Tuesday, 17 December 2019

hii ni ndizi iliyobandikwa ukutani yalindwa na polisi

Ndizi iliyobandikwa ukutani yalindwa na polisi

Huko nchini Marekani ndizi iliyobandikwa ukutani yanunuliwa kwa thamani ya dola laki 1 na elfu 20

Huko nchini Marekani kazi ya sanaa ya msanii maarufu kutoka Italia mchongaji wa masanamu, Maurizio Cattelan ambayo ilijumuisha ndizi iliyobandikwa katika ukuta iliyokua ikiizwa kwa thamani ya dola laki 1 na elfu 20, imekuwa mjadala mtandaoni kutokana na msanii mwingine kuila ndizi hiyo na baadae kukamatwa na polisi.
Video zilizomuonyesha msanii wa vichekesho David Datuna akiila ndizi hiyo iliyokuwa katika maonyesho ya Cattelan yaliyokuwa yakifanyika katika ukumbi wa sanaa wa kimataifa wa Basel uliopo Miami zimesambaa katika mitandao ya kijamii hasa Instagram.
Mara baada ya Datuna kufanya kitendo hicho mfanyakazi wa mmoja wa maonyesho hayo walibandika ndizi nyingine na kuita polisi ili kuilinda kazi hiyo.
Naye mkurugenzi wa maonyesho hayo alisema kwama Datuna hajaribu kazi hiyo kwani, ndizi katika kazi hiyo ilikua ni fikra.
Nakala mbili za kazi hiyo ya sanaa zilinunuliwa kwa bei ya dola laki 1 na elfu 20, nakala ya 3 ilifahamishwa kwamba bei yake itakuwa dola laki 1 na elfu 50

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...