Kitabu kilichoandikwa na kiongozi wa
zamani wa Ujerumani Adolf Hitler kitaanza kuuzwa tena baada ya
hakimiliki za kitabu hicho kufikia kikomo.
Kitabu hicho kwa jina
Mein Kampf kilipigwa marufuku baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na
serikali ya Bavaria, ambayo ilimiliki haki za kitabu hicho.Hii ina maana kwamba hakuna yeyote ambaye angeweza kuchapisha au kusambaza kitabu hicho kwa miaka 70.
Kwa mujibu wa Sheria Ujerumani, hakimiliki hudumu kwa miaka 70.
Sasa hakimiliki ya kitabu hicho imefikia kikomo na Taasisi ya Historia ya Kisasa (IfZ) mjini Munich imesema itaanza kuuza nakala za kitabu hicho wiki ijayo
Nakala za kitabu hicho kinachoangazia sera aliyoifuata Hitler kilikuwa mwongozo wa utawala wa Nazi.
Hatua ya kuchapisha upya kitabu hicho imepingwa na makundi ya Wayahudi, yanayodai kazi za Sanaa za Nazi hazifai kuendelezwa.
Lakini wanahistoria wanasema kitabu hicho Mein Kampf (Mapambano au Mapigano yangu) kitasaidia wasomi kufahamu yaliyotendeka wakati wa uongozi wa Nazi.
Mein Kampf kilichapishwa mara ya kwanza 1925, miaka minane kabla ya Hitler kuingia mamlakani.
Majeshi ya muungano yaliyoshinda vita dhidi ya Ujerumani 1945 yalikabidhi hakimiliki ya kitabu hicho kwa jimbo la Bavaria.
No comments:
Post a Comment
yes by message