Serikali ina mpango wa kukagua vyuo vikuu vyote nchini na vile ambavyo vitakuwa havina sifa itavifunga bila kusita kwani haitaki watanzania wafanyiwe majaribio katika elimu.
Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa Elimu,Prof. Ndalichako ambaye amesema vyuo vingi havina sifa licha ya vyuo hivyo kupewa ithibati.
Prof. Ndalichako amesema inatakiwa angalau asilimia 50 ya walimu katika kila chuko kikuu kimoja wawe na shahada ya uzamivu(Ph.D) na kwamba haitakiwi mwalimu mwenye shahada ya kwanza kufundisha wanafunzi wa shahada ya kwanza.
Prof. ameongeza kuwa uwepo wa vyuo vingi visivyo na sifa kunapelekea uwepo wa vijana wengi wasio na ajira mitaani na hivyo kuongeza hasira.
No comments:
Post a Comment
yes by message