Saturday, 2 January 2016

Mhubiri wa Kishia anyongwa Saudi Arabia

Familia ya Sheikh Nimr al-Nimr inasema maandamano yake yalikuwa ya amani
Saudi Arabia imemuua mhubiri maarufu wa dhehebu la Kishia Sheikh Nimr al-Nimr, wizara ya masuala ya ndani imesema.


Mhubiri huyo ni miongoni mwa watu 47 waliouawa baada ya kupatikana na makosa yanayohusiana na ugaidi, imesema kupitia taarifa.

Sheikh Nimr aliunga mkono sana maandamano dhidi ya serikali yaliyochipuka mkoa wa Mashariki mwaka 2011, ambako Washia walio wengi walilalamikia kutengwa.

Kukamatwa kwake miaka miwili iliyopita kulisababisha maandamano yaliyodumu siku kadha.
Hukumu ya kifo dhidi ya Sheikh Nimr ilithibitishwa Oktoba.

Kakake amesema alipatikana na hatia ya kutafuta watu wa nje wa kuingilia masuala katika ufalme huo, kutotii watawala na kuchukua silaha kukabiliana na maafisa wa usalama.

Iran, inayoongozwa na Washia, awali ilikuwa imeionya Saudi Arabia, inayoongozwa na Wasunni, kwamba kumuua Sheikh Nimr "kuaigharimu Saudi Arabia pakubwa".
Maandamano yalizuka mkoa wa Mashariki mapema mwaka 2011 wimbi la misukosuko lilipokuwa likivuma katika mataifa ya Kiarabu.

Serikali ya Saudi Arabia imekanusha madai ya kuwabagua Washia na badala yake inaituhumu Iran kwa kuwachochea.

Saudi Arabia iliwanyonga watu zaidi ya 150 mwaka jana, idadi ya juu zaidi katika kipindi cha miaka 20.

No comments:

Post a Comment

yes by message

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...