Kundi moja la wapiganaji wa jihad lililobuniwa miaka mitatu iliopita limekiri kutekeleza mashambulio mawili ya hoteli katika eneo la Afrika Magharibi katika kipindi cha miezi miwili.
Kundi hilo linalojiita al-Murabitoun ,lina makao yake katika jangwa la Sahara kaskazini mwa Mali na lina wapiganaji walio watiifu kwa mwanamgambo wa Algeria Mokhtar Belmokhtar.
Mnamo mwezi Novemba mwaka 2015,kundi hilo lilisema ndilo lililohusika na utekaji wa hoteli ya Radisson Blu Hotel katika mji mkuu wa Mali Bamako.
Taarifa ilioripotiwa na shirika la habari la Mauritania al-Akbar lilisema kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa ushirikiano na kundi la al Qaeda katika eneo la Islamic Maghreb{AQIM}.
Mwezi Januari mwaka 2016,taarifa iliotolewa na AQIM ilisema kuwa al-Murabitoun ndio lililoktekeleza shambulio hilo katika hoteli ya Splendid katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou.
No comments:
Post a Comment
yes by message