Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imewaomba wananchi kupendekeza kwa maandishi ya nauli zitakazotumika katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) wa jijini Dar es Salaam.
Huduma katika kipindi cha mpito zimepangwa kuanza Jumapili wiki hii. Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Gilliard Ngewe, alitoa rai hiyo juzi baada ya nauli zilizopendekezwa na Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDA-RT) kukataliwa.
Mapendekezo hayo yalikataliwa katika mkutano wa wadau wa usafiri, uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee. UDA-RT itatoa huduma za kipindi cha mpito.
Alisema katika kuamua suala la nauli, SUMATRA haiwezi kuangalia tu mapendekezo ya waendeshaji, bali inazingatia pia maoni ya wadau, wananchi na hali halisi ya nchi. Aliahidi kwamba maoni na mapendekezo yote yatapewa uzito wakati wa kuamua nauli zitakazotumika. “Sisi ni wadhibiti, maoni yenu yatafanyiwa kazi na endeleeni kujenga utamaduni wa kushiriki majadiliano kama ilivyo hivi leo (juzi). Hii itasaidia mamlaka kufanya kazi zake kwa urahisi na kwa maslahi ya nchi”, alisisitiza.
Amewahakikishia wananchi kuwa nauli zitakazopangwa ndizo tu zitakazotozwa na wenye mabasi na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment
yes by message