabati wa vivuko unazingatiwa
na uboreshaji wa karakana unaendelea ili kuvutia wadau wengi kutengeneza
magari yao katika karakana hizo.
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ulianzishwa mwaka 2006 kwa lengo
la kusimamia huduma za ufundi, umeme na usimamizi wa vivuko ambapo hadi
sasa takriban vivuko 28 vinasimamiwa na wakala huo nchini kote.
BY Lios Media
duuu noma sana
ReplyDelete