Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo wakati akizungumza na madaktari,
wauguzi na watumishi wa hospitali hiyo katikati ya wiki wakati wa ziara
yake mkoani humo.
Majaliwa alisema utaratibu wa kutenga chumba maalum chenye
madaktari wawili kwa ajili ya kuhudumia wazee unaotekelezwa hospitalini
hapo, umeondoa adha ya kusubiri matibabu kwa muda mrefu kwa rika hilo.
Alisema hospitali ya Mkoa wa Ruvuma imethibitisha kwamba agizo la
kutaka hospitali zote za Serikali nchini ziwe na dirisha maalum kwa
ajili ya wazee na watibiwe bure, linatekelezeka na kuzitaka hospitali
zote nchini kuiga mfano huo.
“Hospitali zote nchini ziige mfano wa hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
kwa kuwaheshimu wazee wanaokwenda kutibiwa katika hospitali hizo kwa
kuanzisha dirisha maalum kwa ajili yao; kama agizo la serikali
linavyosema na wasitozwe malipo ya aina yoyote” alisema Waziri Mkuu.
Aidha, Majaliwa alishauri uwekwe utaratibu wa kuwapa kipaumbele wazee wanapokwenda kuchukua dawa ili wasisubiri kwa muda mrefu.
Awali, Waziri Mkuu alitembelea chumba maalum cha wazee ambapo
alipata fursa ya kuzungumza na Antonia Moyo, ambaye alisema hajawahi
kutozwa fedha wala kukaripiwa wakati wote alipofika hospitalini hapo kwa
ajili ya matibabu kupitia dirisha la wazee.
Waziri Mkuu Majaliwa pia ametembelea wodi mbalimbali, chumba cha
upasuaji na duka la dawa kwa wagonjwa wanaotumia huduma za Bima ya Afya.
Waziri mkuuu Kasim Majaliwa Kasim by Lios Media
No comments:
Post a Comment
yes by message