Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wanne Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na kutakiana heri ya Mwaka Mpya, wamezungumzia mambo mbalimbali kuhusu mustakabali wa Serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumzia yaliyojiri katika Mazungumzo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Assad amesema wamezungumzia kupunguza gharama za matumizi ya kuendesha serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Profesa Assad amebainisha kuwa Rais Magufuli ametaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ihakikishe Tanzania inaongeza ukusanyaji wa mapato kutoka asilimia 14 ya pato la Taifa (GDP) kwa mujibu wa hesabu zilizofanyika mwaka juzi.
"Hadi Mwaka juzi Tanzania ilikua inakusanya mapato kwa kiwango cha asilimia 14 ya pato la Taifa ikilinganishwa na Kenya ambayo ilikua ikikusanya asilimia 19 ya pato Taifa, na hakuna sababu za Msingi za kwa nini Tanzania iwe nyuma katika ukusanyaji wa mapato hayo"aliongeza Profesa Assad.
Rais Magufuli pia amekutana na Mkurugenzi wa Mashitaka hapa Nchini (DPP) Mheshimiwa Biswalo Eutropius Mganga ambaye amesema mazungumzo yao yalijikita katika suala la kupeana mikakati ya namna ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inavyopaswa kufanya kazi ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo "Hapa Kazi Tu"
No comments:
Post a Comment
yes by message