Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, ameivunja Bodi ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika vya Wakulima wa Tumbaku mkoani Iringa (ITICOJE).
Sambamba na hatua hiyo, amewafukuza kazi viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika vya wakulima wa tumbaku, waliojaribu kujimilikisha matrekta yaliyokopwa na vyama vyao.
Nchemba alitoa kauli hiyo jana alipozungumza kwenye kikao alichokiitisha kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa wa Iringa kwa lengo la kusikiliza malalamiko ya wakulima wa tumbaku waliokuwa wakiwalalamikia viongozi wao.
Malalamiko hayo ya wakulima nusura yamponze Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Iringa, Kisa Samuel, ambao waliotoa mkopo huo wenye kila dalili ya ufisadi. Mkurugenzi huyo alitakiwa kujibu kwa nini benki imetoa mikopo hiyo yenye harufu ya ufisadi.
Nchemba alisema CRDB mbali na kutaka fedha za watu ambao ni wanachama, imewaacha wanaohodhi matrekta wakati tangu mwanzo walijua wanatumia mwavuli wa vyama kuwatapeli wakulima.
Hata hivyo, Kisa alisema wameingia mkataba na vyama vya msingi na si mtu mmoja mmoja, ndiyo maana hata kadi zina majina ya vyama.
Katika mkutano huo ulidumu takriban saa nne, Nchemba alihitimisha kwa kusema: “Kuanzia leo nitamke kwamba yale matrekta kuanzia kadi zile, umiliki wa kadi, ratiba na mwonekano wake yaende kwenye vyama vya msingi ambavyo ndivyo vimelipia matrekta.
No comments:
Post a Comment
yes by message