Wednesday, 20 January 2016

Washukiwa wanne wa ugaidi wauawa Kenya


Bwana Marwa Amesema Washukiwa wawili wamefanikiwa kutoroka

Polisi nchini Kenya wamewapiga risasi na kuwaua washukiwa wanne wa ugaidi katika mji wa Malindi eneo la Pwani.
Mmoja wa washukiwa hao amekuwa akitafutwa na polisi nchini Kenya kwa kushukiwa kuhusika kwenye shambulizi lililoendeshwa katika chuo kikuu cha Garisa mwezi Aprili mwaka 2015.
Suleiman Mohammed Awadh, aliuawa pamoja na wenzake wakati polisi walifanya uvamizi mapema leo asubuhi kwenye nyumba moja ya mjini Malindameambia wanahabari kwamba wanne hao waliwashambulia wa polisi kwa guruneti na risasi kabla ya kuzidiwa nguvu na kuuawa.
Amesema polisi walipata silaha, ramani ya Malindi inayoonyesha maeneo ambayo walilenga kushambulia na barua iliyokuwa imeandikiwa wafadhili wa al-Shabab kuomba pesa, nguo na chakula.
Washukiwa wengine wawili wametoroka wakiwa na majeraha ya risasi, Bw Marwa amesema.

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...