Sunday, 9 October 2022

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

 

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baada ya mashabiki 125 kupoteza maisha uwanjani. Zipo taarifa zingine ambazo hazijathibitishwa zikionyesha idadi ya vifo ni zaidi ya 170.

Jumamosi usiku, maelfu ya mashabiki waliingia katika uwanja wa Kanjuruhan huko Malang, Java Mashariki, kushuhudia mechi ya kandanda kati ya vilabu viwili hasimu, lakini mechi ikageuka msiba, ikawa majonzi.

Mashabiki waliokuwa uwanja wa nyumbani walivamia uwanja baada ya timu yao kufungwa 3-2 dhidi ya Persebaya Surabaya. Polisi walijaribu kuwazuia kwa kurusha mabomu ya machozi, kukawa na kimbiakimbia, kukanyagana na hatimaye wengine kupoteza maisha wakiwemo watoto kadhaa, mmoja akiwa na umri wa miaka mitatu, mamlaka inasema.

Baadhi ya mashabiki walifia mikononi mwa wachezaji waliokuwa wamefika kuwashangilia, kocha wa timu ya nyumbani Arema FC alifichua.

Tukio la Indonesia sasa linashika nafasi ya pili duniani kwa matukio ya vifo yaliyoua watu wengi uwanjani. Kuanzia tukio la mashabiki wa Liverpool mpaka wale wa Ghana, yapo mengi, lakini haya matano yalitikisa dunia.

Liverpool

5: Mwaka 1996: Mashabiki 84 wafa mbele ya rais GUATEMALA

Mashabiki 84, walipoteza maisha baada ya kuibuka kwa ghasia na kusababisha mkanyagano kwenye uwanja wa taifa wa Mateo Flores, Guatemala katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia la mwaka 1998 kati ya Guatemala na Costa Rica.

Rais wa Guatemala wakati huo, Alvaro Arzu Irigoyen, alikuwepo uwanjani na kuagiza kuvunjwa kwa mchezo huo, usiendelee, na akatangaza maombolezo ya siku 3.

''Ilikuwa mbaya -- mbaya sana,'' alisema Marlon Ivan Leon, mlinzi wa timu ya taifa ya Guatemalan wakati huo, aliyeshuhudia maiti za mashabiki hao. Watu 147 walijeruhiwa.

4: Mwaka 1988: 93 wafa wakikimbia kimbunga uwanjani, Nepal

Maelfu ya mashabiki walikuwa katika uwanja wa taifa wa Nepal wakiangalia timu yao ya taifa ikimenyana na Bangladeshi. Inaelezwa kulikuwa na zaidi ya mashabiki 30,000 uwanjani wakati kimbunga kilipotokea kilichokwenda sabamba na mvua, radi na upepo mkali.

Katika kujiokoa na kimbunga, kilichosababisha mechi kusimama, mashabiki hao walikimbilia kwenye mageti ya kutokea ili kutoka, kwa bahati mbaya ni geti moja tu lililokuwa wazi.

Kwenye kugombea kutoka kupitia geti hilo, walikanyagana, kudondoshana na wengine kukosa pumzi ambapo mashabiki 93 walifariki dunia na mamia wengine kukimbizwa hospitalini.

3: Mwaka 1989: Vifo vya mashabiki 96 wa Liver -Hillsborough

Liverpool

Hili ni tukio baya zaidi katika historia ya matukio ya uwanjani yaliyosababisha vifo nchini England, ilikuwa mwaka 1989,katika uwanja wa Hillsborough, Sheffield.

Tukio hili lilisababisha vifo vya mashabiki 96 wa Liverpool wengine wakitaja 97, waliokwenda kuhudhuria mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA Cup dhidi ya Nottingham Forest.

Kwa mashabiki wa Liverpool ni tukio lisilosahaulika na kwa zaidi ya miaka 30, waliendesha kampeni ya kujua mambo mawili tu, ilikuwaje na kwa nini mashabiki wa timu hiyo walifikwa na umauti.

2: Mwaka 2001: Mashabiki wachukizwa na kipigo, 126 wafa, Ghana

Ghana

CHANZO CHA PICHA,GHANA N

Vifo 126 katika uwanja wa michezo wa Accra, Ghana mwaka 2001, ndio tukio baya zaidi la vifo uwanjani katika bara la Afrika. Tukio lilitokea mwishoni mwa mechi kati ya Hearts of Oaks na Kumasi, ambapo mashabiki wa Kumasi walipopatwa na hasira kufuatia timu yao kufungwa, na kuanza kuvunja viti, kuvirusha na kurusha vitu vingine kama chupa.

Polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi na hapo ndipo mwanzo wa kukanyagana na kusababisha vifo hivyo.

1: Mwaka 1964: Peru - vifo vya mashabiki 320

Peru

CHANZO CHA PICHA,DAILYSTAR

Hili linatajwa kuwa tukio baya zaidi kuwahi kutokea uwanjani na kusababisha vifo vya watu 320 na wengine zaidi ya 1,000 kujeruhiwa.

Lilitokea Mai 24, 1964, katika uwanja wa taifa katika mji mkuu wa Peru, Lima - ingawa vitu vingi kuhusu tukio hilo havikuwekwa wazi sana, idadi ya vifo ilitikisa dunia.

Ikiikaribisha Argentina, Peru ilikuwa nafasi ya pili kwenye kundi lake kutoka Amerika Kusini kwa ajili ya kufuzu michuano ya Olimpiki.

Walikuwa na imani zote. Wakati wakiisubiri Brazil katika mchezo wa mwisho, Peru ilikuwa inata sare tu dhidi ya Argentina ifuzu. Argentina ilitangulia kupata bao katika uwanja uliokuwa na mashabiki zaidi ya 53,000, zaidi ya 5% ya wakazi wote wa Lima wakati huo.

Lakini utata wa bao la kusawazisha, kukataliwa baada ya mpira wa kurushwa kuzuiwa na Kilo Lobaton na kuzama langoni , mashabiki wa Peru 

Friday, 7 October 2022

Tume ya maadili kuchunguza tuhuma za ufisadi Kenya

 Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini Kenya imesema inazifuatilia kaunti 24 kutokana na tuhuma za kuendeleza ufisadi wa kiwango cha juu.

    
Kenia | Amtseinführung Präsident William Ruto

Tume ya EACC inafuatilia matukio ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi katika kaunti 24 kati ya kaunti 47 nchini. Ripoti iliyotolewa na Tume inayosimamia mgao wa fedha na raslimali za umma nchini Kenya imeeleza kuwa serikali za kaunti zimekuwa zikipoteza mabilioni ya pesa kila mwaka kutokana na ufisadi pamoja na mifumo isio thabiti. Mwenyekiti wa tume ya EACC Eliud Wabukhala anasema :

"Tume ya EACC inatathmini hatari ilioko kwenye vitengo mbali mbali vya serikali za kaunti. Tumefanya hivyo kwenye kaunti 24 kufikia sasa.Tumegundua changamoto hizo na tukatoa ushauri kwa mianya hiyo kuzibwa, ndiposa tuweze kuokoa pesa za umma.”,alisema Wabukhala.

Tume ya EACC vilevile ina jukumu la kuchunguza na kushauri wizara, idara na kampuni za umma.

Wakati huo huo, baraza la magavana nchini limetoa wito kuwa Rais William Ruto kuagiza hazina kuu kusambaza fedha zilizotengewa serikali za kaunti kufikia jumatatu wiki ijayo.

''Hali ilivyo sasa kwenye kaunti zote 47 nchini inahuzunisha''

Kenia wartet mit Spannung auf das Urteil des Obersten Gerichtshofs zu den Wahlen

Mwenyekiti wa baraza hilo Anne Waiguru amesema kaunti zote nchini hazina pesa, na kwamba huduma na miradi muhimu imekwama. Waiguru ambaye pia ni Gavana wa kaunti ya Kirinyaga, amesema serikali za kaunti zinaidai serikali ya kitaifa shilingi billion 51.7 ya miezi ya Agosti na Septemba, na wanatarajia fedha zingine shilingi bilioni 29.6 za mwezi wa Octoba.

"Hali ilivyo sasa kwenye kaunti zote 47 nchini inahuzunisha. Inasikitisha kwamba awamu ya tatu ya uongozi wa kaunti nchini inaanza bila raslimali muhimu. Tungependa kuujulisha umma kuwa, katiba ya Kenya pamoja na sera ya fedha ya mwaka 2012 imeratibu kwamba fedha zilizotengewa serikali za kaunti zinapaswa kusambazwa kwa kaunti hizo kila tarehe 15 ya mwezi bila kuchelewa.”, alisema Waiguru.

Itakumbukwa pia kwamba Rais William Ruto alipoingia mamlakani aliiondoa wizara ya ugatuzi iliyokuwa inashughulikia maswala ya kaunti. Hii inaacha pengo katika namna kaunti zinavyofadhiliwa, na baraza la magavana limetoa wito kuwa Rais Ruto kuagiza wizara ya fedha kuwezesha usambazaji wa fedha zilizotengewa serikali za kaunti.

Ushirikiano wa taasisi

Aidha, malumbano kati ya mabunge mawili, bunge la seneti na bunge la kitaifa yameifanya vigumu kutekeleza mifumo na sera inayofaa katika ukaguzi wa raslimali za kaunti. Spika wa bunge la Seneti Amason Kingi aliahidi kuzika uhasama huu katika uongozi wake.

Mwenyekiti wa EACC Eliud Wabukala amehimiza ushirikiano kati ya mabunge ya serikali za kaunti na tume yao ili kufanikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.

Baraza la Haki la UN kumteua mchunguzi huru dhidi ya Urusi

 Schweiz Genf | Sitzung UN-Menschenrechtsrat

Baraza hilo la Haki za binadamu lenye wanachama 47 limepasisha pendekezo hilo lililowasilishwa wiki iliyopita na nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya isipokuwa Hungary. Muda mfupi kabla ya kupiga kura hiyo huko mjini Geneva, Shirika la kutetea haki za binadamu la Russia Memorial lilitajwa kuwa mshindi mwenza wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka huu wa 2022.

Pendekezo la awali lilidhihirisha wasiwasi kuhusu kufungwa kwa wingi kwa vyombo huru vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na makundi ya upinzani nchini Urusi. Wanachama walio wengi wa Baraza hilo waliafiki kuteuliwa kwa "kamati maalum" itakayoendelea kufuatilia matukio ya ukiukaji wa haki nchini Urusi, kwa kutegemea kwa kiasi fulani msaada kutoka kwa makundi ya wanaharakati wa urusi ambao bado wapo nchini humo na hata nje ya nchi.

Soma zaidi:Umoja wa Mataifa kuamua juu ya uchunguzi Ukraine 

Urusi ambayo ilikuwa mwanachama wa Baraza la Haki za binadamu hadi mapema mwaka huu kabla ya kujiondoa kwake,  imechukua hatua kadhaa za kufifiza upinzani wa ndani kutokana na vita vyake nchini ukraine, ikiwa ni pamoja na kupitisha sheria inayopiga marufuku kueneza habari "za uongo" kuhusu jeshi la Urusi. 

Soma zaidi: Urusi yasimamishwa uanachama baraza la haki za Binaadamu la UN

Idadi ya vifo Zaporizhzia yaongezeka

Ukraine | Raketenangriff auf Saporischschja

Vikosi vya zima moto vya Ukraine vikijaribu kuuzima moto baada ya shambulio huko Zaporizhzhia mnamo Oktoba 6, 2022, moja mwa matukio ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Idadi ya waliofariki kutokana na shambulio la makombora katika eneo la makazi huko Zaporizhzhia imeongezeka na kufikia watu 11 huku kwa mara ya kwanza kabisa, ndege zisizo na rubani na zilizobeba vilipuzi zimefanya mashambulizi katika mji huo wa kusini mwa Ukraine na ambako kuna kinu kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi hayo:

" Urusi imeshambulia tena kwa makombora. Kwa bahati mbaya, kuna vifo, watu waliojeruhiwa, na majengo yaliyoharibiwa. Huko Zaporizhzhia, baada ya shambulio la kwanza la roketi, wakati watu wakiondoa vifusi, Urusi ilifanya shambulio la pili la roketi. Ni uovu na ukatili wa hali ya juu. Kumekuwa na maelfu ya matukio kama haya. Na kwa bahati mbaya mengine zaidi huenda yakashuhudiwa

WAKIMBIZI ETHIOPIA WAPEWA HIFADHI

 Afrika Nahrungsmittelspende Church World Service Organisation in Marsabit

Huku makali ya kiangazi na ukame yakiendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya  Pembe ya afrika, idadi ya wahamiaji wanaotafuta chakula inaendelea kuongezeka katika eneo la Uran mpakani mwa Kenya na Ethiopia.

Familia zipatazo mia nne kutoka Ethiopia tayari zimevuka na kuingia upande wa kenya na kwa sasa zinahifadhiwa na wakaazi wa eneo la Uran.  Asili mia themanini ya wahamiaji hao ni akina mama na watoto ambao wamekuwa waathiriwa wakubwa wa baa la njaa.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa mkutano wa wadau wa kupambana na majanga jimboni Marsabit,mratibu katika shirika la World Vision Jarso James Galgallo ,amesema kuwa,kuna haja kwa serikali na wadau wengine kushikana mkono kuwasaidia wahamiaji hao ambao kwa sasa wanaishi katika mazingira duni.

"Kati ya familia mia tatu hamsini na mia nne wametoroka kwa sababu wameathirika na njaa.Mifugo waliokuwa nao wamekufa na sasa katika ile hali ya kujiokoa,wamekuja upande huu.”

''Mifugo wetu huelekea eneo la Ethiopia''

Kenia Marsabit Dürre Dromedar

Afisa huyo amesema kuwa,kuna haja ya mashirika ya kijamii kuwapa wahamiaji hao msaada, ikiwemo malazi na vyandarua vya kujikinga.

Serikali ya kaunti ya Marsabit imekiri kuwa na ufahamu kuhusu wahamiaji hao eneo la uran na kwamba imekuwa ikitoa msaada wa chakula japo hautoshi kwa wakaazi wenyewe.

Katibu wa serikali ya kaunti Ibrahim Adan Sora amesema wafugaji wamekuwa wakihamahama kutafuta malisho kwa mifugo wakati ambapo malisho yamepungua kutokana na hali mbaya ya ukame.

"Kwa sasa,tuna watu wengi eneo la Uran na hili ni kutokana na uhaba wa lishe na chakula.Hata sisi,mifugo wetu huelekea eneo la Ethiopia …”

Serikali ya kaunti aidha,imeeleza kuwa,maafisa kutoka shirika la kimataifa la kuwashugukikia wahamiaji IOM wanatarajiwa kuzuru eneo la Uran wanakohifadhiwa wahamiaji hao kabla ya kuchukua hatua zaidi.

Marsabit imeendelea kuripoti hali mbaya ya ukame huku maelfu ya wafugaji wakiendelea kuhamia katika majimbo Jirani kuokoa Maisha ya mifugo yao wakati huu

Tuzo ya Amani ya Nobel 2022 yawaendea wanaharakati wa haki za binadamu


Washindi wa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu ni mwanaharakati wa haki za binadamu Ales Bialiatski kutoka Belarus, Shirika la haki za binadamu la Memorial la nchini Urusi na shirika la uhuru wa kiraia la Ukraine.Mwenyekiti wa kamati inayosimamia tuzo hiyo ya amani yenye makao yake Norway Breit Reiss-Andersen ametangaza hayo leo mjini Oslo Norway.Tatyana Glushkova ambaye ni mwanachama wa bodi ya shirika la haki za binadamu la memorial la Urusi lililoshinda amesema tuzo hiyo ni uthibitisho kuwa kazi yao ni muhimu ulimwenguni.Reiss-Andersen amewaambia waandishi wa habari kwamba washindi hao wamefanya juhudi kubwa za kurekodi visa vya uhalifu wa kivita, ukiukwaji wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka.Maafisa wa Ulaya wamewapongeza washindi kwa kutetea haki za binadamu na demokrasia Urusi, Belarus na Ukraine.Baadhi ya viongozi waliotoa pongezi zao kwa washindi ni rais wa ufaransa Emmanuel Macron na mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg.

Friday, 3 January 2020

TANGAZO LA KUTANGAZA BISHARA YAKO KATIKA WEBSITE YETU


LIOS MEDIA
+255 756258193 whatsup
+255 788822683

KWA TZS 20000/=UTATANGAZIWA BISHARA YAKO 
NDANI YA WEBSITE NA KWENYE YOUTUBE CHANNEL

YOUTUBE LIOSMEDIA
Email liosmediatz@gmail.com
KATIKA  HIYO EMAIL AU NAMBA YA WHATSUP 
TUMA MATANGAZO YAKO YA BIASHARA YAKO HAPO
NA PIA KATIKA NAMBA HIZO TUMA PESA YAKO BAADA YA
KUTUMA TANGAZO LAKO

Yuor lifted to Lift others

TANGAZO

KWA YEYOTE YULE ULIYE NA TANGAZO LAKO LA BIASHARA BASI USISITE KUTANGAZA NASI IWE NI KAMPUNI AU MTU MMOJA MMOJA TUANAPOKEA MATANGAZO YA KILA AINA NA BEI ZETU NI NAFUU SANA AMBAPO UTATANGAZIWA KUPIA KATIKA WEBSITE YETU NA KWENYE CHANNEL YETU YA YOUTUBE 
KWA SHILING 20000/= KWA MWEZI YAANI NDANI YA WEBSITE PAMOJA NA KWNYE YOUTUBE CHANNEL YETU

KWA WALE WALIOKO MBALI YAANI NJE YA MKOA WA MBEYA TUMA TANGAZO LAKO HWATSUP UKIWA UMELIEDIT VIZURI PAMOJA NA NAMBA ZAKO NA SHUGHULU UNAYOIFANYA KATIKA TANGAZO LAKO 

LIOS MEDIA
+255 756258193 whatsup
+255 788822683
Email liosmediatz@gmail.com
KATIKA  HIYO EMAIL AU NAMBA YA WHATSUP 
TUMA MATANGAZO YAKO YA BIASHARA YAKO HAPO
NA PIA KATIKA NAMBA HIZO TUMA PESA YAKO BAADA YA
KUTUMA TANGAZO LAKO.

HABARI

Fahamu matukio matano mabaya zaidi viwanjani yaliyoua mamia ya watu

  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Raia wa Indonesia wanataka majibu ya moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya mchezo huo duniani, baad...