Rais wa Ghana John Mahama amesema kuwa raia wawili wa Yemeni waliokuwa wafungwa katika jela ya Guantanamo Bay nchini Marekani si tishio kwa usalama wa taifa hilo ,kulingana na shirika la habari la Reuters.
Hatua ya serikali ya kuwapatia hifadhi wageni hao ambao hawakuhukumiwa kwa kutekeleza uhalifu wowote,imekosolewa na wengi nchini Ghana huku viongozi wa kikristo wakisema kuwa huenda wakawa tishio.
Shirika la habari la Reuters limemnukuu Mahama akisema kuwa raia yeyote wa Ghana anakabiliwa na tishio la kufariki barabarani kwa ajali ikilinganishwa na tishio linalosababishwa na wageni hao.
''Wanataka kuanza tena maisha yao ili waendelea kuishi kama watu wa kawaida.hakuna la kutuogofya''.
Awali mmoja ya wafungwa hao wa Guantanamo ,Mahmud Umar Muhammad Bin Atef,amekiambia kituo kimoja cha redio vile yeye na wafungwa wengine walivyoiunga mkono timu ya Black Stars,wakati wa kombe la dunia la mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment
yes by message