Kimbunga kikali cha theluji kinachobashiriwa kuwa kikubwa zaidi kwa muda wa miaka mia moja kimewasili katika ufukwe wa Mashariki mwa Marekani.
Eneo linalotarajiwa kukabiliwa vikali ni mji mkuu wa Washington DC, ambako hali ya hatari tayari imetangazwa.
Afisi za wafanya kazi wa Serikali na shule zilifungwa mapema na huduma za usafirishaji pia kusitishwa
Zaidi ya watu milioni 50 wameonywa kuwa watarajie barafu ya kina cha zaidi ya futi mbili, itakayoongezeka kutokana na kimbunga na upepo mkali utakaovuma saa chache zijazo.
by Lios Media
No comments:
Post a Comment
yes by message