Tuesday, 17 December 2019

Wafahamu Nyota watano wa muziki wa Afrika wa kuangaliwa siku zijazo

Wizkid performing at the Brixton Academy in 2012

Wakamuziki kama vile Davido, Wizkid na Burna Boy kwa sasa wanatambulika kama nyota wakuu wa muziki kote duniani, na nia ya dunia katika muziki wa Kiafrika haijawahi kuwa ya kiwango cha juu kama ilivyo kwa sasa.
Mnamo mwaka 2019, Beyoncé aliwachagua baadhi ya wanamuziki nyota wa Afrika kushiriki katika albamu yake iliyopata umaarufu iliyotokana na filamu ya Lion King huku Mr Eazina Burna Boy wakicheza muziki wao katika tamasha la mwaka la muziki la Coachella mjini California.
Wafuatao ni nyota Watano wa kuawaangalia katika mwaka 2020.

Sheebah Karungi (Uganda)

Sheebah
Akiwa na mafanikio ya kimuziki katika nchi yake ya Uganda, muziki wa Sheebah sasa unavuka mipaka.
Akiwa na sauti mahiri, Sheebah ni msanii mwenye malengo.
Kuanzia kushirikiana na wasanii wengine wa Kiafrika hadi densi, mtindo wake wa fasheni, anatumia talanta yake kuupeleka muziki wa Uganda kote dunaini.
Ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa. Kimaisha yupo tu kama mwanamke mwingine yeyote wa kawaida, na ndio maana anaweza kuwasiliana vema na mashabiki wake.
Lakini anapokua jukwaani, anabadilika na kuwa Superstar - mahiri na mwenye

Joeboy (Nigeria)

Joeboy

Joeboy alipata umaarufu kwa wimbo wake Baby, ambayo ilitazamwa na watu milioni 18 katika kipindi cha miezi tisa kwenye mtandao wa YouTube.
Akiwa na sauti inayotoka moyoni na kujielezea kwa ustadi katika mtindo wa kipekee wa nyimbo zake, mwimbaji huyu wa Nigeria huwasilisha mistari ya nyimbo zake kwa mitindo ya Afrobeats na pop.
Muziki wake anaoutoa mmoja mmoja pia umekuwa ukipokelewa vema na wafuasi wake. Mei uliopita, muimbaji huyu alitoa wimbo ulioitwa Love & Light.
Anapata umaarufu haraka - kwa misingi ya nyimbo hizi mbili tu, na anakaribishwa kote Afrika na tayari ameshafanya onyesho la muziki wake nchini Uingereza.




No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...