Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika dogo la ndege la Western Global Airlines ilisajiliwa nchini Marekani.
Yamkini ndege hiyo ya kibinafsi ilikuwa ikitoka Ujerumani ikielekea Afrika Kusini.
Mkuu wa halmashauri inayosimamia viwanja vya ndege vya Zimbabwe David Chawota anasema mamilioni ya pesa iliyopatikana katika ndege hiyo ni mali ya benki kuu ya Afrika Kusini.
Shirika la habari la FIn24la Afrika kusini linasema kuwa ndege hiyo sasa imekamatwa ilikuruhusu uchunguzi wa kina ufanyike.
''kama mnavyofahamu swala hili linahusu watu wa mataifa mengine na ndege inayomilikiwa na kampuni iliyosajiliwa huko Marekani kwa hivyo tayari hii ni swala linalohusu serikali kuu'' alisema Chawota
No comments:
Post a Comment
yes by message