Waziri wa mambo ya nje wa Iran , Mohammad Javad Zarif, ameuambia Umoja
wa Mataifa kwamba nchi yake haitaki uhasama uliopo kwa sasa mashariki ya
kati kuwa mbaya zaidi.
Mzozo baina ya Iran na Saudi uliibuka wiki
moja iliopita baada ya Ufalme wa Saudia kumuua kiongozi wa madhehebu ya
Shia kwa shutuma za ugaidiKatika barua yake kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon Bwan Zarif aliushutumu utawala wa Riyadh kwa kuunga mkono makundi yenye itikadi kali na kuanzisha vita visivyokuwa na maana nchini Yemen ambako muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unapigana na waasi wa Houthi wa Madhehebu ya Shia.
Kwa upande wake Saudi Arabia inasema serikali ya Iran inajaribu kupata ngome yake nchini Yemen kwa kuwaunga mkono Wahuthi.
Baraza la Utendaji la Ghuba linatarajia kukutana mjini Riyadh leo kujadili mzozo huo.
No comments:
Post a Comment
yes by message