MISS Tanzania 2006, ambaye pia ni mwigizaji wa filamu za bongo, Wema Sepetu, amewataka wabunifu chipukizi wa mavazi na mitindo nchini walitumie vizuri jukwaa la mitindo la Lady In Red Fashion Show 2016, ili wafikie malengo waliyojiwekea.
Wema alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na onyesho litakalofanyika Januari 31, katika ukumbi wa Danken House, uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
“Kwa sasa mnatakiwa muwe wabunifu zaidi mje na vitu vya kipekee ili kazi hizo ziwe chachu na kivutio kwa wateja wenu, pia iwaongezee mashabiki wa mavazi na ajira yenu, iwe ya uhakika na soko,’’ alieleza Wema.
Naye Mkurugenzi wa Fabak Fashions na muandaaji wa jukwaa hilo, Asia Idarous, alisema jukwaa hilo ni shule na daraja la wabunifu wa mavazi na mitindo, hivyo litaendelea kuenziwa ili lizidi kuzalisha wabunifu wengi zaidi.by Lios Media
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI
Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...
-
Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Uingereza Johanna Konta amemshinda Venus Williams 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili ya shindano la tenisi ...
-
Wakali wa ‘comedy’ kwenye tasnia ya Bongo Movies, Mzee Majuto, Asha Boko na Mzee Majanga wamefanya kweli kwenye filamu yao mpya inayokwend...
No comments:
Post a Comment
yes by message