Wednesday, 13 January 2016

Obama: Uchumi wa Marekani unaimarika

Rais wa Marekani Barack Obama ametetea vikali utawala wake huku akielezea matumaini hali bora zaidi ya Marekani kwa siku zijazo katika hotuba yake ya mwisho kwa taifa hilo.
Alikosoa kauli zisizofaa zinazotolewa katika kampeni zinazoendelea za urais, akidai Marekani ina uchumi ''imara na wa kuaminika duniani''.
"yeyote anaedai kwamba uchumi wa Marekani unadidimia anaota ," rais Obama aliwaambia wabunge mjini Washington.
Hotuba hiyo kwa bunge la Congress ilielezea zaidi mafanikio yake kama vile sera yake ya mageuzi katika sekta ya afya.
Hotuba hii itakumbukwa tu si kwa maelezo yake juu ya sera, lakini pia ni tathmini yake kuhusu namna Marekani ilivyo bora zaidi kuliko Barack Obama alipoingia Mamlakani, anasema mhariri wa BBC wa Amerika kaskazini Jon Sopel
Rais Barack Obama Image copyright
Image captionRais Obama amepinga madai kwamba uchumi wa Marekani unadhoofika
Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tu uliopita na Bunge la Congress , hakukuwa na muda wala kura ya kuwezesha mengi kutendeka.
" Katika hotuba ya mwisho kwa bunge hili , sitaki kuongelea a tu kuhusu mwaka ujao . Nataka kuangazia juu ya miaka mitano ijayo , miaka 10 na zaidi,''alisema Obama. " Nataka kuangazia hali yetu ya baadae.''
Alipinga madai ya wanasiasa na wachanganuzi kwamba Uchumi wa Marekani unadhoofika.
Rais ObamaImage copyright
Image captionObama aliwaambia wabunge kuwa anajuta kwamba Democrats na Republicans wamekua maadui
Hata hivyo, aliongeza kuwa : " Kile kilicho sahihi - na sababu inayowafanya wamarekani wawe na shauku - ni kwamba uchumi umekua ukibadilika kwa namna mbali mbali ."
Alitoa wito kwa wapiga kura na wanasiasa kubadili kauli zinazotenganisha za kisiasa na ''kubadili mfumo wa kujitathmini wenyewe".
Bwana Obama alisema kuwa suala analojutia zaidi katika utawala wake ni kwamba Republicans na Democrats wamekua maadui baina yao.
Rais Barack Obama Image copyrightReuters
Image captionRais wa Marekani Barack Obama alionya juu ya kauli za wanasiasa kuhusu waislam na wahamiaji
Na alimbeza kwa njia isiyo ya moja kwa moja mgombea alie mstari wa mbele wa urais wa chama cha Republican Donald Trump ambae amekua akikosolewa kwa kauli zake kuhusu waislam na wahamiaji.
"wakati wanasiasa wanapowatusi waislam, wakati msikiti unapoharibiwa kwa maksudi, ama mtoto anapozomewa, hilo halitufanyi kuwa salama,'' alieleza Obama. " Hiyo sio kueleza mambo yalivyo. Ni kosa... Na ni kinyume na vile tulivyo kama taifa''
Pia alitangaza mpango wa utafiti wa matibabu ya saratani utakaoongozwa na makamu wa rais Joe Biden. Pia alizungumzia suala la siaha kwa ufupi.

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...