Tuesday, 19 January 2016

Unafahamu Unayoyapata Kwenye Pombe? Jua Chakufanya Hapa

Kubwa na zuri la kwanza ni kuburudika na kufurahi. Hakuna maisha bila furaha. Dunia ni njema tukifurahi.
Hata kwenye harusi ya Kana Yesu aligeuza maji mitungini ikafanywa wine safi na harusi ikanoga.
Ila kuna yanayoletwa na pombe ingawa hatuyakusudii. Hatuyapendi pia.
Kwenye kupunguza uzito hatukukatazi chochote. Tunakuelekeza na unaelewa unafanya maamuzi binafsi.
Mimi nimefanikiwa kuondoa zaidi ya kilo 45. Ndio nilikuwa na kilo 134 na hadi desemba 11 nilikuwa na 88. Nataka kuwa na 72 februari 2016 nikitimiza miaka 36. Niulize nakunywaje pombe na bado napungua? Napenda pombe, nakunywa pombe.
Pombe isikuzuie kuondoa uzito ulikuzidia.
Pombe za aina zote zina kemikali ambazo baadhi ya hizo kemikali huwa ni sumu mwilini,hivyo kuacha athari ya kiafya kwa mtumiaji.
Pombe inaweza ikamdhuru mtumiaji kwa kumsababishia madhara yafuatayo:
1.Vidonda vya tumbo.
2.Kansa ya utumbo.
3.Kusinyaa kwa Ini.
4.Kansa ya Ini.
5.Kansa ya umio(oesophagus)
6.Vindonda kwenye mapafu.
7.Utapiamlo hasa wale wanaokunywa huku lishe duni.
8.Matatizo ya ganzi miguuni na mikononi(Peripheral Neuropathy).
9.Kisukari.
10.Figo kushindwa kufanya kazi.(Renal failure)
11.Kansa ya figo
12.Kukosa au upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.(Loss of Libido)
13.Upungufu wa nguvu za kiume kike.
14.Kuongeza kasi kwa baadhi ya magonjwa hata kama unatumia dawa kama vile Kifua Kikuu,Kansa,Kisukari,Shinikizo la damu la kupanda.n.k
15.Kukosa hamu ya kula.(Anorexia)
16.Kutovyonzwa vyema kwa chakula(Malabosorption)
17.Ugonjwa wa kongosho.(Pancreatis).
18.Magonjwa ya moyo.
19.Mwili kutetema(Tremors)
by Lios Media

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...