Amekuwa akiishi pamoja na wakimbizi wengine katika kambi hiyo ambayo ni moja ya kambi tatu ambazo kwa pamoja hujulikana kama kambi za wakimbizi za Dadaab.
Amemwambia mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay kwamba changamoto kuu anayokumbana nayo kambini ni kwamba watu humfanyia mzaha. Watoto pia humfuata kila aendako.
Kutokana na upweke, yeye hutumia muda wake mwingi akitafuna miraa na kuvuta sigara.
Pesa hupata kutoka kwa wahisani kambini.
Wakimbizi wengine wanapopanga kurejea Somalia, Abdullahi hana mpango kama huo.
Anasema akirudi huko, ana wasiwasi kwamba hali ikiwa mbaya hawezi kukimbia na kutoroka kama watu wengine.
No comments:
Post a Comment
yes by message