Thursday, 14 January 2016

Liberia yatangazwa kuwa isiyo na Ebola

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Ebola nchini Liberia na kusema kuwa maambukizi yote ya ugonjwa huo yamemaliziwa katika eneo la Afrika Magharibi.
Lakini WHO inasema kuwa bado kazi haijamalizika. Visa zaidi vinaweza vikaripotiwa na ufuatiliaji wa hali ya juu utahitajika kuwepo miezi inayokuja.
Liberia ilitangazwa kwanza kuwa isiyo na ugonjwa wa Ebola mwezi Mei mwaka 2015 lakini ugonjwa huo ukalipuka tena mara mbili ambapo kisa cha mwisho kiliripotiwa mwezi Novemba mwaka 2015.
Image copyrightGetty
Image captionHata hivyo umoja wa mataia umeonya kuwa eneo la afrika magharibi huenda litashuhudia visa vya ungowa wa ebola
Tangazo la leo linatolewa baada ya siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho kutopatikana na virusi vya ebola.
Liberia inajiunga na Guinea pamoja na Sierra Leone ambazo zilipata kutangazwa kutokuwa na ugonjwa huo mwaka uliopita.
Licha ya hilo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, ameonya kuwa eneo la Afrika Magharibi huenda litashuhudia visa vya ungowa huo. Ebola umewaua zaidi ya watu 11,000 tangu mwezi Disemba mwaka 2013 .
By Lios Media

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...