Tuesday, 5 January 2016

UN yashutumu kuvamiwa kwa ubalozi Iran

Baraza la Usalama la Umoja wa

Mataifa limeshutumu vikali kushambuliwa kwa ubalozi wa Saudi Arabia nchini Iran na waandamanaji
waliokasirishwa na kuuawa kwa mhubiri wa Kishia.
Taarifa ya baraza hilo haijazungumzia kutekelezwa kwa hukumu ya kifo dhidi ya mhubiri huyo maarufu, Sheikh Nimr al-Nimr.
Saudi Arabia ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran Jumapili baada ya ubalozi wake kuvamiwa na kuchomwa moto.
Jumatatu, naibu waziri mkuu wa Uturuki Numan Kurtulmus alihimiza nchi hizo mbili kutuliza mgogoro huo, ikisema eneo la Mashariki ya Kati tayari limo hatarini ya kulipuka.
Baraza la Usalama la UN, likijibu barua kutoka kwa Saudi Arabia, limeshutumu shambulio hilo la katika ubalozi Tehran pamoja na shambulio katika afisi ya ubalozi wa Saudia Arabia katika jiji jingine la Iran la Mashhad.
Baraza hilo limeitaka Iran kulinda mabalozi na mali ya ubalozi pamoja na wafanyakazi wake “kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa”.
Limetoa wito kwa pande zote mbili “kushauriana na kuchukua hatua za kupunguza wasiwasi katika kanda hiyo”.

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...