Thursday, 7 January 2016

Zidane ahimiza bidii Real Madrid

Kocha mkuu wa mpya wa Real Madrid Zinedine Zidane, amewataka Wachezaji wake kuwa na nia moja kwa kila mchezaji kufanya kazi kwa bidii.
Wachezaji wengi wa timu hiyo wameshukuru kuondolewa kwa Rafa Benitez ambapo wamepata morali mpya baada ya kuteuliwa kwa Zidane kwa kuwa wanaheshimu ujio wake.
Wachezaji hao wa Madrid wakiongozwa na mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo, wameapa kuwa na utiifu kwa kocha huyo na wameahidi kufanya kazi kwa bidii na umoja wa kitimu.
Kabla ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, Zidane aliwahutubia wachezaji wote na kuwaelezea mwongozo wake wenye msisitizo wa mambo mawili makuu ambayo ni kazi kwa bidii na kufurahia kazi hiyo.
Katika kuimarisha kikosi cha kwanza cha Madrid, Zidane, amewachukua wachezaji watatu kutoka kikosi B, ambacho hujulikana kama Castilla ambao ni Borja Mayoral na viungo Marcos Llorente na Martin Ødegaard ili waanze kufanya mazoezi katika kikosi cha kwanza.
Wakati huo huo imeripotiwa kuwa Madrid inajipanga kutenga kitita cha paundi milioni 100 kwa ajili ya kuwania kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard katika majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...