Wednesday, 13 January 2016

Samatta azawadiwa na serikali ya Tanzania

Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa nyumbani Mbwana Samatta amekabidhiwa sehemu ya ardhi na serikali ya Tanzania kufuatia uhodari wake uliomwezesha kuondoka na tuzo hiyo na kuisaidia TP Mazembe kutwaa kombe la vilabu bingwa Afrika.
Mchezaji huyo pia alitunukiwa zawadi nyinginezo kwenye hafla iliyoandaliwa ili kusherekea mafanikio yake katika soka yaliyoiweka Tanzania katika ramani ya soka.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wadau wa michezo nchini Tazania wakiwemo waziri wa michezo Nape Nnauye na Thomas Ulimwengu ambaye ni mchezaji mwenza wa Samatta.
Amepewa kipande cha ardhi eneo la Kigamboni, Dar es Salaam na serikali kupitia wizara ya ardhi na nyumba.
Mchezaji huyo pia ameteuliwa nahodha mpya wa timu ya taifa Taifa Stars, nafasi ambayo awali ilishikiliwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anayeichezea klabu ya Yanga.
Samatta, maarufu ‘Samagoal’ aliwapiku Robert Kadiaba na Bounedjah Baghdad wa Algeria anayeichezea klabu ya Etoile du Sahel na kutwaa tuzo hiyo.
Baada ya kupokea taji lake katika sherehe za kuwatuza wachezaji bora Afrika, mjini Abuja, Samatta alirejea Tanzania na baadaye kualikwa na Rais wa Zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Mnamo mwaka wa 2013, serikali ya Nigeria iliwakabidhi wachezaji wake sehemu ya ardhi mjini Abuja na pesa kwa kushinda kombe la Afcon.

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...