Kufuatia mashitaka matatu ya ufisadi aliyofunguliwa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuliomba bunge limpe kinga dhidi ya mashitaka yanayomkabili
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema atawasilisha maombi bungeni ya kupewa kinga dhidi ya mashitaka matatu tofauti ya ufisadi aliyofunguliwa na mwendesha mashitaka mkuu wa Israel, Avichai Mandelblit.
Katika taarifa aliyoitoa wiki iliyopita Netanyahu alisema kinga ni katika misingi ya kidemokrasia na akaashiria kwamba ataomba kinga hiyo bungeni.
Wataalamu wa Israel wanasema kwa hali iliyopo itakuwa ngumu kwa Netanyahu kupewa kinga hiyo na bunge.
Muda mfupi baada ya taarifa ya Netanyahu, kiongozi wa kambi ya upinzani Benny Gantz alisema,
"Kinga kwa Netanyahu ni kuvunja misingi ya usawa wa kisheria kwa kila mmoja, Netanyahu anafahamu kwamba yeye ni muhalifu”.
No comments:
Post a Comment
yes by message