Mke wa makamu wa rais wa Zimbabwe ameshtakiwa na jaribio la kutaka kumuua mumewe.
Mary Mubaiwa ambaye tayari anashutumiwa kwa madai ya ufisadi, aliwasilishwa mbele ya mahakama moja ya Harare siku ya Jumatatu .
Amekana mashtaka yote.
Waendesha mashtaka wanasema kwamba alijaribu kumuua Jenerali Constantino Chiwenga wakati alipokuwa akipokea matibabu Afrika Kusini
Jenerali Chiwenga alihusika pakubwa katika kumpindua rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe mwaka 2017.
Jenerali huyo anadai kwamba bi Mubaiwa alijaribu kumzuia kupokea matibabu Afrika Kusini miezi sita iliopita.
Wakati alipolazwa hospitalini mjini Pretoria , imedaiwa kwamba aliutoa mrija wa kumpatia maji katika mkono wake.
enerali Chiwenga baadaye alielekea China kwa kipindi cha miezi minne kwa matibabu na kurejea mwezi uliopita.
Bi Mubaiwa aliwekwa kizuizini huku mahakama ikikataa kumwachilia kwa dhamana.
Wakati alipokamatwa siku ya Jumamosi, maafisa wa polisi walisema kwamba bi Mubaiwa alishutumiwa kwa mashtaka ya ulaghai na ulanguzi wa dola milioni moja.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya Afrika Andrew Harding anasema kwamba kesi hiyo inaenda sambamba na mfumo wa taifa ambalo wakuu wa taifa hilo wanashutumiana kwa kupanga njama za mauaji na kuwekeana sumu ambapo maafisa wa polisi na mahakama hutumika.
Zimbabwe inakabiliwa na kiwango cha juu cha mfumuko wa bei, ukosefu wa umeme na baa la njaa.
Lakini je Mary Mubaiwa ni nani?
Alizaliwa 1983 na ni mama wa watoto sita.
Ni mwana wa Kenny Mubaiwa, ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya soka ya Dynamos.
Ni mwanamitindo wa zamani na mke wa makamu wa rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga ambaye ni kamanda mstaafu wa jeshi la Zimbabwe.
Alikuwa mke wa Shingi Kaondera, mchezaji kandanda ambaye aliichezea klabu ya Caps.
Mwaka 2012 alikuwa msimamizi wa shindano la malkia wa urembo nchini Zimbabwe akichukua uongozi kutoka kwa mtangulizi wake Kiki Divaris hadi alipojiuzulu February 2018.
Alitarajiwa kuliimarisha shindano hilo nchini Zimbabwe.
Shindano la malkia wa urembo 2014 lilionyesha uwezo wake kwani liliwavutia wengi likiwa na mbwembwe za kila aina yake.
Mwaka 2014 malikia wa urembo watatu walitawazwa kuwa washindi wa tuzo hilo kwa pamoja wakiwa Thabiso Phiiri, Catherine Makaya na Tendai Hunda.
Hatua hiyo ilifuatiwa na shutuma kali dhidi ya Mary
Mitindo ya Mary Mubaiwa
Mary Mubaiwa amekuwa akiongea sana, anadaiwa ana majivuno mengi na hupendelea sana mtindo wake kibinafsi na anaamini kuwa ana fursa na haki ya kukumbatia na kuonyesha umbo lake la kuvutia na hadhi yake.
Anasema kwamba mavazi yake humuonyesha yeye ni nani na hayuko tayari kubadilisha ili kuwafurahisha wengine, na badala yake hubadili mitindo yake kutokana na uzingatiaji wake.
Pia anajivuna kwasababu mumewe, makamu wa rais Constantino Chiwenga anependa mitindo yake, akidai kwamba hawezi kutoka nyumbani kwake kwa vazi ambalo mumewe hajaliidhinisha kulingana na jarida la Whats hot in Africa.
No comments:
Post a Comment
yes by message