Sunday, 17 January 2016

Rwanda kuwahamisha wakimbizi kutoka Burundi

Image copyrightAFP
Image captionWakimbizi Rwanda
Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa itaanza shughuli ya kuwahamisha wakimbizi kutoka Burundi walioko katika kambi za muda hadi kambi ya wakimbizi ya mahama kufikia mwisho wa mwezi huu.
Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa wizara inayohusika na masuala ya wakimbizi nchini, Frederick Ntawukuriryayo.
Ntawukuriryayo aliyasema hayo wakati alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa wakimbizi walioko katika kambi ya muda ya Gashora.
Kwa muda wakimbizi hao wamekuwa wakiitaka serikali ya Rwanda kuwahamisha hadi kambi ya Mahama ambayo wanasema ina vifaa vya kimsingi kama vile huduma za afya na elimu.
Afisa huyo amesema shughuli hiyo ilichukua muda kwa sababu wao walikuwa wakijenga nyumba zaidi ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao kutoka Burundi.
Kambi ya muda ya Gashora kwa sasa ina wakimbizi mia sita nayo kambi ya Nyanza ina wakimbizi mia nne ili hali kambi ya Rusizi inawakimbizi mia mbili.
Kwa sasa kambi hiyo ya Mahama ina zaidi ya wakimbizi elfu hamsini, elfu moja mia tano kati yao wakiwa wanafunzi.
Huku mzozo wa Burundi ukiendelea inakadiriwa kuwa kati ya wakimbizi hamsini na mia moja huingia nchini Rwanda kila siku.
By Lios Media

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...